Father Titus Amigu: Unaweza kuishia na ndoa ya Facebook na Instagram

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,338
4,672
Katika Ukurasa wake Wa Facebook,Fr.Titus Amigu amekuwa akifundisha vijana kwa mambo mbalimbali ya kijamii,Kiuchumi, kiutamaduni na kiroho.Hii ni makala yake akiwausia wale wote wanaokusudia kuanzisha taasisi ya ndoa.Basi fuatana naye hapa chini kwa mada yake hii juu ya uwezekano kuambulia " ndoa za mitandaoni" ikiwa hutazingatia mambo muhimu katika kuchagua mchumba:

Vijana lazima mjichunge sana katika ujana wenu, la sivyo, MTAAMBULIA NDOA YA WHATSAPP, FACEBOOK AU INSTAGRAM TU. Kama fainali yenu ni uzeeni, basi nusufainali yenu haiko mbali sana: MAISHA YA NDOA.

Namaanisha nini? Naamaanisha linapokuja suala la kuoana watu huchunguzana sana. Vyeti feki havifai katika suala hilo. Akinakaka au wanaume huhitaji kupata wenzi ambao watakuwa wasaidizi wa kufaa maishani mwao na hali kadhalika akinadada au wanawake. Kwa maisha ya ndoa ya kudumu, mwanaume anamhitaji dada au mwanamke atakayeweza kuwa msaidizi wake, mkewe na mama watoto wake (Mwa 2:18. 21-24, 3:20). Kifupi, anamhitaji mwanamke anayeweza kuwa mke na mama.

Hali kadhalika, mwanamke anamhitaji kaka au mwanaume anayeweza kuwa mume na baba. Ndiyo maana wakati mwingine huchukua muda kuchunguza, kuulizia ulizia na hatimaye kuamua kumteua mmoja kati ya akinadada au wanawake wengi au kati ya akinakaka au wanaume wengi.

Acha nianze na akinakaka na wanaume. Kwa kuwa kaka au mwanaume hapendi kujibebesha mzigo wa matatizo huku akijua, hapendi amchague tangu mwanzo dada au mwanamke fulani ambaye ni mgonjwa (mfano, mwenye tabia ya kulialia, mwenye kuanguka anguka, anayejulikana kuwa na mapepo, mwenye kuweweseka, anayeumwa skizofrenia, “multipersonality”, hofu iliyopitiliza mipaka [Greneralized Anxiety Disorder], kichaa, tahaira, mwenye maradhi sugu, asiyeweza kuzaa [tasa], mwenye kilema kikubwa n.k.) au mwenye tabia mbaya (kwa mfano, domokaya, sakubimbi. mwongo, mwizi, kiruka njia, mhuni, mvuta bangi, asiyeambilika, mvivu, asiyejua kupika, asiyeweza kufanya usafi nyumbani, asiyeweza kuosha nguo na vyombo, asiyejua kupiga pasi, mchafu, asiyeweza kumtengea mume maji ya moto, asiyeweza kutandika kitanda, aliyewahi kufamaniwa, mwenye watoto wasiojulikana baba zao na kadhalika).

Hivi, wewe, dada au mwanamke unayekusudia kupata bwana na kudumu katika ndoa chunga sana afya yako na tabia yako. Nakusihi sana acha kudekeza magonjwa ya kujidekeza kama kulialia na kuanguka anguka. Narudia, magonjwa ya kujidhalilisha kama ya kuangukaanguka eti una mapepo, kulialia, kuweweseka na kadhalika yakimbie “kama ukoma”. Na kama umedanganywa na kuingia chama au kikundi cha kulialia na kuangukaanguka jitoe kwa haraka kabisa maana umeweka rehani kuolewa kwako. Ninatakuambia kwa nini. Yaani, umejianzishia safari kwa mguu wa kushoto! Yaani umejilambisha garasa.

