Faida za Muswada mpya wa vyama vya Siasa

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
Mambo niaje wana JF wapambananji, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa punzi na kuweza ku-share nanyi mambo machahe juu yafaida za muswada mpya wa vyama vya siasa. Je mlikuwa mnayajua haya?:-

1. Kifungu cha 3 cha Muswada kimerekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya maneno Mkutano Mkuu wa Chama cha Siasa, Kamati Tendaji ya Taifa na Mwanzilishi wa Chama cha Siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki kinasaidia kutoa tafsiri ya misamiati iliyotumika katika sheria hii ambayo tafsiri za maneno hayo hazikuwepo

2. Kifungu cha 4 cha sheria ya sasa kimerekebishwa kwa kuongeza kifungu kidogo cha (5) ambacho kimeainisha kazi za Ofisi ya Msajili. Marekebisho haya ni mazuri kwa kuwa, Sheria ya saa haikutaja kazi za Msajili.

FAIDA:
Muswada umeainisha majukumu ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa, Msajili sasa anayo majukumu ya kufuatilia mapato na matumizi ya Vyama vya Siasa, kusimamia mienendo ya Vyama vya Siasa pia, kusimamia elimu ya kiraia inayotolewa na Vyama vya Siasa.
Aidha hii inasaida kwa kuwa Msajili anapofuatailia mapato na matumizi ya Chama cha Siasa itakupunguza au kufuta kabisa migogoro ya kifedha ndani ya Chama inayotokana na matumizi mabaya ya Rasilimali za chama kwa viongozi.
Vilevile, Msajili ataweza kudhibiti utoaji wa elimu ya uraia wenye lengo la kupotosha jamii, wenye nia ovu, na pia atajiridhisha na elimu ambayo inatokana na ufadhili wa asasi za kiraia zenye mlengo hasi kwa Taifa.

3. Muswada umeongeza pia, kifungu kipya cha 6(B) kinachotaja sifa za mtu anayetaka kusajili chama cha siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki ni kizuri kwa kuwa, kitasaidia kutambua uraia wa kila mwanzilishi wa chama na hivyo, kitazuia mapandikizi yenye lengo la kuhujumu nchi.
4. Ibara ya 7 imerekebisha kifungu cha 6A kwa kuweka masharti ya kuvitaka Vyama vya Siasa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Zanzibar na Sheria za nchi.

FAIDA:
Vyama vya Siasa vinatakiwa kupiga vita rushwa, kudumisha uzalendo, amani na utulivu. Vilevile, vinatakiwa kuzingatia Katiba ya chama husika, misingi ya Kidemokrasi, Utawala Bora, kuzingatia jinsia na kujumuisha makundi mbalimbali katika jamii.

5. Kifungu cha 6C kimetaja sifa za Mtu na mwanachama wa Chama cha Siasa.

FAIDA
:
Kifungu hiki kimezingatia uraia wa mwanachama wa Chama cha Siasa hii itaepusha kuwa na mapandikizi ambayo yana lengo la kuhujumu nchi na Pia kifungu hiki kimezuia mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti kwa wakati mmoja ili kuepusha mgongano wa maslahi.

6. Kifungu cha 8A kimerekebishwa kwa kuongeza vifungu vinavyoelekeza wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa kutunza kumbukumbu zote zinazohusu vyama vya siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki kinasaidia kutaja kumbukumbu ambazo zitatunzwa na Msajili. Kumbukumbu hizi zitajumuisha kumbukumbu ya vyama vya siasa, kumbukumbu ya Viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa na kumbukumbu ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya chama cha siasa.

7. Kifungu cha 8E kinakataza utaratibu wa vyama vya siasa kuanzisha, kufundisha na kuwa na ulinzi binafsi wa vyama.

FAIDA:
Masharti haya yanawezesha vyama vya siasa kujikita katika masuala ya kisiasa pekee na kuviacha Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutekeleza majukumu ya kisheria na kuhakikisha unakuwepo ulinzi wa usalama kwa vyama.

