ivunya
JF-Expert Member
- Sep 18, 2015
- 2,290
- 2,231
Donald Trump alisindikizwa na familia yake alipopanda jukwaani kutoa hotuba baada ya kushinda urais Marekani. Unawafahamu wake zake na watoto?
1. Barron Trump ndiye mwana wa pekee wa Donald na mke wake wa sasa Melania. Ingawa alijitokeza katika mikutano kadha ya kampeni, mvulana huyu wa miaka 10 hajakuwa akioneshwa sana hadharani. Hucheza gofu na babake na anaaminika kuzungumza Kislovenia kwa ufasaha. Mamake alitoka Slovenia.
2. Melania Trump, ni mwanamitindo wa zamani, mzaliwa wa Slovenia, ambaye aliolewa na Donald Trump Januari 2005. Alijitokeza na kumtetea mumewe baada ya kanda ya video kutokewa wakati wa kampeni na kumuonesha akijitapa kuhusu kuwadhalilisha kimapenzi wanawake. Julai 2016, aligonga vichwa vya habari baada ya kutoa hotuba mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, baada ya Bw Trump kuidhinishwa kuwania urais, ambapo alituhumiwa kuchukua maneno mengi kutoka kwa hotuba iliyotolewa na Bi Michelle Obama mwaka 2008.
3. Jared Kushner ni mume waIvanka, binti mkubwa wa Donald. Bw Kushner ni mwana wa mfanyabiashara tajiri wa New York anayefanya biashara ya nyumba ya ardhi. Amekuwa pia mmiliki wa gazeti la kila wiki la Observer jijini New York kwa miaka 10. Kushner, ambaye ni Myahudi, anadaiwa kuwakera watu wa familia yake alipoandika makala kutetea hatua ya Donald Trump kutumia Star of David (Nyota ya Daudi ambayo ni nembo ya Wayahudi) kwenye ujumbe kwenye Twitter akimshambulia Hillary Clinton. Akiandika kwenye gazeti hilo lake, alisema: "Shemeji yangu hana chuki dhidi ya Wayahudi". Aliendelea: "Tofauti kati yangu na wanahabari na watu wa Twitter wanaodhani huu ni wakati mwafaka sana wa kumshambulia shemeji yangu ni rahisi. Mimi namfahamu (ni mtu wa aina gani), wao hawamfahamu.
4. Ivanka Trump labda ndiye mwana wa Donald Trump anayefahamika zaidi na watu. Ndiye binti wa pekee wa mke wa kwanza wa Trump, Ivana. Alikuwa mwanamitindo mzamani lakini sasa ni makamu wa rais wa shirika la The Trump Organization na pia jaji katika kipindi cha runinga cha babake cha The Apprentice. Alibadili dini na kujiunga na didi ya Kiyahudi baada ya kuolewa na Jared mwaka 2009. Kwenye hotuba mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Republican, aliunga mkono babake na kusema anatetea haki za wanawake. "Kama mama, wa watoto watatu, najua jinsi ilivyo vigumu kulea familia. Na najua hilo kwa sababu nimebahatika kuliko watu wengi. Familia nyingi Marekani zinahitaji usaidizi. Sera ambazo zinawaruusu wanawake wenye watoto kufanikiwa hazifai kuwa jambo nadra sana, zinafaa kuwa kawaida."
5. Tiffany Trump ni binti wa Donald Trump kutoka kwa mke wake wa pili Marla Maples, mwigizaji wa zamani na nyota wa TV. Hutumia sana Twitter na Instagram, na ujumbe wake mitandao ya kijamii huashiria maisha ya kifahari. Amekuwa sana hajitokezi kwenye kampeni lakini alisifiwa na babake kwa kutoa hotuba nzuri sana wakati wa kongamano kuu la chama cha Republican, ambapo alisema babake ni mtu mwenye sifa za kuwasaidia na kuwahimiza wengine.
6. Vanessa Trump, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Haydon, aliolewa na Donald Trump Jr mnamo Novemba 2005. Wawili hao wamejaliwa watoto watano, akiwemo Kai, mwenye umri wa miaka minane (pichani). Vanessa alianza uanamitindo akiwa mtoto na wakati mmoja alikuwa mpenzi wa Leonardo DiCaprio. Yeye huhudumu katika kamati tendaji ya wakfu wa mlamu wake Eric. Huwa na bunduki nyumbani - na kwa mujibu wa mahojiano yake na SilencerCo, kampuni inayounga vifaa vya kunyamazisha mlio wa bunduki, pia ana leseni ya kubeba silaha na hufanya mazoezi ya ulengaji shabaha mara kwa mara.
7. Kai Trump ndiye kifungua mimba waVanessa na Donald Jr, ambao wamejaliwa watoto watano.
8. Donald Trump Jr ndiye mwana wa kwanza wa kiume wangu Donald Trump na mke wake wa kwanza Ivana. Kwa sasa ni makamu wa rais mtendaji wa shirika la The Trump
Source: bbc swahili