Fatma Karume ni mwanasheria asiyezifahamu sheria

Jul 10, 2017
22
33
FATMA KARUME NI MWANASHERIA ASIYE ZIFAHAMU SHERIA.
SAKATA LA USHOGA LIMEWASAIDI WATANZANIA KUFAHAMU UWEZO WA KISHERIA WA FATMA KARUME.
.
Nimesoma maandiko kadhaa ya mwanasheria Fatma Karume, Kwa wale wasiomfahamu vizuri Fatma Karume ni mjukuu wa muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibari,
Fatma ni miongoni mwa Watanzania na Wazanzibar wachache mno waliolelewa na kukulia maisha mazuri kwa kupata kila wakitakacho.

Fursa alizopata Fatma zilimuwezesha kusoma kwa kadri ya uwezo wa Akili yake sio uwezo wa fedha za mzazi au mlezi kama ambavyo watanzania wengine na Wanzanzibar walipata, hivyo kushindwa kwa Fatma kuwa Professa au Daktari kielimu ni kutokana na uwezo mdogo wa Akili yake, Kwa kuthibitisha hili unaweza kulinganisha na Watanzania wengine wenye uwezo mkubwa wa Akili kama Dkt John Pombe Joseph MAGUFULI ambaye amefanya vizuri sana kwenye Masomo yake ya Sayansi mpaka kupata Udaktari katika Elimu yake akitokea katika Familia ya kawaida kabisa na Prof Ibrahim Haruna LIPUMBA ambaye amefanikiwa kupata Uprofessa wake katika masuala ya UCHUMI akitokea kwenye Familia ya kawaida mno..

JE TANZANIA HAKUNA SHERIA YA KUKATAZA USHOGA.?
Katika Andiko lake Mtoto wa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibari na Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) ambaye pia ni PRIVATE ADVOCATE Bi, Fatuma Karume amesema
NANUKUU,

'' Tena nitawatetea Homosexuals, Maana ni binadamu kama sisi. Na Amber ana haki ya kutumia mwili wake anavyotaka, Sodomy between two consenting adults canot possibly be crime for goodness sake, Manchueia sheria za Uingereza mnazitumia bila kujua historiu.''
Kwanza suala la kuwatetea kwangu siwezi kusema ni kosa kwa kuzingatia shughuli zake kama wakili (ADVOCATE) Lakini nipingana na yeye wazi wazi kuhusu kueleza kwamba hakuna sheria ya kukataza USHOGA .

Kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1954 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1998 kifungu 154 (1) (a) Anae muingilia mtu yoyote kinyume cha Maumbile au. (b)Anaemuingilia mnyama kimwili au(c) Anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile , Atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini.''

Sasa Mtoto aliyekulia IKULU Zanzibar Fatuma Karume aka Shangazi mwenyewe hupenda sana kujiita ''Am lawyer'' kashindwaje kufahamu kwamba sheria hii ipo na ni katazo kwa mujibu wa sheria zetu?

Lakini kwa mujibu wa sheria zetu Tanzania sio tu kufanya kitendo cha USHOGA hata kujaribu pia ni kosa Kifungu cha 155 '' Mtu yoyote ambaye atajaribu kutenda kosa mojawapo katika makosa yaliyotajwa katika kifungu 154 atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika na adhabu ya kifungo kisichopungua miaka ishirini''

Hapa Amber unaesema utamtetea hakujaribu bali kaingiziwa na kakiri na kuomba msamaha watanzania kabla hata ya kukamatwa, hovyo kifungu cha 155 hakimuhusu maamna yeye katenda hakujaribu, Fatuma Karume wewe sasa ni mwanasheria gani usiejua sheria hizi?
Kwa mujibu wa sheria zetu jambo hilo la USHOGA hata kama likifanywa kwa kificho ikibainika ni kosa Kifungu 157 '' mwanaume yoyote ambaye iwe hadharani au katika faragha anatenda kitendo chochote cha aibu pamoja na mwanaume mwingine au anafanya mwanaume mwingine kufanya kitendo hicho na yeye au anajaribu kufanya kitendo hicho na mwanaume yeye mwenyewe au mwanaume mwingine, Iwe hadharani au katika faragha, mwanaume huyo atakuwa ametenda kosa na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka mitano.''