8. Kifungu cha 12(6) kinasema mtu hatatumia dini au taasisi ya kidini kufanikisha malengo ya chama.

FAIDA:

Kifungu hiki kitasaidia kujenga umoja wa kitaifa kwa kuzuia ubaguzi wa kidini kwenye uteuzi wa viongozi wa chama ambao ubaguzi huo unaweza kusababisha migogoro na wakati mwingine kupelekea machafuko kwenye jamii au kuchonganisha Serikali na jamii kupitia dini.

9. Muswada pia, unapendekeza kurekebisha kifungu cha 15 kwa lengo la kuvitaka vyama vya siasa kuwa na akaunti ya benki tofauti kwa ajili ya fedha za ruzuku.

FAIDA:
Kifungu hiki kitasaidia kujua matumizi ya fedha za ruzuku ndani ya vyama jambo ambalo litasaidia wanachama wadogo ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamikia matumizi mabaya ya ruzuku kwa vyama vyao bila kupewa mrejesho.

10. Muswada unapendekeza kurekebisha kifungu cha 18A kwa kuongeza kifungu kipya kinachohusu uwasilishwaji wa ripoti za kifedha.

FAIDA
:
Kifungu cha 18A kinapendekeza kurekebishwa ili kuweka masharti yanayohusu mwaka wa fedha wa chama cha siasa na kuvitaka vyama vya siasa kuwasilisha taarifa za hesabu zao kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi na pia, kuwasilisha taarifa ya hesabu zilizokaguliwa kwa Msajili.

11. Kifungu kipya cha 19 kinapendekeza kuongezwa ili kumwezesha Msajili kusitisha usajili wa chama cha siasa kitakachovunja masharti ya sheria.

FAIDA:
Itasaidia kuepusha uanzishaji wa vyama vya siasa kiholela; na Itafundisha jamii au wanaoanzisha vyama vya siasa kufuata utaratibu ulioainishwa kisheria.

12. Kifungu cha 21 kinapendekezwa ili kukataza mtu kuwa mwanachama wa Bodi ya Wadhamini wa chama cha siasa ikiwa mtu huyo ni kiongozi wa chama

FAIDA:
  • Itasaidia kuepusha kiongozi wa chama kuwa na nguvu kubwa ya kimaamuzi ndani ya Bodi; na
  • Itaepusha mtu mmoja kushika madaraka mengi ndani ya chama.
13. Kifungu cha 21B kimeongezewa kifungu kidogo cha 5 ambacho kinasema Baraza litafadhiliwa kutoka kwenye bajeti ya Serikali au fedha za wafadhili kupitia Serikali.

FAIDA:
  • Kifungu hiki kitasaidia kuwezesha fedha hizo kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujua matumizi na uhalali wake; na
  • Itasaidia Serikali kujua Mabaraza yanayodhaminiwa na watu wa aina gani na kwa maslahi yapi.
14. Kifungu cha 21D kinapendekeza kuongezwa ili kuimarisha makosa na adhabu na kusitishwa kwa usajili wa vyama vya siasa vitakavyokiuka masharti ya sheria.

FAIDA:
Itazuia chama au mtu ndani ya chama kufanya kosa kwa kuhofia adhabu zilizoainishwa kisheria.

15. Kifungu cha 21E (1) kinampa Msajili mamlaka ya kusimamia mwanachama yeyote wa chama cha siasa ambaye amevunja kifungu chochote cha sheria kutokufanya shughuli za kisiasa.

FAIDA:
Itasaidia utii wa sheria kwa chama na mwanachama kufanya shughuli za kisiasa kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kisheria.

16. Kifungu cha 21(3) kinampa Waziri Mamlaka ya kutunga kanuni zinazoelezea taratibu za kusimamishwa kwa mwanachama wa vyama vya siasa.

FAIDA
:
Kanuni zitasaidia kufafanua kipengele kuhusu namna ya kumsimamisha mwanachama na kuondoa utata ambao unaweza kuonekana kwenye sheria.

