Nasikitika sana kueleza kuwa Kitengo cha Huduma kwa Mteja au Customer Care FASTJET hakitoi hutuma bora kwa wateja. Leo nimepiga simu yao na ikapokelewa lakini majibu niliyokuwa napewa na Mhudumu (Binti) sio kabisa. Anaongea kama kalazimishwa na anakuwa mkali kama vile anaongea na houseboy wake. Hii tabia si nzuri na endapo atapatikana Mshindani wa Fastjet si ajabu wakapoteza wateja wengi ikiwemo mimi ambaye ni Regular Traveller.
Kwa masikitiko makubwa nimeona heri niliweke hili suala wazi ili pengine Uongozi uchukue hatua. Hili limetokea leo tarehe 21/04/2016. Tabia hii ni mbaya sana na inakera mnooo. Ukiwa kazini fanya kazi nyodo ziache mtaani.
Nawasilisha