Hizi ni kati ya sheria nyingi zinazokataza matendo yanayompendeza Shangazi Fatuma Karume anasema Amber anayohaki ya kutumia mwili wake atakavyo Lakini sheria zetu zinakataza na sio hivyo tu hata kufanya mapenzi kuna taratibu zake Mfano kifungu 158 (1) ''Mwanaume yeyote ambaye amekatazwa kufanya ngono na mwanamke yeyote ambaye anamjua kuwa ni mjukuu wake, Binti yake Dada yake au mama yake, mwanaume huyo akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atastahili adhabu''

Hapa sheria imeona kwamba wapo watu wanaweza kuwa na Akili kama ya Fatuma Karume na Amber wakaamua kufanya ngono na watoto wao au kaka zao kwa kile anachokiita Fatuma Karume uhuru wa kuutumia mwili wake apendavyo au kwa kile anachosema kwa nia njema (goodness sake).

MALEZI YA FATUMA KARUME NA KINACHOTOKEA LEO.

Waswahili husema "mwana kioo cha mzazi". Yaani matendo na maneno na maandishi ya mtoto yana reflect makuzi. Ndio maana waswahili wana msemo mwingine wa " mwana umleavyo ndivyo akuavyo". Fatuma Karume Baba yake mzazi kahudumu IKULU ya Zanzibar na Kaka yake wa mama na Baba mmoja Aman Abeid Karume kahudumu pia IKULU ya Zanzibar kwa miaka kumi, Kaka yake mwingine Ali Abeid Karume ni Balozi katika nchi mbalimbali.

Sasa wengi tumemsoma na kumsikia Fatuma Karume. Huyu hakupitia shida za kimaisha kama wengi wetu. Ni msomi mwanasheria. Fatuma ni mwislamu. Tena Mtoto Wa Alhaji na Hajra. Ungetegemea Fatuma aelewe vizuri machukizo na makatazo ya kitabu kitukufu cha Quran kuhusu zinaa na matendo ya kinyume na maumbile. Isitoshe kwa nafasi yake kama Rais Wa TLS ungetegemea Fatuma aongoze katika kujua sheria za nchi hazikubali alichokishabikia,

Rais Wa TLS ni rais Wa kujua sheria! Sio rais wa kujua uchafu na upuuzi,Fatuma wetu yoote haya katupa kapuni. Ndio tunajiuliza huyu Fatmua ana wazazi au haya ndio malezi kutoka kutoka IKULU ? Tunashindwa kujiuliza ana mume na watoto maana hatujasikia akiwatambulisha. Tuna assume ni msela! (Atatusamehe kama tumekosea). Ila tuna uhakika ana wazazi. Tena sio wazazi Wa kawaida! Ni wazazi Wa matawi ya juu.

HEBU TUULIZE MASWALI HAYA KIGODO.
Je ni wazazi Wa namna gani waliomzaa Fatma?

Je wazazi hawa walimlea vyema Fatma ? Nadiriki kusema hawakumlea vyema! Wanafiki wengi watajifanya kuwatetea! Hakika wazazi wa Fatma wangekuwa hohehahe watu haohao wangesema hakupata makuzi mema. Tunaona kwa kina WEMA SEPETU. Mama anashambuliwa hakumlea Mtoto vizuri. Na ni kweli! Waswahili hawakuwa wajinga kusema Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo! Wala hawakusema "Mtoto Wa masikini umleavyo"! Lakini kwa kuwa binadamu wengi wanafiki kwa huyu FATMA wazazi hawaguswi!

