Fanya haya kwa mume wako

Fanya haya kwa mume wako

Alvin A.

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2016
Posts
2,865
Reaction score
3,639
1. Muite kwa jina lake la utani
2. Muache atumie mamlaka yake kama
kichwa cha nyumba.
3. Usimcheke akiwa ameumizwa na
jambo fulani.
4. Kaa kimya pale anapokuwa na hasira.
Unaweza ukaenda kumuomba msamaha
na kumueleza kwanini ulimkosea pale
hasira zinapokua zimemuisha.
5. Kuwa na haraka ya kuomba msamaha
pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale
anapokusamehe.
6. Ongelea mazuri yake na yeye kabla
ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya
hivyo.
7. Waheshimu wazazi wake.
8. Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia
wazazi wake na kuwapelekea chochote.
Na afanye hvyo na kwa wazazi wako pia.
9. Msuprise kwa chakula akipendacho,
hasa kipindi kile anapokuwa na msongo
wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.
10. Usiruhusu dada wa kazi amhudumie
chakula mume wako ukiwa nyumbani.
11. Mkaribishe kwa kumkumbatia
anapotoka kwenye mihangaiko yake.
Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.
12. Tabasamu pale unapomtizama, vaa
vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka
wote kwenda kwenye warsha mbalimbali.
13. Mpigie simu na umwambie kwamba
unampenda na umemkumbuka 14. Muamshe asubuhi na umpe romance
kiasi kwamba ifike hatua ya kuhitaji, mpe
na hata jishughulisha na wanawake
wengine siku hiyo.
15. Kamwe usithubutu kutamka kuwa
hakuridhishi na tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
16. Mwambie ni kiasi gani una bahati
kuwa nae kama mume wako.
17. Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.
18. Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu
wako katika maisha yako.
19. Kumbuka kumuombea na kumkabidhi
mikononi mwa Mungu.
20. Tengenezeni utaratibu wa familia
nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja
kila asubuhi na usiku kabla ya kulala.
Mungu abariki ndoa yako.
Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya
kweli leo na daima.
Na wasio serious na mahusiano
wanaokupotezea muda wako wajikatae
kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya
kutimiza kusudi la Mungu kwako.

FB_IMG_1570411851026.jpeg
 
Ujumbe mzuri sana, safi sana, sasa Kama mwanamke atanifanyia hayo yote, nitaanzaje kumuacha?. Nashukuru Mungu mke niliye naye anajitahidi japo si kwa hayo yote uliyoyataja, offcourse Sio mbaya kwasababu na yeye ni Binadamu hawezi kuwa mkamilifu kwa asilimia Mia moja, maana hata mimi mwenyewe sio mkamilifu.
 
Ujumbe mzuri sana, safi sana, sasa Kama mwanamke atanifanyia hayo yote, nitaanzaje kumuacha?. Nashukuru Mungu mke niliye naye anajitahidi japo si kwa hayo yote uliyoyataja, offcourse Sio mbaya kwasababu na yeye ni Binadamu hawezi kuwa mkamilifu kwa asilimia Mia moja, maana hata mimi mwenyewe sio mkamilifu.
Safi mkuu
 
Wapi nimeandika hivyo, mimi nina mwanamke mfupi, shameless mwenye sura ya baba yake ndo ananifanyia hayo yote mtoa mada aliyoandika na usitegemee kufanyiwa hivyo vitu na hawa masista du utasubiri sana.
ukimwambia mkewako hicho ulichokiandika atafurahi kweli anakufanyia haafu unamwambia anafanana ma baba yake>?
 
Back
Top Bottom