Faza James: Tufikirie tunavyoweza kuelimishana namna sahihi ya kufanya maombi ya ajira, tuliwatoa 50% ya waombaji bila kuangalia CV au vyeti

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
Anaandika Faza James,
_______________________
Wiki iliyopita nilipata nafasi ya kuchakata maombi ya kazi ya taasisi moja binafsi hapa nchini. Maombi takribani 450 yalipokelewa ya wahitimu wa vyuo mbali mbali.

Ninashauri tufikirie namna tunavyoweza kujipanga na kuelimishana namna sahihi ya kufanya haya maombi ya ajira. Yapo makosa madogo madogo yaliyofanya tuwatoe katika ushindani takribani 50% ya waombaji wote bila hata kuangalia CV au vyeti vyao.

Baadhi ya makosa nikiyoyaona ni kama ifuatavyo;

1. Emails nyingi zilitumwa bila heading. Yani email haisemi ni ya nini. Au mtu anaandika "Application", au anaandika "My cv", au "dear sir". Hayo yote ni makosa. Kwa kawaida unapaswa kuandika title ya email yako in a Title cased format ikitaja nafasi unayoomba. Kwa mfano "Application for Tutorial Assistant in Mathematics"

2. Emails nyingi zilizokosewa title. Yani title na kilichomo ni tofauti. Mtu ameandika "Application for Tutorial Assistant in Mathematics" lakini ukifungua barua yake ya maombi ameomba nafasi ya Estate Manager. Mara nyingi hutokea ikiwa ofisi imetangaza nafasi zaidi ya moja.

3. Kulikua na "blank emails". Yani mtu ametuma email akasema "please see the attachments" lakini hajaambatanisha attachment hata moja.

4. Kuna mtu ametuma email yenye attachments tu bila kuandika chochote sehemu ya ujumbe. Hilo ni kosa. Andika sentensi mbili au tatu. Kwa mfano "Dear sir/Madam, please see my attached credentials applying for the Tutorial Assistant post"

5. Weka attachment ulichoelekezwa tu. Kama mwajiri anataka CV na Cover letter usiattach certificate unless awe anataka na certificate pia. Na hata ukiambiwa attach certificate weka zile za muhimu tu. Sio unaweka cheti cha primary, cha ubatizo au Living certificate ya form four/six.

6. Attachments zote lazima uzipe majina kabla ya kuattach. Mfano cv inatakiwa isomeke Peter Elia CV - Tutoria Assistant Post au vinginevyo ili mradi mtu akiidownload asihitaji kulazimika kui-rename. Elewa kwamba waombaji ni wengi na anayefungua hizo attachment ni mtu mmoja au wawili. Fanya maisha yake yawe mepesi. Hakuna mtu ana muda wa kufungua attachment yako na kuirename wakati wapo walioattach kwa kuzipa majina attachment zao.

7. Poor scanned documents. Tuache uvivu usiscan taarifa za kutumia simu ya mkononi. Andaa copy nzuri ya nakala ya vyeti vyako tumia scanner nzuri, na ikiwezekana save kabisa kwenye "email" yako ili siku yoyote ukivihitaji uvipate.

8. CV format. Kuna watu wanafanya utani na CV zao. Yani unakutana na CV ina font size tofauti kila section, font types tofauti, spelling errors hadi kwenye majina yako. Hapa ukikosa kazi huna wa kumlaumu.

9. Usitumie majina tofauti na yaliyopo kwenye vyeti vyako. Kama vyeti vyako vimeandikwa Peter Elia Mosha usiandike Peter Elia au Peter Mosha. Hao ni watu wawili tofauti.

10. Acha kutumia email uliyofungua ulipokuwa "teenage" enzi ukiwa na miaka 16. Unakuta mtu anaitwa Peter Elia lakini email yake ni snakeboy@yahoo.com. Tengeneza email yenye majina yako na isajili kwa majina yako balisi. Kwa mfano peterelia@gmail.com

11. Usitumie email ya mtu mwingine kutuma maombi. Tuache uzembe. Yaani kama natafuta mtu mmoja kati ya watu 450 niambie kwa nini nimchukue mtu ambaye hata hana email address?

12. Epuka kuchanganya herufi. Hata kama lafudhi katika kuandika kwa usahihi. Mfano hela - ela, asubuhi - asubui. Sasa hivi wana mtindo mpya wa xa badala ya sa. Na hawakubali kurekebishwa. Mwisho wa siku utasikia "my wangu nimekutumia ujumbe mpaka xaxa ujanijibu"
_____
TAKE A SERIOUS NOTE. Maombi ya kazi ni jambo serious sio mambo ya JOMONI.!
 