Hivi wazazi Wa Fatma hawasomi wala hawasikii kauli za mtoto wao kuhusu ushoga? Wanakubaliana naye? Hivi walipoenda Makkah hawakumuahidi Mola wao Leo wanasikia mtoto wao anashabikia ushoga hadharani wao kimyaaaa?!!!

Ili tuamini ni mtoto kakataa kufuata makuzi na mafundisho mema ya wazazi hebu na watokee hadharani wamuonye mtoto wao!! Mtoto wao hakujificha au hakushabikia ushoga kimyakimya! Katoka hadharani mchana kweupee na kuuthibitishia ulimwengu anaupenda ushoga. ?

MASWALI KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA.
Na BAAVICHA, JUV-CUF na UVCCM mko wapi? Ninyi si ndio vijana? Mnakubaliana na FATMA? Kazi yenu nini haswa kama mnashindwa kumkemea FATMA kwa uhimiza ushoga? Au mndhani kazi yenu ni siasa tu? Hebu tusiie matamo yenu ili vijana nchi nzima wajue FATMA kakosea.
Umoja wa wanawake wa CCM, CDM, CUF ACT- Wazalendo Tanzania mtoto wa kike kanena mnayakubali? Mbona kimya?

ZILE NGO'S ZA KUITUKANA SERIKALI KILA LEO MKO WAPI.
Hivi ina TNGP, Jukwaa la Katiba, TAMWA na wengine mmefurahi? FATU amewakilisha msimamo wenu? Hebu tuwasiie mkilaani basi. Sio kila siku kelele tu mnaacha jambo kubwa hivi lipite!

VIONGOZI WA KIDINI NINI MSIMAMO WENU.
Na nisimalize bila kuwageukia viongozi wa kidini! Nyie ni viongozi Wa kiimani kweli? Ni kwa nini MTU katamka hadharani kushabikia mambo yanayomchukiza mungu na nyie mko kimya utadhani katangaza neno la mungu? Tunataka tusikie matamko yenu. Sio kukimbilia kutoa nyaraka za kichochezi mnaacha maadili yanaharibiwa kiasi hiki. Hivi kina zaidi ya hili liloshabikiwa na Fatma?
Au na nyie mmo?

Hongera sana Paul Makonda! Walau wewe umeonyeshwa kukerwa kwa sababu dini zote zinakataza haya maovu...nashangaa huyu ambae sio muislamu imemkera ambae ana jina la kiislam na ni muislam anaushabikia
 
Wakati mwingine ukumbuke na msemo wa wahenga,
"Ndugu wakigombana chukua jembe kalime, wakipatana chukua kapu kavune".

Kwan umeona sehemu wahenga wanasema uwashabikie?, uwasuluhishe, uwakosoe?
 
Kwa haraka haraka naona Fatma is very right and she know what she stands for. Kuna nchi moja niliitembelea nikaona umalaya uliokithiri. Nilipowauliza kulikoni wakasema prostitution is prohibited by the law, but it is highly tolerated in the society. Nadhani ndio maana hata Waziri wetu serialism haina mpa go watch kupambana na mashoga ili hali katiba yetu imekataza.
 
Kwa Zanzibar Sheria ya kupinga ushoga ilikuwepo miaka ya 1800+
 
Makasuku kwenye ubora wenu weka namba ya simu upate teuzi
 
Ujinga ni kwamba umeacha kujibu hoja zake umeanza kumchambua yeye. Ndiyo maana waTanzania wachache mno ndiyo wenye uwezo wa kuandika hoja kwenye mitandao inayojulikana dunia nzima.

Hata mimi nilipinga hoja ya Fatma lakin niliipinga kwa sheria ambayo ilisema nikaishia hapo.

Sasa ikulu, kaka yake ni balozi, baba alhaji, mama hajra vinatoka wapi?
 
Back
Top Bottom