Naomba kuwasilisha wapambanaji wenzangu
 
Samahan ntoe.kwenye hyo list ya wapambanaji wa aina yako
 
Mnajisahau hamuwezi kuwa madarakani milele.
 
kwa kweli hivi vyama vya siasa visipodhibitiwa mwisho wa siku vitageuka vikundi vya kiuhalifu.....na Mabeberu hutumia hivi hivi vyama kuleta vita ili kuweka kiongozi wanaemtaka na kuvuna rasilimali zetu.....
LAZIMA MUSWADA UPITA KUWA NA NIDHAMU
 
hii ni sawa na kusikia jirani kila siku anampiga mke wake, hivyo ni la zima uingilie!!!!! bigup serikali
 
UCHAMBUZI MZURI....KUNA BAADHI YA MAMBO KINA ZITTO NA WASHIRIKA WENZAKE WANATUPOTOSHA
 
Tunashukuru sana kwa ufafanuzi, kwani ZITTO na wenzake walishafanya hapa ndo mahali pa kutupotosha.
 
kwa kweli hivi vyama vya siasa visipodhibitiwa mwisho wa siku vitageuka vikundi vya kiuhalifu.....na Mabeberu hutumia hivi hivi vyama kuleta vita ili kuweka kiongozi wanaemtaka na kuvuna rasilimali zetu.....
LAZIMA MUSWADA UPITA KUWA NA NIDHAMU
Gas inayochukuliwa na mabeberu iliuzwa na CCM kwa bei chee ili kujipatia fedha mifukoni mwao.

Umeona eeh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
15. Kifungu cha 21E (1) kinampa Msajili mamlaka ya kusimamia mwanachama yeyote wa chama cha siasa ambaye amevunja kifungu chochote cha sheria kutokufanya shughuli za kisiasa.
Binasi mi hiki kifungu kidogo kitakuwa kinareta mgogoro mkubwa sana kati ya msajili na Chama kwangu ningeshauri labda msajili autake mkutano mkuu kumvua uanachama huyo mwanachama aliyevunja sheria na kama wakishindwa basi msajili apeleke kesi mahakamani ili mahakama itoe uamuzi kidogo itapunguza presha
 
Mambo niaje wana JF wapambananji, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa punzi na kuweza ku-share nanyi mambo machahe juu yafaida za muswada mpya wa vyama vya siasa. Je mlikuwa mnayajua haya?:-

1. Kifungu cha 3 cha Muswada kimerekebishwa kwa kuongeza tafsiri ya maneno Mkutano Mkuu wa Chama cha Siasa, Kamati Tendaji ya Taifa na Mwanzilishi wa Chama cha Siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki kinasaidia kutoa tafsiri ya misamiati iliyotumika katika sheria hii ambayo tafsiri za maneno hayo hazikuwepo

2. Kifungu cha 4 cha sheria ya sasa kimerekebishwa kwa kuongeza kifungu kidogo cha (5) ambacho kimeainisha kazi za Ofisi ya Msajili. Marekebisho haya ni mazuri kwa kuwa, Sheria ya saa haikutaja kazi za Msajili.

FAIDA:
Muswada umeainisha majukumu ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuwa, Msajili sasa anayo majukumu ya kufuatilia mapato na matumizi ya Vyama vya Siasa, kusimamia mienendo ya Vyama vya Siasa pia, kusimamia elimu ya kiraia inayotolewa na Vyama vya Siasa.
Aidha hii inasaida kwa kuwa Msajili anapofuatailia mapato na matumizi ya Chama cha Siasa itakupunguza au kufuta kabisa migogoro ya kifedha ndani ya Chama inayotokana na matumizi mabaya ya Rasilimali za chama kwa viongozi.
Vilevile, Msajili ataweza kudhibiti utoaji wa elimu ya uraia wenye lengo la kupotosha jamii, wenye nia ovu, na pia atajiridhisha na elimu ambayo inatokana na ufadhili wa asasi za kiraia zenye mlengo hasi kwa Taifa.

3. Muswada umeongeza pia, kifungu kipya cha 6(B) kinachotaja sifa za mtu anayetaka kusajili chama cha siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki ni kizuri kwa kuwa, kitasaidia kutambua uraia wa kila mwanzilishi wa chama na hivyo, kitazuia mapandikizi yenye lengo la kuhujumu nchi.
4. Ibara ya 7 imerekebisha kifungu cha 6A kwa kuweka masharti ya kuvitaka Vyama vya Siasa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Katiba ya Zanzibar na Sheria za nchi.

FAIDA:
Vyama vya Siasa vinatakiwa kupiga vita rushwa, kudumisha uzalendo, amani na utulivu. Vilevile, vinatakiwa kuzingatia Katiba ya chama husika, misingi ya Kidemokrasi, Utawala Bora, kuzingatia jinsia na kujumuisha makundi mbalimbali katika jamii.

5. Kifungu cha 6C kimetaja sifa za Mtu na mwanachama wa Chama cha Siasa.

FAIDA
:
Kifungu hiki kimezingatia uraia wa mwanachama wa Chama cha Siasa hii itaepusha kuwa na mapandikizi ambayo yana lengo la kuhujumu nchi na Pia kifungu hiki kimezuia mtu kuwa mwanachama wa vyama viwili tofauti kwa wakati mmoja ili kuepusha mgongano wa maslahi.

6. Kifungu cha 8A kimerekebishwa kwa kuongeza vifungu vinavyoelekeza wajibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa kutunza kumbukumbu zote zinazohusu vyama vya siasa.

FAIDA:
Kifungu hiki kinasaidia kutaja kumbukumbu ambazo zitatunzwa na Msajili. Kumbukumbu hizi zitajumuisha kumbukumbu ya vyama vya siasa, kumbukumbu ya Viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa na kumbukumbu ya Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya chama cha siasa.

7. Kifungu cha 8E kinakataza utaratibu wa vyama vya siasa kuanzisha, kufundisha na kuwa na ulinzi binafsi wa vyama.

FAIDA:
Masharti haya yanawezesha vyama vya siasa kujikita katika masuala ya kisiasa pekee na kuviacha Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutekeleza majukumu ya kisheria na kuhakikisha unakuwepo ulinzi wa usalama kwa vyama.

8. Kifungu cha 12(6) kinasema mtu hatatumia dini au taasisi ya kidini kufanikisha malengo ya chama.

FAIDA:

Kifungu hiki kitasaidia kujenga umoja wa kitaifa kwa kuzuia ubaguzi wa kidini kwenye uteuzi wa viongozi wa chama ambao ubaguzi huo unaweza kusababisha migogoro na wakati mwingine kupelekea machafuko kwenye jamii au kuchonganisha Serikali na jamii kupitia dini.

9. Muswada pia, unapendekeza kurekebisha kifungu cha 15 kwa lengo la kuvitaka vyama vya siasa kuwa na akaunti ya benki tofauti kwa ajili ya fedha za ruzuku.

FAIDA:
Kifungu hiki kitasaidia kujua matumizi ya fedha za ruzuku ndani ya vyama jambo ambalo litasaidia wanachama wadogo ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamikia matumizi mabaya ya ruzuku kwa vyama vyao bila kupewa mrejesho.

10. Muswada unapendekeza kurekebisha kifungu cha 18A kwa kuongeza kifungu kipya kinachohusu uwasilishwaji wa ripoti za kifedha.

FAIDA
:
Kifungu cha 18A kinapendekeza kurekebishwa ili kuweka masharti yanayohusu mwaka wa fedha wa chama cha siasa na kuvitaka vyama vya siasa kuwasilisha taarifa za hesabu zao kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa ajili ya ukaguzi na pia, kuwasilisha taarifa ya hesabu zilizokaguliwa kwa Msajili.

11. Kifungu kipya cha 19 kinapendekeza kuongezwa ili kumwezesha Msajili kusitisha usajili wa chama cha siasa kitakachovunja masharti ya sheria.

