Falsafa ya Dkt. John Pombe Magufuli

zebedayo musibha

Senior Member
Oct 26, 2019
111
86
Tangia mwaka 1776, Taifa la Marekani limepitia vipindi tofauti tofauti ambavyo ndani yake vilitofautishwa na falsafa mbali mbali za uongozi katika kutekeleza sera ya nchi chini ya maraisi wao.

Lakini falsafa za maraisi mbali mbali katika taifa hili la marekani kuna zilizo kumbana na ukinzani dhidi ya azimio la mfumo fulani(x) ambao ulikuwa unatekelezwa na MaJesuit dhidi ya Mataifa ya Amerika ikiwemo Marekani.

Amri ya Wajesuiti ilitimiza kiapo chao tena kwamba watatia sumu, wataua, au watafanya chochote kinachohitajika ili kuwaondoa wale wanaopinga mipango yao.

Kuanzia 1841 hadi 1857, Marais watatu wa Marekani walishambuliwa na Wajesuiti kama ilivyoainishwa katika Bunge la Vienna, Verona, na Chieri. Wawili walifariki na mmoja kutoroka (RAIS HARRISON, TAYLOR, NA BUCHANANI) akiwemo pia Rais Lincoln.

Hu ulikuwa ni mpango wa Majesuit kuakikisha kuwa Hawaruhusu chochote kusimama katika njia yao ya utawala kamili wa Amerika, na uharibifu wa Katiba. Pia waliazimia kuimiliki United kwa usiri mkubwa kwa kutumia mawakala wao walio jofanya masikini na waaminifu wa kutoka kila kona ya ulimwengu, na kuwakusanya katika mioyo ya miji ya Washington, New York, Boston, Chicago, Buffalo, Albany, Troy, Cincinnati. Chini ya vivuli vya miji hiyo mikuu, Wamarekani.

Waliwatazama mawakala kama watu maskini na kwa dharau kubwa, kama wanaofaa tu kuchimba mifereji yao, kufagia mitaa yao na kufanya kazi katika jikoni zao. Hi ilikuwa ni moja ya mbinu zilizo tumiwa na hao Majesuit mda si mlefu Majesuit walipenya hadi kwenye idara nyeti za nchi hapo ndio ikawa mwanzo wa kuimiliki United.

Lakini falsafa za kizalendo za hao Marais (Lincoln, HARRISON, TAYLOR NA BUCHANANI) ziliendana ambazo zilijikita zaidi kuijenga United isiyo mpigia magoti mtu yeyote au taifa lolote ulimwenguni na kuifanya kuwa taifa huru lisiro na mfungamano wa Dini yoyote.
Ni falisafa ambazo zilikinzana na matakwa ya Majesuit na kwakuwa walipenya ndani ya serikali na idara nyeti ndio sababu walitekereza adhima yao ya kumfuta yeyote aliye ingilia njia zao na ndio maana hawa Marais waliuwawa.

Kwa mfanano huo wa Taifa la Marekani leo hii tunalitazama Taifa la TANZANIA chini ya Rais JOHN POMBE MAGUFULI
Falsafa yake ya uongozi imejikita zaidi katika uzalendo wa utaifa kwanza kulijenga taifa katika nyanja ya kiuchumi na kuziba mianya ya unyonyaji katika wizi wa rasilimali za taifa.

Kama ilivyo kuwa kwa taifa la Marekani leo hii africa tunafanywa hivyo hivyo ambapo tunashindwa kuwa na maamzi ya aina ipi ya demokrasia tunapaswa tuwenayo, tunashindwa kuwa na maamzi kwenye uchumi, Elimu na Siasa kwani hivyo vyote tumeingiliwa na mataifa ya nje(mabeberu)