Mkuu Mungu akubariki sana kwa bandiko hili murua, yaani nina vijana wangu tunagombana kila siku kuhusu haya haya uliyosema but hawanielewi kabisa. Yaani email address eti hachizoboy@gmail.com, CV mpaka nawaandikia, unakuta eti ameweka mpaka primary school wakati nimewaunganishia sehemu za kujitolea na wamefanya zaidi ya 6 months...
 
Muongozo mzuri lakini makosa hayo yanavumilika na kurekebishika,nachokiona ni ajira hakuna na wahitaji ni wengi Ndio maana mnaangalia Mpaka Nukta na mikato.

Enzi ajira zikiwepo unatoka chuo unakuta Unaitwa kila mahali bila kuandika barua, yani barua utaandika tu as formality ukiwa umeshakula Mishahara kadhaa
 
...Yapo makosa madogo madogo yaliyofanya tuwatoe katika ushindani takribani 50% ya waombaji wote bila hata kuangalia CV au vyeti vyao.
.............................................................................................................................................................................
8. CV format. Kuna watu wanafanya utani na CV zao. Yani unakutana na CV ina font size tofauti kila section, font types tofauti, spelling errors hadi kwenye majina yako. Hapa ukikosa kazi huna wa kumlaumu.
...bila kuangalia CV, halafu unakutana na CV...
 
Mkuu thank you so much for this thread.

Nadhani HR Managers wanaweza kutuletea makosa mengine yanowafanya watu wasiwe shortlisted for interview

Lets make this a learning thread for the young generation.

Mfano makosa niliyoyaona

1. Mtu anakosea tarehe kwenye barua ya kuomnba kazi, eg. kazi imetangazwa May, 2020 barua yake kaandika April or March 2020

2. If possible attach all your documents in a single PDF file and name it as advised by Faza James

3. Make your CV short and readable, possibly 4 pages

4. Check your grammar on your application, If possible ask your colleagues to read and correct it
 
Muongozo mzuri lakini makosa hayo yanavumilika na kurekebishika,nachokiona ni ajira hakuna na wahitaji ni wengi Ndio maana mnaangalia Mpaka Nukta na mikato.

Enzi ajira zikiwepo unatoka chuo unakuta Unaitwa kila mahali bila kuandika barua, yani barua utaandika tu as formality ukiwa umeshakula Mishahara kadhaa
Hii ndio point ya msingi mkuu.
 
Mkuu thank you so much for this thread.

Nadhani HR Managers wanaweza kutuletea makosa mengine yanowafanya watu wasiwe shortlisted for interview

Lets make this a learning thread for the young generation.

Mfano makosa niliyoyaona

1. Mtu anakosea tarehe kwenye barua ya kuomnba kazi, eg. kazi imetangazwa May, 2020 barua yake kaandika April or March 2020

2. If possible attach all your documents in a single PDF file and name it as advised by Faza James

3. Make your CV short and readable, possibly 4 pages

4. Check your grammar on your application, If possible ask your colleagues to read and correct it
Hakuna binadamu aliyekamilika kwa 100%
 
Unakuta umejikunja kuandaa docs. hizo kwa usahihi kabisa afu hakuna hata historia ya kuwa shotlisted, Ndugu yaku mkuu sijui saizi kuna njia nyingine ishatoka? Vipi una uelewa na connection either long/short or penetration passes?
 
Asante kwa elimu hii mkuu, lakini ikiwa ndio mnaangalia makosa yote hayo ni ngumu sana kupata mtu ambaye hana kosa kati ya hayo yote uliyoyataja.
 
PAGEPATROL

Pagepatrol Tunatoa huduma za Editing, Proofreading And Translations.

Editing and proofreading in terms of.
Research
paper,Journals,Thesis,Articles, contract,Essay writings etc.

Translation in terms of;
Germany, English,French and Swahili.

Gharama zetu ni kwa bei nafuu Sana.

Editing and proofreading @ page Tzshs1000/=

Translation @ page Tshs 10,000/=

Pia Tunatoa huduma za kuandika

Barua za aina zote Kama vile
Application letter, scholarship letters etc. Kwa gharama nafuu kabisa Tshs 15,000/=

Pia Tunatoa huduma za kuandika CV kwa gharama nafuu Kabisa 20,000/=

Tunapatikana :

Chuo Cha CBE dar es salaam
Bibi titi Road
Kituo Akiba ( unapita mnazi mmoja )
Tupo Mkabala na chuo cha DIT

Kwa mawasiliano:.
Contact Person (Mr Mahali)

WhatsApp 0767316144

Telephone no: 0714316144/0784507548

Karibuni Sana wote mnakaribishwa
 
Back
Top Bottom