tourist2020
Member
- Feb 2, 2017
- 13
- 17
Hivi karibuni kumekuwepo na katazo la kuzuia wafanya kazi walioachishwa kazi kuchukua pesa zao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kigezo cha umri kuwa lazima awe amefikisha umri wa miaka 55.
Lazima wajue kuwa kuna watu ambao huwa wanafanya kazi za mkataba mfu pengine mwaka mmoja au miwili sasa huyu mtu akikosa kazi mda mrefu au hata akiamua kujiajiri inamaana atakaa mpaka afikishe miaka 55 ndio akachukie hiyo hela?
Huu ni uonevu tena mkubwa sana lazima hii sheria ipitiwe upya ili kutofautisha wafanyakazi wenye ajira za mda mfupi na wale wenye ajira za kudumu.
Kinachoniuma zaidi ni kuwa hata kwenye bunge ambalo linaendelea kwa sasa hilo swala wameliweka kando hatujui mpaka lini.
Wako wapi wawakilishi wetu tulio wachagua kwenda kutuwakilisha BUNGENI kimya chenu kinatutia shaka na wasiwasi mkubwa au mnasubiri watu waandamane ili muwapige virungu?