Mtabiri
Senior Member
- Jun 23, 2009
- 152
- 5
HIFADHI ya Wanyamapori ya Wamimbiki, mkoani Morogoro, iwashikilia watu wanne wakiwa na gari la serikali lenye namba STJ 9587, kwa tuhuma za kutumiwa katika shughuli za ujangili.
Watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakiwa ndani ya hifadhi hiyo iliyoko katika Wilaya ya Mvomero,wakiwa na wanyama saba aina ya swala na kudai kuwa walitumwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatuma Mwassa. Habari zaidi:
Gari la serikali lakamatwa katika ujangili
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Mwananchi Newspaper
9/7/2009

Watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakiwa ndani ya hifadhi hiyo iliyoko katika Wilaya ya Mvomero,wakiwa na wanyama saba aina ya swala na kudai kuwa walitumwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatuma Mwassa.
Kaimu Meneja wa Mradi wa Wamimbiki,Abubakar Msonde, aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni, pamoja na Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Thadeus Macha.
Hali kadhalika Benard Mlengela ambaye ni dereva wa gari la Idara ya Misitu mkoani Morogoro,Abdalah Jumanne mkazi wa mji mpya na Salum Muya, wote ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro.
Akizungumzia tukio hilo,Msonde alisema watu hao wakiwa na gari la serikali, walivamia Hifadhi ya Wamimbiki na kuua wanyama hao.
Alisema hata hivyo wakati wakijiandaa kuondoka, gari lao lilipata pancha na hivyo kulazimika kutafuta usafiri mwingine, ili kusafirisha nyama hizo.
Alisema wakati wakiendelea na harakati hizo, askari wa hifadhi hiyo waliwakuta na kuwaweka chini ya ulinzi na kwamba baada ya kuwahoji walidai kuwa walitumwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.
Hata hivyo dereva wa teksi ambalo watu hao walilitumia kubeba nyama hizo, akititumia gari lenye namba T 767 AQX ,Mohamed Said alidai kuwa alikodishwa na Macha kupeleka nyama hizo kwa mkuu wa wilaya.
Dereva huyo alidai kuwa watu hao walimkabidhi mkuu huyo wa wilaya swala saba.