Hebu nikutafakarishe kidogo. Nani akuoe wakati unajionesha tangu mwanzo kwamba wewe ni mgonjwa? Je, ukianguka siku ya harusi? Je, ukianguka mbele za wakwe? Je, siku moja ukianguka kutoka kitandani? Je, mume atapata faida gani utapokuwa unatumia muda mwingi “kutolewa” hayo mapepo yako? Utapika lini? Utafanya kazi za nyumbani saa ngapi wakati wewe unaanguka anguka ukidai umepagawa na mapepo, au “majini” kadiri wewe mwenyewe unavyopenda kukopa teolojia ya Waislamu? Utawatunzaje watoto? Hakika magonjwa kama hayo yanakutoa kabisa kwenye orodha ya mabinti au wanawake wa kufikiriwa kuolewa. Labda akutake “mgonjwa mwenzio”.

Tabia mbaya vile vile ni shimo lako lingine. Kama umezama humo toka kwa haraka ukitaka kuingia katika soko la kutafuta kuolewa. Uvivu utakuponza kabisa. Tafakari. Kwa nini ulie kuosha sahani? Kwa nini ulie kufua nguo? Kwa nini usifanye usafi wa nyumba yako mwenyewe? Kwa nini usipike chakula cha mumeo na watoto wako? Nakubia siri moja , mume hupenda sana kuoshewa nguo na mkewe, hali kadhalika kula chakula kilichopikwa vizuri na mkewe.

Vitu kama hivyo uonesha na huchagisha upendo wa ndoa. Kaidi ulimwengu ukufunze kwa milele. Na tena, ole wako umtumaini “binti wa kazi”, kama hujui, kwa jambo hilo, utakuwa umebinafsisha ndoa yako mwenyewe. Ukipigwa talaka au kupinduliwa na “binti wako wa kazi” usimlaumu mumeo, utakuwa umefanya ujinga mwenyewe! Usinishangae. Si kwamba nina mdomo mbaya, au ninataka kukutisha, hapana, isipokuwa ndivyo inavyokwenda.

Kwa magonjwa kama hayo ya kujidekeza na tabia mbaya, hutachumbiwa. Kama ukichumbiwa mchumba anaweza kughairi hata kabla ya harusi. Kama utaolewa, utaolewa kwa ajali. Kama utaolewa kwa ajali, ukweli wa kwamba hufai kuolewa utafichuka punde si punde. Hapo ndipo utakapokuwa umepiga picha ya Whatsapp, Facebook au Instagram, lakini mara ukaachika. Nakwambia “kutokufaa kwako” kutabainika nawe hutakawia kuachwa, na mume atakuwa akijilaumu kujitwisha mzigo kama wewe. Kumbe, jihadhari kabla ya mkasa huo wa kuachika mara.

Hali kadhalika, kwa tabia yako mbaya, yatakufika madhila hayo hayo. Mtu mwongo kwa nini uolewe? Umdanganye nani maisha yote? Mtu mvivu, sawa na ukanda wa nailoni, akuoe nani? Nani anapenda kujibebesha mzigo huku akijua? Kwani unadhani kuolewa ni harusi tu? Hapana, kuolewa ni kukaa na mume na kusaidiana kuijenga na kuilea familia. Mtu huwezi hata kupika, huwezi hata kupiga deki nyumba yako mwenyewe, huwezi kutandika hata kitanda, huwezi hata kumtengea mumeo maji ya kuoga, mtu huwezi kufua nguo za kuvaa hata na shuka, mtu huwezi kupiga pasi nguo za mumeo wala na zako, akutake nani kama mwenzi wa maisha?

Hufai. Kwa kweli “huna CV” ya kukufanya ufae kama mke wala mama wa kudumu. Kumbe, wewe ni mtu wa “kukudate” kwenye “kucheza singeli” na kupiga nawe picha za kurusha kwenye Whatsapp, Facebook au Instagram tu.

Narudia, wewe ufai kuolewa kwa kudumu! Waulize akinakaka au wanaume wote, kama hawatakuonea haya watakwambia ninayokuambia. Kumbe ikiwa utaolewa na bwana ambaye hakukujua sawasawa, ndiyo mtafunga ndoa yenu kwa “matarumbeta’ na mbwembwe lakini kutokufaa kwako kutafichuka punde si punde, kwa maana “pembe la ng’ombe halifichiki”. Mambo ya jubilee ya ndoa miaka ishirini na tano au hamsini utasimuliwa na watu tu. Kwa nini? Kwa sababu utaachwa kwa spidi ya mwanga.

