Fao la kujitoa lazidi kuwindwa

UKAWA2

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2014
Posts
2,182
Reaction score
1,972
SSRA yaja na mbadala wa fao la kujitoa


Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa SSRA, Ansgar Mushi

WAKATI fao la kujitoa likiendelea kujadiliwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imependekeza kuanzishwa kwa fao mbadala la upotevu wa ajira.

Fao hilo litatolewa kwa wafanyakazi waliopoteza ajira kwa njia ya kufukuzwa kazi au kupunguzwa kazini lakini si kwa wale walioamua kuacha kazi wenyewe.

Pia mamlaka hiyo, imebainisha kuwa hadi sasa takribani wafanyakazi milioni 23 kati ya wafanyakazi milioni 25 waliopo kwenye sekta rasmi ya ajira ambayo ni sawa na asilimia 91.2 hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Utafiti na Sera wa mamlaka hiyo Ansgar Mushi, wakati akiwasilisha mada kuhusu dhana ya hifadhi ya jamii na changamoto ya wanachama kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, katika semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.

Alitaja sifa za fao hilo la ukosefu wa ajira kuwa ni pale mwanachama atakapothibitika kufukuzwa kazi au kupunguzwa kazi, mfuko utampatia asilimia 33 ya mshahara wa mfanyakazi huyo kwa kipindi cha muda wa miezi sita.

“Ila masharti ya fao hili, litatolewa pekee kwa mfanyakazi aliyechangia kwa kipindi cha miezi 18 kwa wale waliochangia kwa chini ya miezi 18 watapewa asilimia 100 ya kile walichochangia,” alisema Mushi.

Alisema sifa nyingine ya fao hilo, halitoathiri mafao ya pensheni ya mfanyakazi ikiwemo mafao mengine yanayotolewa na mifuko ya jamii kama vile, fao la elimu, uzazi, matibabu na ulemavu.

Alisema fao hilo la upotevu wa ajira halitatolewa kwa mfanyakazi aliyeacha kazi mwenyewe kwa kuwa kwake itakuwa si janga linalohitaji msaada kama ilivyo dhana nzima ya uanzishwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Tafiti zetu zinaonesha takribani asilimia 78 ya wafanyakazi wanaoomba fao la kujitoa wengi ni wataalamu wakubwa kwa maana ya kuwa na uwezo wa kuendelea na kazi sehemu nyingine. Wengi wao wanaacha kazi huku wakiwa na mikataba ya ajira sehemu nyingine, wanaomba fedha hizi tu kwa ajili ya shughuli nyingine,” alisema.

Mushi alisema lengo la kuanzishwa kwa mifuko ya jamii kwa mujibu wa sheria na Katiba ni kumlipa mafao mfanyakazi wakati wa uzeeni ili kumrahisishia maisha yake katika kipindi hicho ambacho hawawezi kujiingizia kipato.

Hata hivyo, alisema athari za fao la kujitoa ni nyingi ikiwemo mfanyakazi kukosa fursa ya kupata mafao ya muda mfupi kama vile, uzazi, elimu, ulemavu na ugonjwa, kupoteza sifa ya kupata mafao ya pensheni na kukosekana kwa ukwasi katika mifuko ya hifadhi ya jamii na hivyo kushindwa kulipa mafao kwa wafanyakazi wengine wanaostahili.

“Katika fao la kujitoa, mfanyakazi akishalipwa mafao yake ndio anakuwa ameondolewa kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii hata akizeeka au kupata janga lolote mfuko haumtambui. Ofisi yangu imekuwa ikipokea wafanyakazi wengi tu takribani 34,000 waliopewa fao hilo la kujitoa sasa wanaomba warejeshwe,” alisisitiza.

Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa mamlaka hiyo Honorius Njole alisema bado fao hilo katika hatua ya mjadala na halijapitishwa wakati pia mjadala kuhusu fao la kujitoa ukiendelea kwa kupokea maoni.

Alisema katika kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii, SSRA imeanzisha miongozo 14 tangu kuanza kwake kazi mwaka 2008, ikiwemo miongozo ya ukomo wa gharama za matumizi ya mifuko hiyo, mwongozo wa usajili wa wanachama na utunzaji wa kumbukumbu au taarifa za mwanachama.

