Fao la kujitoa NSSF

Fao la kujitoa NSSF

Scofied

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2012
Posts
2,456
Reaction score
1,685
wakuu heshima kwenu....kama kuna mtu humu jamvini aliye nssf am aye anaweza nifanyie mpango nipate fao langu haraka iwezekanavyo anipm tuongee Dili....natoa ofa ya 500000 kwa atakayefanikisha...me nipo Arusha.
 
Unapo acha kazi na ukapanga kupata mafao yako ndani ya mwezi 1 au 2.Bila kuhonga Kaa ukijua unamiezi 5 na kuendelea.Yaan mafao yako yanaonekana kama ni hisan au msaada!Sio rahis kujua ninacho andika mpaka yakukute.....
 
kaka umeeleza ukweli kabisa yani, na mimi nakaribia kufuatilia ila wenzangu walioanza wameshaanza kuzungushwa, mtu kaambiwa aende mwezi wa 6, hapo ni baada ya kwenda zaidi ya mara 3.
 
du!, TUTAITOKOMEZA RUSHWA KWELI KWA MTINDO HUU, YAANI MTU HAONI HATA AIBU. FUATA TARATIBU ZOTE ZINAZOTAKIWA UTAPATA PESA YAKO HIYO NI HAKI YAKO HUITAJI KUHONGA.
 
du!, TUTAITOKOMEZA RUSHWA KWELI KWA MTINDO HUU, YAANI MTU HAONI HATA AIBU. FUATA TARATIBU ZOTE ZINAZOTAKIWA UTAPATA PESA YAKO HIYO NI HAKI YAKO HUITAJI KUHONGA.

baba hayajakukuta. ukifuata taratibu utazingushwa mpaka yesu arudi.
 
wakuu heshima kwenu....kama kuna mtu humu jamvini aliye nssf am aye anaweza nifanyie mpango nipate fao langu haraka iwezekanavyo anipm tuongee Dili....natoa ofa ya 500000 kwa atakayefanikisha...me nipo Arusha.

Eti laki 5 au ulikusudia elfu 50 .. mm nimefatilia baaada ya kukamilisha all documents ilinichukua mwezi ...
 
wakuu heshima kwenu....kama kuna mtu humu jamvini aliye nssf am aye anaweza nifanyie mpango nipate fao langu haraka iwezekanavyo anipm tuongee Dili....natoa ofa ya 500000 kwa atakayefanikisha...me nipo Arusha.

Ndugu yangu sikupi namba yoyote ingawa ninazo, ila nakushauri nenda kafungulie Dar es salaam katika kimojawapo ya vituo vya NSSF e.g Ilala (BAVARIA HOUSE) wapo opposite na Shoprite PUGU Road, au Nenda pale Mlimani City, ukweli hawakuombi chochote na within two weeks pesa yako unapata na huo ndio ukweli bila kuweka fitina za mitaani jamaa wapo safi na nimewahi waeelekeza jamaa zangu wengi tu na hakuna aliyenung'unika, sikatai huko mikoani yawezekana kwani wapo mbali na makao makuu na huenda wamejisahau na kuwa waomba rushwa
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Watanzania tunashida sana ya kupenda short cut..
Binafsi nilikuwa Mdau wa NSSF na nimeshachukua fao langu la kujito, Siwezi kukubali kwamba kuna usumbufu kwani nilipojitoa sikutoa hata senti 5 na wala sikuwahi kuonana na mtu yoyote Kiufupi niko Dar es salaam na niliposubmit document zangu tawi la kinondoni op Mlimani city waliniambia 30 days wataniwekea hela yangu bank, baadaya ya siku 22 nikapokea sms ya mtego inasema hivi, " Mr Jubilant ni mimi ........natarajia kukuwekea mafao yako bank leo...Sikuijibu hiyo sms, na kweli baada ya 24 hours nikaenda bank account yangu ilikuwa imejaa na kufurika....

Nakushauri kabla ya kujitengenezea mazingira yatakayo kusumbua na kukumalizia hilo fao lako fuata taratibu utafanikiwa bila usumbufu wowote...

Huwezi amini rafiki yangu alijitoa akatafuta short cut kweli hela ilitoka baada ya 14 days ila walimla milioni 1....Tafakari na chukua hatua
 
baba hayajakukuta. Ukifuata taratibu utazingushwa mpaka yesu arudi.
sio kweli mimi ni mmoja wa wanufaika wa fao la kujitoa. Ukiwa na kiherehere utaliwa hela zako na bado fedha yako utaipata kati ya miezi sita mpaka kumi.
 
Mimi nilikuwa PPF nilifuata steps zote vizuri na nilipokea hela ndani ya mwezi, so acha short cuts
 
Samahan wapendwa naomba kufaham hiv mtu anapo fungua madai nssf kuna sehem anajaza bank acount swali langu ni je pesa inapotoka huwekwa moja kwa moja kweny bank akaunti ya mteja au kuna ulazima wa hadi urudi tena nssf kuchukua cheque?
 
unapewa cheque ukadeposit mwenyew kwenye bank ac yako..
 
Samahan wapendwa naomba kufaham hiv mtu anapo fungua madai nssf kuna sehem anajaza bank acount swali langu ni je pesa inapotoka huwekwa moja kwa moja kweny bank akaunti ya mteja au kuna ulazima wa hadi urudi tena nssf kuchukua cheque?

Kwa kawaida unatakiwa ufuate hundi ikitoka. Lakini pia unaweza andika barua ya kuomba wakuwekee kwenye akaunti yako. Bila barua ni lazima ufuate hundi yako.
 
usumbufu wa hawa jamaa husababishwa na yafuatayo, inabidi ukafungue madai katika tawi lile ambali mwajiri alikuwa anapeleka michango yaani hawako centralized ......huduma kwa wateja hili ni tatizo la kitaifa....hakikisha hufanyi kazi popote pengine wakati unapeleka madai yako kwani ni kinyume cha sheria na watagundua kwani wameajiri wapelelezi chungu nzima....hi njo kesho njo kesho nadhani huwa wanapeleleza au mifuko inakuwa haina hela kifupi hii mifuko ni janga
 
Asanteni wakuu kwa majibu mazuri maana niko mbali na nilikofungua madai
 
Hiyo laki tano tununulie juice ya azam na korosho wote tuliosoma mada yako na kukupa mchango Wa mawazo kuliko kwenda kumhonga mtu.
 
Tunaomba NSSF Arusha badilikeni Jamani hii sasa too much Jamani dah! Watu kila kona wanalia walioacha kwa Ugonjwa shida waliofukuzwa wanataka rudi makwao mikoani mpaka basi aiiiiibu ata wew??????
 
Back
Top Bottom