Sasa hapo itakuwa umeambulia nini ikiwa umeolewa kwa saa chache au kwa majuma machache tu? Bila shaka, utakuwa umeambulia hiyo hiyo picha ya Whatsapp, Facebook au Instagram. Halafu ukumbuke, ukishavurunda hivyo maishani, shida yako ya kuanguka anguka itapamba moto nawe utamaliza makanisa yote ukitafuta kuombewa na utaingia vyama na vikundi vyote vya maombezi na kulialia na hivyo kujizamisha zaidi kwenye matatizo.

Utakuwa siku zote unaruka majivu na kukanyaga moto. Utaeleza sababu ya kutoolewa kwako kwa kila aina ya jawabu: “Oh nimerogwa!”, “Oh nimelaaniwa na maneno ya bibi!”, “Oh nimeolewa na pepo!”, “Oh kuna watu wananionea kijicho!”, “Oh nyota yangu imefungwa!”, “Oh nahitaji ibada ya kufunguliwa!”, “Oh ninahitaji kukata mti wa ukoo”, “Oh nahitaji kuombewa”, “Oh nahitaji maombezi yenye upako kutoka kwa mtu mwenye upako”, Oh nahitaji kwenye kumwona Nabii Joshua huko Nigeria”, “Oh nahitaji kujiunga na Karismatiki!” na kadhalika. Yote hayo wapi na wapi. Utakuwa umesahau “ulivyolikoroga”. Utakuwa umesahau ulivyoyadharau maneno kama haya ya kwangu. Utakuwa unalalamikia guu lililovunjika baada ya kukataa kuyasikia ya wakuu. Utakuwa unavuna mabua baada ya kujizoeza kumchekea nyani!

Ndipo hapo hapo hapo utakapotumiwa kama shamba na mjanja yeyote anayeishi kwa “kula vya wajinga”. Wapo watakaokuaminisha ukinyonywa maziwa nuksi itakuondoka. Wapo watakuaminisha, hata wengine wasioolewa wenyewe, kwamba ukiwa mwamini katika kanisa lao nawe ukawa unatoa michango minono kwa bidii, Mungu atakuletea mume wa maisha yako na kadhalika. Kwa njia hii utaliwa kila ulicho nacho nawe utakuwa mweupe kama “msaga unga mashinine” kwa manung’umolp na kufilisika kimwili na kiroho. Hiyo imani yako ya kutowagutukia wanaokudanganya, itakufikisha pabaya. Usisahau kuna wachungaji na mapadre wengine wamegeuza ile methali ya “Wajinga ndio waliwao” na kuwa “Wenye imani ndio waliwao”. Kumbe, nakusisitizia, hutatulia mpaka ujirekebishe mwenyewe. Basi, binti yangu na dada yangu, jiepushe kabla ya ajali.

HAYA NINAYOYASEMA KWA AKINADADA NA WANAWAKE, napenda uyageuzie kwa akinakaka na wanaume. Akinadada na wanawake, hata kama wenyewe ni wagonjwa au watu wa tabia mbaya, hawawapendi akinakaka au wanaume wagonjwa au watu wenye tabia mbaya vile vile. Ni ajabu lakini ni kweli. Kila dada na mwanamke humtafuta “mwanaume wa nguvu” yaani yule anayeweza kumpatia pasipo shida mahitaji yake yote (pesa, nguo, vipodozi, mafuta ya kujipaka, wigi, viatu vya kila sampuli, pesa za kutumia, pesa za mahitaji ya nyumbani na kadhalika). Nakwambia humtafuta mwanaume anayetoka jasho (Mwa 3:17-19) na hivyo anayeweza kuwa mume na baba wa familia yake tarajiwa. Hivi hawezi kuthubutu kumteua mwanaume mgonjwa mgonjwa au mwenye tabia mbaya tangu mwanzo. Kwa nini? Kwa sababu kaka au mwanaume wa namna hiyo hana “CV” ya kufaa kama mtafutaji, mume na baba.

Kifupi, hafai au hana sifa. Ikiwa dada au mwanamke fulani ameangukia kwenye mikono ya kaka au mwanaume mwenye maradhi ya kutisha, mvivu au mwenye tabia mbaya ya kutisha “atakaa mkao wa kuondoka tu”. Dada au mwanamke huyo, punde si punde atajua aliyemteua “ana vyeti feki”.