Miongozo mingine ni wa kuhamia mfuko wowote wa hifadhi ya jamii, mwongozo wa uwekezaji, usalama wa fedha za wanachama, ukwasi wa mifuko ya hifadhi za jamii na mwongozo kwa bodi za wadhamini wa mifuko.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sara Kibonde, alisema bado jamii inahitaji kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa ina manufaa kwa jamii yote wakiwemo wale wasiokuwepo kwenye sekta rasmi ya ajira.

Alisema kwa mujibu wa takwimu za mamlaka hiyo, jumla ya wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi ni mmilioni 2.1 kati ya wafanyakazi milioni 25 waliopo.

“Kwa maana hiyo wafanyakazi takribani milioni 23 ambao ni sawa na asilimia 91.2 hawajiunga na mifuko hii.”

Aidha alisema wakati mifuko ya pensheni ina wanachama milioni 2.1, kati yao, mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii wapo wanachama milioni 1.1 wakati mfuko wa bima ya afya wapo wanachama 920,701.

Alisema mpaka sasa mifuko hiyo ina wastaafu 105,057, michango ya wanachama hao inayofikia Sh trilioni 1.69 na bima ya afya Sh bilioni 88.5, ambayo jumla yake ni Sh trilioni 1.78.

Chanzo: Habari Leo
 
hili fao la kujitoa ndio kwishney.....

kama hukuwahi kulifaidi miaka iliyopita ndio subiri uzeeeke tu...

awamu ya kuisoma namba hiiiiiii
 
Kumbe songombingo bado zinaendelea? nasubiria kupata 'singeli' ya nguvu sasa kutoka kwa hawa SSR.
 
SSRA , hawa wasipokuwa makini hii mifuko ya jamii itawapelekesha mpaka kila siku waje na matamko, kwa nini wasitunge sheria moja mifuk yote ifuate? wao wanakuwa kama wanabembeleza vile, mifuko fulani inafuta fao kabla wao hawajatoa sheria sijui hapa nani anamsimamia mweingine., hovyo sana.
 
Duuh hawa jamaa vip hela zetu wanachezea danadana Mungu anawaona[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Labda kwa sababu ya ubabe wao watafanikiwa lakini huu mwiba ni mchungu sana.Ni kama wamefanikiwa kwa PPF,na hiyo ni kwa sababu asilimia kubwa ya wanachama wa mfuko huu ni watumishi wa umma ambao kimsingi sio wahitaji sana wa fao la kujitoa,wale wachache wa sekta binafsi waliokutwa huko ndio imekula kwao. Lakini unapouongelea mfuko kama NSSF ambao asilimia kubwa ya wanchama wake ni sekta binafsi, hapo ndipo moto unapowakia.
 
Waache wajadili wee lakin cha mtu mav....i
 
1. Fao litawahusu wale walioachishwa kazi au kufukuzwa kazi na waajiri wao.
- Ni kwa wale waliyochangia kuanzia miezi 18 au zaidi. (Kama umechangia chini ya miezi 18
utapewa hela yako yote uliyochangia mfuko wa hifadhi ya jamii).
- Watalipwa 33% ya mshahara wao wa mwisho kwa muda wa miezi sita
- Baada ya miezi 6 kama bado atakuwa hajapata ajira mpya basi mfuko wa hifadhi ya jamii
utamlipa nusu ya fedha yake aliyochangia.
2. Kama mwajiriwa ambaye ni mwanachama wa mfuko wa jamii akiacha kazi kwa hiari yake
mwenyewe basi hili fao halitamhusu (hatapata chochote kati ya hivyo vilivyotajwa hapo juu).

