FALSAFA #2
: Kua muwazi na mwaminifu pale matatizo yanapokupata..
: Kua wa kawaida sana (Low profile) pale pesa inapokupatašš„¶
: Kua mnyenyekevu pale ambapo unapata madaraka na uongozi...!
Kwani kiburi hua kinatabia ya kukuchimbia shimo refu pasipo wewe,kutambua hivyo utashangaa ghafla umetumbukia.
: Na pia kua mtulivu pale ambapo hasira inapanda kutokana na makwazo....
Hii ndio ninayoita Falsafa#2
Usimamizi mzuri wa Fikra zako juu ya mazingiraš¤£
Katika FALSAFA #7
Ni heri niteseke ndani taratibu pekeangu,,,,huku nikiishughulisha Akili na Fikra katika kuumba suluhisho.
Kwa maana katika kuwaeleza watu shida na matatizo yangu..
Asilimia 70 Watafurahia na kucheka
Asilimia 25 watasema afadhali yamenikuta...
Asilimia 5 watajiangaisha kutatua
Sasa ni kwanini niusumbue utu wangu katika kujidhalilisha namna hii. Katika kundi kubwa la wasio maana.?
##4
Nilifikiria Nina shida na matatizo yangu kwamba ni makubwa kuliko ya wengine,lakini ilinibidi nicheke tu š¤£
Baada ya kumwona rafiki yangu ambaye alikua anahangaika kulipa madeni ambayo alikopa kwajili ya sherehe ya Harusi yake...
Na wakati huo tayari wameshatalikiana na Aliyekua mkewe.
#99
BINTI
Sikuizi wanaume nao wanawinda na kudate na kuoana na wanawake matajiri,utakufa single lady na style zako za kupika tu,Nenda katafute hela mama
Usisiburie mwanaume wa kuja kubeba na kutatua shida za huko kwenu
Utanisamehe ni utaniš¤£
#00
Mwaka huu hakuna wazo la biashara ambayo halikupita kwenye Akili yangu,,,
Duh pesa ngumu wakuu
Ndio maana sasa nafikiria mwakani ni bora nifungue kituo cha polisi tu tutajuana mbele kwa mbele
#####FALSAFA#6
Ninaamini Umbea na unafki unakufa pale unapofika kwenye sikio la mtu mwenye ufahamu na hekima....
Kwa maana umbea husambazwa na watu wenye chuki,
Na kuchukuliwa na kubebwa na wapumbavu....
Na kuaminiwa na wajinga
MWISHO
Content created by : magical power