Nakutafakarisha, kaka umelegealegea kama uji wa ngano, nawe unaweweseka na kuangukaanguka kama nini sijui, yaani eti na wewe una mapepo nani akubali kuishi nawe kwa kudumu! Kama una fedha, “bora uchunwe” na kisha kukimbiwa. Wa nini mtu kama wewe kwa maisha ya kudumu katika ndoa fulani? Kijana au mwanaume mwoga kama kunguru, hata ukimwona nyoka unakimbia kama mwanariadha, mvivu wa kufa hata “chipsi” unakula za kupewa, nani akubali kuolewa nawe? Sioni haya, naongeza mifano unielewe vizuri zaidi. Tazama, kaka au mwanaume mwongo kama umechanjiwa dawa, mtu mwizi kama mashine, mtu mlafi kama gari mkweche, au mlevi kama kisima cha zamani, mtu jeuri kama unalalia magunia ya pilipili, wa nini wewe? Ndiyo kwa ujanja wako wa kiuanaume unaweza kuoa tena hata binti mbichi tu, lakini ujue hujachaguliwa kwa kudumu. Kuna mawili mwenzi wako ama hakujui sawasawa au anakujua lakini anataka kukutumia kama ATM au “buzi la kuchuna” tu.

Ndiyo kisa dada au mwanamke aliyekubali kuolewa nawe, saa na siku yoyote, anaweza kugeuzwa “nyumba ndogo” na kaka au mwanaume yoyote atakayejionesha kuwa bora kuliko wewe. Ni balaa kweli, lakini ndivyo mambo yanavyokwenda. Ndiyo kisa kwa hali hii ya mambo, mwanaume anayejitutumua na kujionesha anaweza kumudu kuwapa mahitaji akinadada au wanawake na kujinasibu kuweza kuwa mume na baba wa nguvu anaweza kuwaoa wanawake hata mia moja. Hujasikia habari za mitara yenye wake wengi hivyo?

Kama hujasikia pole, lakini itembelee mitandao ujijuze kidogo. Kumbe, kwa niliyokueleza usiniulize tena anawezaje mwanaume fulani kuwapata akinadada au wanawake wengi kama hao. Anawapata wote hao kwa sababu anajitutumua na kuwaaminisha akinadada na wanawake kwamba anaweza kuwa kwao mwanaume, mume na baba. Kumbe, jiepushe na “CV” isiyofaa kwa ndoa ya kudumu, UTAAMBULIA NDOA YA WHATSAPP, FACEBOOK AU INSTAGRAM TU.

Kumbe, usijilishe hasara ya mwaka, au hasara ya maisha yako mwenyewe “gangamala” kijana wangu. Walio kwenye miito (upadre na utawa) wana sababu nyingine, sababu ya juu (higher reason) ndiyo KUJITOA SADAKA KWA AJILI YA JINA LA YESU NA UFALME WA MUNGU, kama hujawa katika miito hiyo usijiponze mwenyewe kwa magonjwa ya kujidekeza na tabia mbaya.

Badala yake jipatie CV nzuri kusudi uolewe au uoe na kujipatia ndoa yenye heshima na ya kudumu. Kwa heri na kibwagizo changu. Kisome tena kama hujanipata uzuri!

Source: Ukurasa wa Facebook/Fr.Titus Amigu.
 
Anazungumziaje tabia ya kuabudu sanamu ?

af553ac9eafcb6e6c19ed1c12210adf3.jpg
 
Kanisa Katoliki hudai kufanya badiliko la siku ya ibada kutoka Jumamosi (siku ya 7) kwenda Jumapili, siku ya kwanza ya juma.
Kuhusu siku ya Jumapili, Kanisa Katoliki hudai kuwa:
“Sunday is our mark of authority… The [Catholic] Church is above the Bible, and this transference of the Sabbath observance is a proof of that fact” (Catholic Record, Sept. 1, 1923).
“Jumapili ni chapa yetu ya mamlaka … Kanisa [Katoliki] linayo mamlaka yaliyo juu zaidi ya Biblia, na kitendo hiki cha kuhamisha uadhimishaji wa Sabato ni uthibitisho wa ukweli huo” (Catholic Record, Sept. 1, 1923).
Na bado linadai kushikilia msimamo huu hadi leo. Toleo la 1977 la Katekismo ya Waongofu ya Mafundisho ya Wakatoliki (The Convert's Catechism of Catholic Doctrine) lina mfululizo huu wa maswali na majibu:
“Swali: Sabato ni siku gani?
“Jibu: Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
"Swali: Kwa nini tunaadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi?
“Jibu: Tunaadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki lilihamisha utukufu kutoka Jumamosi kwenda Jumapili” (Peter Geiermann, The Convert's Catechism of Catholic Doctrine (Rockford, IL: Tan Books and Publishers, 1977), uk. 50.
BIBLIA INASEMA
Daniel 7:25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati

ROMANI KATOLIKI INAPOTEZA MAELFU YA WATU
 
Toleo la 1977 la Katekismo ya Waongofu ya Mafundisho ya Wakatoliki (The Convert's Catechism of Catholic Doctrine) lina mfululizo huu wa maswali na majibu:

b058dd8765da8f783102d680e6e65ff9.jpg
 
Unataka kuelewa au kubadilishwa kutoka usabato?
 
Sio Kweli,kuna ongezeko kubwa la Waumini sijapata kuona, Jimbo nililopo juzi tu kulikuwa na Parokia 19,hivi sasa zimefikia 26,sasa utasemaje kuwa linapoteza Waumini ???. Believe me kuna WASABATO Wengi waliohamia huku RC. Hiyo ni baada ya kujua kuwa Ellen White alikuwa anawahadaa.
 
Unataka kuelewa au kubadilishwa kutoka usabato?
Kutoka katika CATHOLIC ENCYCLOPEDIA,
Gombo la IV, ukurasa 153, "Kanisa... baada ya kuibadili siku ya mapumziko kutoka Sabato ya
Wayahudi, au siku ya saba ya juma, kwenda siku ya kwanza, likaifanya amri ya tatu
kumaanisha Jumapili kuwa ndiyo siku itakayotakaswa kama Siku ya Bwana."
3cc9a1da8848ac6b3c00b57bd7cc45ba.jpg
 
Sio Kweli,kuna ongezeko kubwa la Waumini sijapata kuona, Jimbo nililopo juzi tu kulikuwa na Parokia 19,hivi sasa zimefikia 26,sasa utasemaje kuwa linapoteza Waumini ???. Believe me kuna WASABATO Wengi waliohamia huku RC. Hiyo ni baada ya kujua kuwa Ellen White alikuwa anawahadaa.
Kutoka katika CATHOLIC ENCYCLOPEDIA,
Gombo la IV, ukurasa 153, "Kanisa... baada ya kuibadili siku ya mapumziko kutoka Sabato ya
Wayahudi, au siku ya saba ya juma, kwenda siku ya kwanza, likaifanya amri ya tatu
kumaanisha Jumapili kuwa ndiyo siku itakayotakaswa kama Siku ya Bwana."
 
Toleo la 1977 la Katekismo ya Waongofu ya Mafundisho ya Wakatoliki (The Convert's Catechism of Catholic Doctrine) lina mfululizo huu wa maswali na majibu:
“Swali: Sabato ni siku gani?
“Jibu: Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
"Swali: Kwa nini tunaadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi?
“Jibu: Tunaadhimisha Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu Kanisa Katoliki lilihamisha utukufu kutoka Jumamosi kwenda Jumapili” (Peter Geiermann, The Convert's Catechism of Catholic Doctrine (Rockford, IL: Tan Books and Publishers, 1977), uk. 50.
b058dd8765da8f783102d680e6e65ff9.jpg
Siyo Kweli. Huo ni Uzushi.
 
Siyo Kweli. Huo ni Uzushi.
Kutoka katika CATHOLIC ENCYCLOPEDIA,
Gombo la IV, ukurasa 153, "Kanisa... baada ya kuibadili siku ya mapumziko kutoka Sabato ya
Wayahudi, au siku ya saba ya juma, kwenda siku ya kwanza, likaifanya amri ya tatu
kumaanisha Jumapili kuwa ndiyo siku itakayotakaswa kama Siku ya Bwana."

BISHA NA HII NI KITABU CHAO WAKATOLIKI, UKIBISHA NALETA KINGINE KAANDIKA PADRI WA HAPO PERAMIHO,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom