Faida za M-PESA VODACOM kwa wateja wake kila mwisho wa mwezi

victor2015

Member
Jul 24, 2015
53
8
Kumekuwa na uelewa mdogo kuhusu faida za m-pesa kwa kila mtumiaji wa Huduma ya m-pesa Vodacom. Mwezi wa sita katikati nimebahatika kujua kumbe vodacom wanatoa faida kila mwisho wa mwezi kwa mteja yoyote anayetumia m-pesa na wanasema kujua faida yako tuma neno KIASI kwenda 15300 na utapokea Ujumbe unaokuarifu faida yako na kukuekeza kuwa utaipata mwisho wa mwezi.

Sasa imefika mwezi wa sita sijawekewa hiyo faida na leo ni tarehe 2July nikaamua kuwapigia Vodacom na kuataarifu kuhusu faida yangu wakaniuliza meseji imekuletea unapata faida kiasi gani nikawajibu Meseji nimetuma hata Leo 3July inasema faida yangu ni tsh 11,546 na utapata kabla ya June 20, 2016, wakaniambia nisubiri ndani ya Massa 72 faida yangu nitakuwa nimeshaipata.

ANGALAZO NA UMAKINI KWA WANA JF: Vodacom inaonyesha kitengo cha mpesa hakiwi makini na kuna mchezo unafanyika huduma hii imeanza muda mrefu je ni faida ngapi hazijaingia muda wa huko nyuma? Naamini wateja wengi hawajui hii faida basi wana JF fuatilieni na tupeane mrejesho.
Nawakilisha hata kama nimekosea kujieleza tusaidiane.
 
Utapokea Tsh 11546 kabla ya 30.6.2016 kama faida ya kutumia M-Pesa. You will receive Tsh 11546 before 30.6.2016 as your benefit for using M-Pesa.
 
Ombi lako lililopokelewa na FN limepewa namba CSR156006579. Tutakujulisha punde tu litakapotatuliwa. Asante kwa kuchagua Vodacom.
 
Nimecheki aise Ni 43,300.... So niwatwangie?
Watwangie Mkuu pia jiulize huko miezi ya nyuma zimeenda wapi? Au ndio wametupiga? Ila nimewapigia wameniambia Ngoja hiyo ya mwezi wa sita iingie kwanza ndio niwapigie kwa kuuliza miezi ya nyuma
 
Back
Top Bottom