FAIDA:
Itasaidia kuepusha uanzishaji wa vyama vya siasa kiholela; na Itafundisha jamii au wanaoanzisha vyama vya siasa kufuata utaratibu ulioainishwa kisheria.

12. Kifungu cha 21 kinapendekezwa ili kukataza mtu kuwa mwanachama wa Bodi ya Wadhamini wa chama cha siasa ikiwa mtu huyo ni kiongozi wa chama

FAIDA:
  • Itasaidia kuepusha kiongozi wa chama kuwa na nguvu kubwa ya kimaamuzi ndani ya Bodi; na
  • Itaepusha mtu mmoja kushika madaraka mengi ndani ya chama.
13. Kifungu cha 21B kimeongezewa kifungu kidogo cha 5 ambacho kinasema Baraza litafadhiliwa kutoka kwenye bajeti ya Serikali au fedha za wafadhili kupitia Serikali.

FAIDA:
  • Kifungu hiki kitasaidia kuwezesha fedha hizo kukaguliwa na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili kujua matumizi na uhalali wake; na
  • Itasaidia Serikali kujua Mabaraza yanayodhaminiwa na watu wa aina gani na kwa maslahi yapi.
14. Kifungu cha 21D kinapendekeza kuongezwa ili kuimarisha makosa na adhabu na kusitishwa kwa usajili wa vyama vya siasa vitakavyokiuka masharti ya sheria.

FAIDA:
Itazuia chama au mtu ndani ya chama kufanya kosa kwa kuhofia adhabu zilizoainishwa kisheria.

15. Kifungu cha 21E (1) kinampa Msajili mamlaka ya kusimamia mwanachama yeyote wa chama cha siasa ambaye amevunja kifungu chochote cha sheria kutokufanya shughuli za kisiasa.

FAIDA:
Itasaidia utii wa sheria kwa chama na mwanachama kufanya shughuli za kisiasa kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa kisheria.

16. Kifungu cha 21(3) kinampa Waziri Mamlaka ya kutunga kanuni zinazoelezea taratibu za kusimamishwa kwa mwanachama wa vyama vya siasa.

FAIDA
:
Kanuni zitasaidia kufafanua kipengele kuhusu namna ya kumsimamisha mwanachama na kuondoa utata ambao unaweza kuonekana kwenye sheria.

Naomba kuwasilisha wapambanaji wenzangu
Kuna Faida tu?
 
Waheshimiwa Wabunge tabia ya kupitisha Miswaada kwa Maslahi ya Vyama vyetu ni Janga la Taifa.Tumeshuhudia hivi karibuni tukiifanyia marekebisho Makubwa baadhi ya Miswaada yetu iliyopitishwa kwa Shinikizo la kisiasa na kulisababishia Taifa Hasara kubwa.Hivi karibu Bunge lilipitisha Sheria Mpya ya Mafao na kuzusha Mtafaruku mkubwa mpaka Mh.Rais akaingilia kati na Kuamuru Sheria ya Kikokotoo cha zamani kiendelee kutumika.Hivi sasa kuna Muswaada wa Sheria za Vyama vya Siasa , Muswaada ambao unapingwa na Wadau ni vema Wabunge wetu wakawa makini kwani usipoondolewa vipengere vyenye Utata utakuja kuwa tatizo kwa mustakabali wa Vyama vyetu sio Chama tawala au Vyama vya Upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo kubwa la wabunge wetu ni kutokuwa na uhuru wa mawazo! Hivyo watakachokifanya nikusubiri vyama vyao vina misimamo gani ili nao wafuate! Kibaya zaidi ni kuwa endapo watafanya tofauti na matakwa ya vyama vyao hatua za kinidhamu zinawahusu!
 
Wale wabunge yawezekana wanafanya makusudi sio bure.Wamegundua kuwa vyuma vimekaza hadi bungeni.
Au wanajipangia kustaafu Nov 2020 hawataki kujitengezea matatizo,kwani wanajua watakatwa majina yao.
 
Back
Top Bottom