Fatuma Mwasa anajihusisha na Ujangiri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fatuma Mwasa anajihusisha na Ujangiri?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtabiri, Sep 8, 2009.

 1. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HIFADHI ya Wanyamapori ya Wamimbiki, mkoani Morogoro, iwashikilia watu wanne wakiwa na gari la serikali lenye namba STJ 9587, kwa tuhuma za kutumiwa katika shughuli za ujangili.

  Watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakiwa ndani ya hifadhi hiyo iliyoko katika Wilaya ya Mvomero,wakiwa na wanyama saba aina ya swala na kudai kuwa walitumwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatuma Mwassa. Habari zaidi:

  Gari la serikali lakamatwa katika ujangili

  Na Mwandishi Wetu, Morogoro
  Mwananchi Newspaper

  9/7/2009


  HIFADHI ya Wanyamapori ya Wamimbiki, mkoani Morogoro, iwashikilia watu wanne wakiwa na gari la serikali lenye namba STJ 9587, kwa tuhuma za kutumiwa katika shughuli za ujangili.

  Watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita wakiwa ndani ya hifadhi hiyo iliyoko katika Wilaya ya Mvomero,wakiwa na wanyama saba aina ya swala na kudai kuwa walitumwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Fatuma Mwassa.

  Kaimu Meneja wa Mradi wa Wamimbiki,Abubakar Msonde, aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni, pamoja na Afisa Maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Thadeus Macha.

  Hali kadhalika Benard Mlengela ambaye ni dereva wa gari la Idara ya Misitu mkoani Morogoro,Abdalah Jumanne mkazi wa mji mpya na Salum Muya, wote ni wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

  Akizungumzia tukio hilo,Msonde alisema watu hao wakiwa na gari la serikali, walivamia Hifadhi ya Wamimbiki na kuua wanyama hao.

  Alisema hata hivyo wakati wakijiandaa kuondoka, gari lao lilipata pancha na hivyo kulazimika kutafuta usafiri mwingine, ili kusafirisha nyama hizo.

  Alisema wakati wakiendelea na harakati hizo, askari wa hifadhi hiyo waliwakuta na kuwaweka chini ya ulinzi na kwamba baada ya kuwahoji walidai kuwa walitumwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.

  Hata hivyo dereva wa teksi ambalo watu hao walilitumia kubeba nyama hizo, akititumia gari lenye namba T 767 AQX ,Mohamed Said alidai kuwa alikodishwa na Macha kupeleka nyama hizo kwa mkuu wa wilaya.

  Dereva huyo alidai kuwa watu hao walimkabidhi mkuu huyo wa wilaya swala saba.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndio hivyo tena kila ng'ombe anakula kwa urefu wa kamba yake. NDio maana nilishawahi kutanabahisha kuwa ili kila mwananchi afaidike ni vyema nchi ikauzwa kila mtu akapewa chake kuliko hivi sasa wenye visu vikali ndo wala nyama.
   
 3. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mh ila hilo wazo lako kaka linatia shaka!
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  si walikuwa na gari ya serikali sasa wamekasa nini waacheni inawwezewkana walitumwa na wakubwa kufanya hujuma ila najua wataogopa kuwataja....
  ''Mvumilivu hula mbivu.....ila mvundika mbivu hula mbovu''
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280

  Ghafla utasikia mkuu wa hifadhi amehamishwa au ofisa aliyehusika kuwakamata ghafla kupisha upelelezi ambao hautazaa matunda!!!!
   
 6. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Hao walioshikwa na nyara hizo waulizwe vizuri na watatoa maelezo yatakayopelekea kujua ukweli wa jambo hilo...Na kama ni kweli mzigo huo ulikuwa wa DC iwekwe wazi..DC Mwassa ni mtu wa karibu sana na Mkuu wa nchi,alifanya kazi katika ofisi ya communication Ikulu kwa muda,kabla ya kuwa Msaidizi Maalumu wa Mama Salma na baadaye mwaka jana kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya.

  Imeandikwa kuwa watu hao walikuwa wanatumia gari la serikali (STJ 9587) na kutaja wazi kuwa Mzigo huo ni mali ya DC Mwassa,sidhani kama Wanyama hao walikuwa ni kwa ajili ya kitoweo,na pia kuna utaratibu wa vibali vya uwindaji...Ofisi ya DC inatakiwa itoe maelezo ya kina kuhusu hujuma hiyo......inawezekana ikawa ni hali ya kawaida kwa Viongozi wetu kufanya uwindaji wa namna hiyo mara kwa mara,Idara ya wanyamapori inatakiwa iangalie kwa ukaribu uwindaji huo haramu.
   
 7. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Inaonekana watu kweli hawako informed na masuala ya conservation. Maliasili mnageuza kama shamba la bibi?
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa kawaida mtu yeyote akitaka kuwinda ni lazima apate kibali cha maliasili na kununua wanyama anaowahitaji kisha kupewa askari mmoja wa wanyama pori kwenda katika shughuli hiyo.

  Haya mambo ya kuingia na kuua wanyama bila utaratibu si tu kwa mkuu wa wilaya bali ni hata juu, watu wenye madaraka wanaona kuwa kwa kutumia majina yao wanaweza kuvunja utaratibu na sheria. Umefika wakati sasa hili liishe.
   
 9. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Halafu wana harakati wa mazingira vitu kama hivi wala hawavipigii kelele. Sijui kama wanaogopa hawa watu au vipi. NGO za jinsia na haki za binadam wanajitahidi sana kushikia bango issue za area zao. LEAT mpo wapi? JET mpo wapi? na wengine wengi wengineo. Saidieni ktk kupata ukweli wa jambo hili. Environment na biodiversity ya bongo ni mtaji wa kujivunia bana. Hatuwezi kukubali watu kuziharibu kirahisi namna hiyo. Hivi mheshimiwa alipopita kwenda Ruaha National park that time angeenjoy nini kule bila wanyama? Au kila mtu akivuna wanyama atakavyo tutakua na mbuga za wanyama/hifadhi kweli?
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Shaka iko wapi?
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  Sep 8, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hamtaki DC ale nyama pori wajameni? anyway, huo ndo utarataratibu wa viongozi wetu,wala sitegemei jipya hapo, tulie tuuuuu!
   
Loading...