1. Kula chakula hai/chenye kiini cha uhai
Chagua chakula ambacho kiini Cha uhai wake haujaharibiwa kama ni tunda basi mbegu yake iwe na uwezo wa kuota na kuendeleza kizazi.
Pia chakula fresh ni bora zaidi kuliko chakula kilichoandaliwa na kuhifadhiwa Kwa muda mrefu.
2. Kula chakula kizima
Hii husaidia mwili kula kiasi Cha nishati kinachohitajika tuu na mwili ukaridhika na Hilo. Mfano ni rahisi kutumia nusu kikombe Cha mbegu za alizeti kuungia mboga na ikawa tamu lakini nusu kikombe ya mbegu za alizeti ukikamua mafuta utapata kiasi kidogo sana ambacho yasingetosha kupikia mboga hiyo hiyo hivyo kufanya utumie zaidi ya kiasi kinachohitajika.
Mara nyingi maandalizi ya uhifadhi wa vyakula yanalenga kukifanya kuvutia machoni mwa mtumiaji na kukifanya kikae muda mrefu zaidi hivyo sehemu ya chakula inayoharibika kwa urahisi ama ambayo inapunguza mvuto wa kibiashara huondolewa, mfano kwenye maandalizi ya sembe kiini na magamba ya mahindi ambayo ndio bora zaidi hupotea hivyo kufanya chakula kipungue virutubisho muhimu.
Michele wa brown ni bora zaidi kuliko mchele mweupe vivyo hivyo kwenye ngano na bidhaa nyengine.
3.Kula zaidi chakula chenye unyevunyevu.
Maji ni muhimu katika kufanikisha na kurahisisha karibu process zote za mwili; digestion na secretion zikiwemo. Hivyo ulaji wa vyakula vikavu husababisha mwili upoteze maji ambayo yataelekezwa kwenda kurahisisha mmeng'enyo wa vyakula hivyo na tabia hii ikiwa ni ya kudumu inaweza kukuletea madhara mengine kama vile jasho kunuka isivyo kawaida, constipation na hemorrhoids.
Vyakula vyenye unyevu nyevu humeng'enywa kirahisi ndani ya mwili hivyo kuupunguzia stress mfumo wako wa chakula na matokeo yake huweza kuonekana hata katika ngozi ya mtu.
4. Lainisha viungo vyako vya ndani Kwa kutumia mafuta mazuri.
Mwili unahitaji mafuta Ili kutengeneza nishati na pia kama kilainishi kuzikinga ogani muhimu za mwili hivyo unahitaji kilainishi chenye ubora mzuri ili utendaji wake uwe ni wenye athari bora zaidi zisizo na madhara.
Mfano wa vyakula vyenye vilainishi hivi ni mafuta ya nazi, mafuta ya zaituni, parachichi, samaki wenye mafuta na mbegu kama karanga.