MASWALI YANGU KWENU WADAU:

1. Hivi nini lilikuwa lengo kuanzishwa kwa fao la kjitoa la hapo awali na sababu hivyo hazipo sasa?
2. Je kwa mshahara wa kima cha chini cha wafanyakazi 33% itamfanya mtu aliyeacha kazi kumudu
gharama za maisha ya sasa assuming kwamba hana njia nyingine ya kipato kwa wakatio huo.
3. Je kwa yule ambaye ameamua kuacha kazi kwa sababu muhimu kabisa kama mahusiano
mabaya na mwajiri au ameona nivyema akajiajiri yeye mwenyewe binafsi, kutompa hela yake
aliyochangia kwa muda wote huo ni halali?
4. Kwa sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii mstaafu anatakiwa kulipwa pension ikiwa amechangia
miezi 180 (miaka 15) au zaidi. Hivyo nikiachishwa kazi au kufukuzwa kazi nikiwa nimechangia
miezi pungufu ya 180 maanake ni kwamba sitapata pension. Sasa je hela yangu niliyochangia
mfuko wa hifadhi ya jamii itanisaidiaje ikibaki huko (maana sitapewa yote - angalia swai no. 2)?

🙁Kwa kweli kwa hayo machache tu nawasilisha ili wadau mtujuze zaidi maana naona huu ni mwanzo wa mifuko ya jamii kuwa mifuko nyonyaji na kuwaletea umasikini waajiriwa na wanachama wa mifuko hiyo!

Nawasilisha!
 
Kama watu walio katika serikali wananyanyasika kupata mafao yao baada ya ajira zao kukoma je walionje ya serikali watayapata kwa wakati watakapoyahitaji?
 
Wabunge ni wachache saana. Kwahiyo wasishugulikie wao peke yao, zaidi hii mifuko waende moja kwa moja kuwa uliza wateja wao ambao ndio washiriki wa mifuko hiyo.
 
Cjawahi ona hela ya mtu inapangiwa mda wa kuitumia
 
Wameshindwa kukusanya michango ya waajiriwa 23m bila aibu wanataka kuwanyonya hao wachangiaji wachache.

Sekta zote binafsi Tanzania zitaumia sana wakiwemo hao wanaoandika taarifa magazetini sema hawajitambui.

Hili jambo nawashauri SSRA waliache watu wapewe chao
 
Wanakomaliaaa sana...pesa za watu! Nashangaa sana wanavyohangaika na pesa za wafanyakazi! Kosa ni kutuwekea hizo pesa? Utaratibu ubadilishwe tuwe na access ama bank na mafao yetu! Watacaha kuchezea pesa zetu kwenye miradi ya siasa! Serikali isingekuwa inakopa zile pesa kisiasa...wasingehangaika na matamko ya kipuuzi kama haya
 
Wana Jf nimemsikia waziri mkuu jana akitangaza ya kuwa serikali imefanikiwa kulipa deni la mifuko ya jamii hadi asilimia 80.

Kama ndo hivyo kwa vile financial position yake sasa ni sound, kwann wasiwarudishie wanachama fao lao la kujito ili liwanufaishe kama ilivyokua mwanzo?
 
Unajua maana ya SIASA? = Si Hasa. Kalagabaho!
 
Hawa jamaa hawatarejesha fao la kujitoa mpaka wafanyakazi waje juu.
 
Ni miezi kama sita sasa tangu mfuko wa ppf kutangaza kusitisha utoaji wa fao la kujitoa, madai ya ppf ni kwamba hakuna sheria inayotoa fao la kujitoa japo tunajua mswada uliwasilishwa 2012 na haukupita bungeni, kutokana na upinzani mkubwa uliokutana nao. maelekezo yalitolewa kufanya malekebisho ili mfuko uwe na mafao rafiki kwa wanachama.

badala yake kabla ya hata kufanya marekebisho ya kisheria mifuko karibia yote imesitisha wanachama kujitoa. fao hilo ni mhim mno kwa wafanyakazi wa mikataba ambayo pale inapomalizika mwanachama anaweza kupata au asipate mkataba mwingine kutokana na hali ya mishagara ya nchi yetu mtu anapisitishiwa au kumaliza mkataba anakua hana akiba yoyote, hivyo fao lake linakuja kua mkombozi kwa wakati huo.

Mifuko hii iko kwa ajiri ya wanachama , pamoja na kelele zote za wafanyakazi mifuko bado imekazania uamuzi wake kwamba no kujitoa. swali langu kuna nini au kuna siri gani nyuma ya uamuzi huu?

Afanyakazi wafanye nini ili kupata haki yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…