Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
FANYA TAMBIKO LITIMU.
Mstahiki Zack​:
Siandiki kuwatisha,ila navuta Amani.
siwatilii presha,ila yabidi wendani.
leo mja kanichosha,aiba mwangu nyumbani.
Leo Tambiko Latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Uloandika yatisha, yamevuruga amani,
Ila hayaleti presha, na maumivu kichwani,
Huyo mja wa kuchosha, ndiye weye ubaini,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako
Mstahiki Zack:
Kwa siku na madakika,meonekana wazimu.
ila siku imefika,leo tunamwaga damu.
kwa mwembe nitafika,babu ashike hatamu.
leo tambiko litimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Sekunde mbio dakika, sasa mwaka umetimu,
Mambo ya kusadikika, yamekutia wazimu,
Kwa babu sitatishika, bure zake talasimu,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
Mstahiki Zack:
Kwa Kioo takuona,nikutilie mizungu.
utakoma na kunona,usahau na kizungu.
familia talizana,wapagawe kwa machungu.
leo tambiko latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Kwa kioo taziona, fikira zako mwenzangu,
Heri, shari, za Rabana, bure ufanye mizungu,
Hivi hivi taniona, tena sifanyi machungu,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
Mstahiki Zack:
Zack sitarudi nyuma,Naapa kwa Subuhana.
sitakumbuka Huruma,leo wazi nimekana.
nitamtesa kinyama,hapo utu taukana.
leo tambiko latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Zack nenda fanya hima, uape kwa kutabana,
Hutokumbuka huruma, ikiwa wajua huna,
Sawa uwaze unyama, sababu utu hauna,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
Mstahiki Zack:
Msidhani sitaweza,kuua haiwi kazi.
kwa waganga hutoweza,kujitibu mwana kinzi.
lazima nitakuliza,kwa simanzi na machozi.
leo tambiko latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Kuwa sababu waweza, kuua si yako kazi,
Allahu ndio MUWEZA, nategemea Azizi,
Hakuna la kuniliza, kwa ndumba hata hirizi,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
Mstahiki Zack:
Hata uende polisi,sitopatikana juwa.
jipunguzie mikosi,akuauni moliwa.
kufa kwako nakufosi,tanzania si maluwa.
leo tambiko latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Nani aende polisi, punguza kujizuzuwa,
Vipi nipate mikosi, ikiwa nimestiriwa,
Kifo kwa kila nafsi, si jambo la kukimbiwa,
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
Mstahiki Zack:
Sijatisha jamanini,ma'na sina mahasidi.
ukijishuku mwendani,kukufa huna budi.
mwisho wangu samahani,amani itashitadi.
leo tambiko latimu,mahasidi jipangeni.
Njano5:
Mstahiki una nini, si moto wala baridi,
Na ulikula yamini, iweje nyuma urudi?
Nauona walakini, upewe dawa yabidi.
Fanya tambiko litimu, hasidi vitendo vyako.
uTuNzI wA sAuTi yA BaBu Kenya
NA
Dotto Rangimoto Chamchua​ (Njano5)
255784845394/255762845394
mzalendo.njano5@gmail.com
Morogoro Tanzania