Mimi ni daktari bingwa wa magonjwa ya ndani na pia ni mkufunzi wa kitaifa wa magonjwa ya mlipuko ikiwapo COVID. Na nimekuwa nikitibu wagonjwa wengi wa COVID toka huu ugonjwa uje nchini kwetu na ningependa kuwapa ushauri ufuatao.
Naamini unafahamu dalili za ugonjwa huu kwakuwa zimetangazwa sana, labda nikuongezee zingine chache kama kuharisha, kichwa kuuma, mwili kuchoka, viungo kuuma kupoteza ladha na kupoteza uwezo wa kuhisi harufu.
Sasa ukiwa unajihisi umepata maambukizi fanya yafuatayo. Hii inawahusu wale ambao dalili zao sio kali sana, yaani mild illness au hata hawana dalili kabisa. Watu wenye dalili kali waende hospitali tafadhali!
Basi fanya yafuatayo:
Naamini unafahamu dalili za ugonjwa huu kwakuwa zimetangazwa sana, labda nikuongezee zingine chache kama kuharisha, kichwa kuuma, mwili kuchoka, viungo kuuma kupoteza ladha na kupoteza uwezo wa kuhisi harufu.
Sasa ukiwa unajihisi umepata maambukizi fanya yafuatayo. Hii inawahusu wale ambao dalili zao sio kali sana, yaani mild illness au hata hawana dalili kabisa. Watu wenye dalili kali waende hospitali tafadhali!
Basi fanya yafuatayo:
- Fanya mazoezi ya viungo: mazoezi yatakusaidia kuboresha mfumo wako wa kinga, kuimarisha afya yako na kuboresha uwezo wa mapafu na upumuaji wako kwa ujumla. Fanya kwa dk 30 - 40/siku
- Kula vyakula vyenye mchanganyiko ulio kamili. Yaani protini, mafuta, wanga, vitamins, n.k. Unahitaji rutuba zote ili kutengeneza seli mpya za kinga ya mwili. Kunywa maji lita 3-4 kama hauna tatizo lingine la kiafya ambalo linakuzuia usinywe maji mengi.
- Tumia multivitamins: kwakuwa wengi wetu hatuna muda au nafasi ya kupata virutubisho vyote kama mwili unavyohitaji basi unaweza kutumia vidonge vya multivitamins. Weka msisitizo katika vitamins zifuatazo: C, D, B, A na madini kama ya Zinc. Virutubisho hivyo vitakusaidia kuujengea mwili uwezo wa kujikinga/kupona.
- Kula antibiotics kama kinga: haswa kama una dalili za awali za kifua. Tumia Amoxiclav 625mg BD 5/7 (Altenatively: Tumia Azithromycin)
- Tumia Paracetamol (1g TDS 5/7). Hii pia tumia kama una dalili za awali za kifua, homa, ambazo sio kali.
- Tumia dawa za kikohozi m.f. Cetirizine, Antihistamines, Cough syrups.
- Epuka baridi katika mapafu, mf. AC au feni ambayo inakupiga moja kwa moja kifuani.
- Epuka kujifungia sana ndani, yaani hakikisha mwili unapata hewa safi inayozunguka. Good ventilation. Kwahiyo toka nje mara kwa mara upumue hewa safi na kupigwa na jua.
- Pima na utibu magonjwa haya: Malaria, UTI, Sukari, Figo, Presha, n.k. Magonjwa kama haya huwa na tabia ya kuzidi au kukuletea shida zaidi iwapo pia una maambukizi ya virusi vya korona. Kwahiyo hakikisha unapimwa na kutumia dawa sahihi mapema.
- Dalili zikizidi kuwa mbaya tafadhali fika hospitali kwani kuna dawa ambazo inabidi tukupatie na vipimo vya ziada vya kufanya.