Familia zote zingatieni ushauri huu

Familia zote zingatieni ushauri huu

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,988
Wengi Wetu Tumekaa mkao Wa Kusubiri Jumapili Kupeleka Watoto Mbele ya Madhabahu kwa Ajili ya *KURUDI SHULE*.
Na Jambo Hili la kwenda Madhabahuni, Wengine Wamelichukulia Kawaida Saana *KIASI CHA KUMZOEA MUNGU KWA KIWANGO CHA JUU, JAMBO AMBALO NI HATARI SANA*.

Nakuomba fanya yafuatayo

1. Fanya Ibada na Watoto Wako.
2. Waite na Uhakikishe wote Wametulia na Kusikiliza Mafundisho toka Kwako Mwenyewe au Mtumishi.
3. Wape, Mafundisho ya Namna wanavyorudi Shule Msimu huu mpya ambao sio Mwepesi kwa Wengi, Waonye kitabia maana wamekaa nyumbani Kwa Muda Mrefu,
4. Waombee Toba na Rehema Mbele za Mungu Yamkini Walitenda Dhambi Nyingi mno au kuharibiwa Akili na Mambo ya Mtandao na Video Mbalimbali ambazo kwa Kiwango kikubwa Vimeharibu Fahamu zao.
5. Watolee sadaka kwa Hofu, Unyenyekevu Mbele za Mungu huku ukimwambia Mungu awatengenezee Msimu Mpya kwa Agano la Damu ya Yesu Kristo.
6. Ombea Yale Majengo na Vyumba Vyote Shuleni yamkini Kwa Kipindi Hiki yako Mengi ambayo Yalitendeka Kwa Siri hasa Shule Binafsi ambazo baadhi yao hawana Hofu ya Mungu na Wanafanya biashara kwa Nguvu za Giza na Makafara ili Wapate Watoto na Pesa nyingi
7. Kataa kwa Dhati Magonjwa ya kuambukizwa yasiwapate watoto wako. Waombee ulinzi
8. Mshukuru Mungu kwa Ajili yao na Familia nzima.
9. Ombea Ndoto zao kwamba Wawe watu kati ya watu kupitia Elimu yao
10. Kaa na Familia Mle Pamoja, Mfurahi Pamoja na Kutakiana Amani Kwa Jina La Yesu

ISAYA 54:12-17

Nakutakia Maandalizi Mema.
 
Wengi Wetu Tumekaa mkao Wa Kusubiri Jumapili Kupeleka Watoto Mbele ya Madhabahu kwa Ajili ya *KURUDI SHULE*.
Na Jambo Hili la kwenda Madhabahuni, Wengine Wamelichukulia Kawaida Saana *KIASI CHA KUMZOEA MUNGU KWA KIWANGO CHA JUU, JAMBO AMBALO NI HATARI SANA*.


Nakutakia Maandalizi Mema.
Maelezo yameisha hayo
 
Back
Top Bottom