Lakini falsafa ya Dkt. MAGUFULI ni kupambana na Diplomasia ya uchumi katika kulijenga Taifa ambapo katika nyanja hii ya uchumi ndipo kuna mizizi ya wanyonyaji ambao mpango wao ni kuliangamiza Taifa kuendelea kuwa masikini hivyo ni vita ambayo ni kari sana ambapo kama watanzania inatupasa kusimama pamoja na Rais wetu pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa na kidini tuwe mstari wa mbele katika kumwombea Rais wetu na Taifa letu kwa ujumla (Yanayo endelea huko duniani ni makubwa sana kwa kuwa yanaendelea kwa siri kubwa ila matokeo yake ni kunyongwa kwa uchumi na kutaabika katika umasikini sana sana zawadi ambayo tunaweza pewa ni vita kuuwana sisi kwa sisi)

Watanzania tubadilike tuwaelewe viongozi wetu leo hii mifumo mingi ya nchi inashikiliwa na watu wachache ambao adhima yao ni kuitawala Dunia tuna tengenezewa majanga mbali mbali vita, magonjwa na njaa lengo lao ni nchi ziyumbe kiuchumi na tutumbukie kwenye mikopo ambayo tutaendelea kuwa wategemezi na hatuta weza kujikwamua KIUCHUMI mfano mwaka jana na mwaka huu wametengeneza janga la CORONA lakini wazuia nchi zingine kutengeneza chanjo lakini chaajabu wametengeneza wao chanjo na leo inapigwa promo ili mataifa yanunue au wapewe kama msaada kwa njia ya mkopo kupitia WB na IMF.

Sasa pale tunapo pata Rais ambaye kila njia za hawa watu anapambana kuzikwepa huyo ndie SHUJAA na MZALENDO wa kweli wa Taifa letu. Huyu ndie Raisi aliye weza kuonyesha falsafa ya uongozi wa kizalendo na ujasiri mkubwa katika kulijenga Taifa.

JE DEEP STATE IMEHUSIKA KATIKA KIFO CHA HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI?

Makala yangu hapo juu ilimlika kuhusu Falisafa ya aliye kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI.

Jinsi gani Falisafa yake ya uongozi ilivyo kuwa mwiba kwa MABEBERU pamoja na baadhi ya vigogo ndani ya nchi.

Je, DEEP STATE imehusika?
Nianze kutolea mfano utawala wa D. TRUMP aliye kuwa Raisi wa Marekani, ukisoma katika vitabu vya
- IN DEEP by David Rhode
(THE FBI, THE CIA AND THE TRUST ABOUT AMERICA'S DEEP STATE)
- DONALD TRUMP Vs. THE UNITED STATES INSIDE THE STRUGGLE TO STOP A PRESIDENT. BY Michael s Schmidt
-RAGE BOB WOODWARD
-DISLOYAL by Michael Cohen

Utagundua kuwa ilikuwa lazima Rais DONALD TRUMP asiendelee na pia utagundua kuwa mbali na mamlaka ya Rais kwa nchi ya Marekani ipo mamlaka ya siri (DEEP STATE) ambayo ndio ina control Marekani moja ya sababu kadhaa ambavyo vilisababishwa Rais TRUMP ang'olewe ni:
  • Biashara yake ya siri na urusi (Moscow)
  • Ubaguzi na mengineyo mengi ambayo yameorodheshwa kwenye hivyo vitabu hapo juu.
Nini na maanisha kwa mfano huu
Ipo nguvu ya ziada ambayo ni ya siri inayo control baadhi ya nchi Duniani kutokana na mazingira yake na huitaji wake kwa agenda za nchi na watu wake.

Endapo hii nguvu ikiamua kumuondosha Rais madarakani wasipo tumia njia ya uchaguzi basi kuna hatari ya kuuwawa kama ilivyo kuwa kwa baadhi ya maraisi wa Marekani walivyo uwawa kama nilivyo elezea kwenye makala iliyo tangulia.

Nguvu hii hata africa ipo na kipindi nchi nyingi za africa zinapata uhuru zilikabidhiwa kwa makubaliano maalum hivyo upandikizwaji wa hii nguvu yaan DEEP STATE iliendelea kustawi kwa kuhusiha baadhi ya viongozi wa maeneo (nchi) husika kutokana na huitaji wa nchi yenyewe.

Mfano tumeshuhudia uchaguzi wa DRC ulio pita pale kuna nguvu ya ziada ili husika kumuweka Raisi wasasa kuwa madarakani.

Je kwa Tanzania DEEP STATE inahusika? Pengine kifo cha HAYATI DKT JOHN POMBE MAGUFULI

Tukitazama baadhi ya matukio kuna namna ya mfumo wa siri.

1. Tukianzia kwenye uchaguzi 2020
kabla ya uchaguzi kulikuwa na vuguvugu fulani kama vile Rais MAGUFULI lazima ang'oke madarakani na hi vuguvugu ilianzia ndani ya chama chake na baadae nje ya chama.
Swali la kujiuliza je lile kundi ambalo liliitaji kusimamisha mgombea ndani ya chama wachuane na Raisi aliyepo madarakani hiyo nguvu hilo kundi na huyo mtu waliitoa wapi? Na hadi kufikia kuaminisha na watanzania

Lakini baadae huo mpango ulivyo shindikana baada ya Rais MAGUFULI kufanya maamzi magumu kama mwenyekiti wa chama kwa kuwafuta na kuwafungia uwanachama baadhi ya makada.

Tunaona kwenye uchaguzi kuna kete nyingine inachezwa baada ya kada na mwanadiplomasia nguli BERNARD MEMBE kujiunga ACT WAZALENDO hii ilikuwa ni hesabu ya kuwa lolote lingetokea kwenye uchaguzi kutokana na vuguvugu la uchaguzi lilivyo kuwa na pengine hesabu za matokeo ingekuwa kama ilivyo kuwa DRC walipo kabizi madaraka kwa mtu wa tatu badala yule wa upinzani mkuu
Sasa kwa endapo lolote lingetokea kwa ccm kulemewa njia ya CHADEMA ilikuwa wazi lakini wasinge kabidhiwa badala yake wange kabidhi kwa MEMBE (ACT).

Shida hesabu za MEMBE zilialibiwa na chama chenyewe kwa kuungana na CHADEMA na ndio maana CCM alifurahi sana pale walipo ungana.

Ingawaje haikutokea lakini mtambue kuwa ACT ni planned hiki kimekuja kushusha tempa ya upinzani bara na visiwani (Note kifo cha self kuna miujiza ya penetration za ACT ili ku stabalize visiwani)
Hivyo ACT ni sumu na mwiba ambao sasa watu wengi hamta elewa lakini ipo siku mtaelewa.

2. Kufeli kwa plan ya uchaguzi ndipo tunashuhudia kifo kina mkuta MAGUFULI
Kifo ambacho kimeacha maswali mengi sana kwa watanzania.
Lakini kabla ya kifo tulishuhudia taasisi ya kidini tena kubwa ulimwenguni wao wakitoa walaka kwa waumini wao maana yake walikuwa kinyume na maamzi ya serikali kuhusu CORONA.

Pia awali ya yote Rais MAGUFULI alikuwa akikaliliwa akisema tumuuombee mtangulize MUNGU na kama amejitoa kafara kwa watanzania kana kwamba kuna mfumo ambao wazi alikuwa akipambana nao au kwenda nao kinyume na ndio maana bali na katiba alikasimisha madaraka yote ya nchi mikononi mwake hadi kutowaamini baadhi ya watendaji wake wa karibu.

Lakini kinyume cha watangulizi wake alichukua mda mwingi kuendèsha shughuli za kiserikali Chato kuliko Magogoni au chamwino hi hali kama ilileta wasiwasi pengine kulikuwa na siri nyuma ya haya matukio yote.

Mwisho. Pengine Falisafa ya Raisi MAGUFULI kama nilivyo elezea kwenye makala ya mwanzo huwenda ikawa sababu ya kifo chake na kama ni hivyo huwenda tukawa na nguvu ya ziada inayo control Tanzania yaani DEEP STATE
 
Nukuu "Falsafa yake ya uongozi imejikita zaidi katika uzalendo wa utaifa kwanza kulijenga taifa katika nyanja ya kiuchumi na kuziba mianya ya unyonyaji katika wizi wa rasilimali za taifa" mwisho wa nukuu.
 
Back
Top Bottom