Faini za Traffic Polisi

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,069
Reaction score
1,332
Habari wana JF.

Katika mfumo uliopita uliokuwa unatumiwa na Traffic kunakili makosa ya madereva/magari , ungepiga *152*75# ungepata taarifa zote i.e sababu ya Faini, kiasi cha kulipa, reference namba wakati unapolipa nk. Je kwanini huu mfumo (tracking) haufanyi kazi kuanzia July mwaka huu? Je kuna namba mpya za kutrack makosa zimetolewa?

Ahsante



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhan kuna maboresho/marekebisho yanafanyika kwa sasa, maana hata ile mikeka ya kukusanyia madeni haionekani barabarani sasahivi.
Kuna uwezekano mfumo wao ulikuwa linked na TRA maana toka kufutwa kwa hii kitu sijaona tena wakiweka na mikeka yao, naiman kuna marekebisho yanakuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani hizi faidi wanagawana wenyewe, siku moja nililipa faidi baada ya kulipa naitafakari hela niliyompa nikamwona trafiki akiagiza supu na chapati, hapo mie sijui chai ntapata wapi! Iliniuma sana.
 
Hivi inakuwaje wenye vituo vya mafuta tunawakomalia watumie efd mashine tena tunatishia na kuharibu pump, lakini hawa jamaa wa uhasama barabarabi wenyewe hawatumii efd.

Tuhamasishane hakuna kutumia gari, ukifika job lipaki hadi jioni na weekend hakuna kutumia gari hadi wanyooke, mauzo ya mafuta yakishuka watapata akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…