Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,663
- 729,778
Ni mafanikio ya kujivunia kwa mara ya kwanza katika historia ya jeshi la police kitengo cha barabarani kukusanya kiwango hicho cha pesa kutokana na makosa ya barabarani...ila nachelea kuwapongeza
Kimsimgi faini nyingi zilikuwa za uonevu na kwa kiasi kikubwa zimetokana na barabara mpya ya mwendo kasi ..ni barabara ngeni kwa matumizi ya Tanzania alama ni ngeni na lugha ni ya kiingereza..kitu ambacho ni changamoto kwa madereva wengi
Ukiachilia mbali utumiaji wa mashine za EFD ambazo pia zimesaidia mno kupaisha mapato yaliyokuwa yanapotelea mifukoni mwa wachache
Jeshi la police lilipaswa na bado linapaswa kutoa elimu ya matumizi ya barabara hii mpya kupitia vyombo vya habari na hata vipeperushi
Kujivunia kukusanya pesa hiyo wakati wananchi wengi hawana ufafanuzi wa kutosha kutokana na hiyo barabara tajwa sio sifa