Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,443
Hivi kuna nini huko FastJet? Tulitarajia kwamba walipoongeza ndege kutoka tatu hadi sita tunazoambiwa, ufanisi wao ungeongezeka hata zaidi, lakini sasa ni matatizo hata zaidi. Wanazidi kuwa ATC ya enzi zile za kila safari kucheleweshwa au kuahirishwa kimoja.
Nasikia siku hizi wamekuwa wakali sana kwenye nauli - wanatafuta kila namna kukulipisha penalty kwenye ticket. Na of course hakuna kuahirisha safari au kurudishiwa nauli kama huwezi kusafiri. Ukiahirisha safari utaambiwa fee ya kuahirisha lazima iwe zaidi ya nauli uliyokatia tiketi.
Katika kipindi cha siku kama kumi zilizopita FastJet wamekuwa na matatizo mengi na haya ni kati ya yale ninayoyaelewa mie. Huenda wengine nao wamekumbwa na matatizo mengine wanayoweza kusimulia.
Jumanne iliyopita wali-cancel safari ya Nairobi Dar wakidai "operational problems". Na ni baada ya abiria kulalamika ndipo wakawapeleka kwenye hoteli moja ndogo pale Nairobi. Siku saba kabla ya hapo safari ya kutoka Kilimanjaro kuja Dar ambayo kawaida ni ya saa tatu usiku ilicheleweshwa hadi saa tano na nusu usiku.
Kisha wiki iliyopita siku ya Jumatano waliamua - ku cancel safari ya asubihi ya Dar - Kilimanjaro na kuchanganya abiria wa asubuhi na wale wa mchana. Kama hiyo haitoshi, pilot akatanganza kwamba kwa kuwa kila siti ya ndege imekaliwa na abiria ambao walionekana ni wanene sana, basi asingebeba begi hata moja kwa kuwa ndege ingezidiwa uzito na injini zingeshindwa. Hivyo pilot aliogopa ndege kuanguka, na ndege ikaenda Kilimanjaro na abiria lakini bila begi hata moja!
Hivi hakuna chombo kinachodhibiti usafiri wa ndege (regulator) Tanzania ili abiria wasinyanyaswe na kuibiwa na mashirika kama haya?