GE2025 Faris: Octoba 29 hakuna mende hata mmoja atabaki kabatini

GE2025 Faris: Octoba 29 hakuna mende hata mmoja atabaki kabatini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera, ndugu Faris Buruhani ameendelea kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge kwenye kata na majimbo mbalimbali ya mkoa wa Kagera, huku akiendelea kusisitiza na kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuwachagua wagombea wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi, ili kurahisisha upatikanaji wa maendeleo kwenye maeneo yao.

Akiwa katika jimbo la Karagwe, kata ya Nyabiyonza kwenye ufunguzi wa kampeni za Mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM, amewaomba wananchi wa Karagwe tarehe 29 Octoba 2025 kwenda kusafisha kabati na kuhakikisha hakuna mende hata mmoja atakaebaki kabatini.

Kwahiyo wakuu, sisi wananchi ndio mende au? Aliyeelewa anieleweshe🤔

Pia Soma: GE2025 - Mwenyekiti UVCCM Kagera: Maneno tumepita bila kupingwa yanaweza kuwa sumu kupunguza kura za Chama chetu
 
Kuna haja ya kujipanga vema ule usiku wa kuwmkia 29 wenyeviti na Makatibu wote wa ccm na jumuiya zake ktk ngazi ya Shina, mitaa na kata wapumzishwe mahala pema. Halafu 29/10 wawe bize kuomboleza
 
Kinachofurahisha sasa hivi hawasemi kuhusu uchaguzi zaidi ya kuhutubia mandamano safi sana sasa kila mtu anahuburi Mandamo tutaelewana tu
 
Back
Top Bottom