Faida za kula ndizi mbili kwa siku

amfather93

New Member
Feb 15, 2018
1
0
NDIZI ni kati ya matunda yanayopatikana katika maeneo yetu,basi leo nataka nikushirikishe faida kuu utajazopata kwa kula ndizi mbili tu kwa siku:
->Ndizi husaidia kuondoa tatizo la allergy -ndizi ina acidi za amino ambazo husaidia kupunguza matatizo ya allergy.
->Ndizi huongeza nishati -ndizi zimeundwa na sukari kama fructose,sucrose na glucose ambazo husaidia kuupatia mwili nishati yaani nguvu.
->Ndizi husaidia kutibu kuhara -ndizi hutumika katika kutibu kuhara kwa kusawazisha njia ya mmeng'enyo wa chakula.
->Ndizi husaidia kuondoa uchovu -mchanganyo wa ndizi asali na maziwa husaidia kuondoa uchovu,husawazisha njia ya mmeng'enyo wa chakula na huongeza maji mwilini.
->Ndizi husaidia kuacha sigara -ndizi ina madini ya magneziamu na potashiamu ambayo husaidia kuondoa nikotini ambayo nisumu inayopatikana kwenye sigara.
->Ndizi huongeza mood -ndizi zina amino acid inayoitwa tryptophan ambayo hutoa hormone inayoitwa serotonin ambayo husaidia kuongeza mudi.
->Huongeza ufanisi wa ubongo -.madini ya potassium yanayopatikana kwenye ndizi husaidia ufanyaji kazi vizuri wa ubongo na kuwa active
->Hutibu upungufu wa damu -ndizi zina madini ya chuma ya kutosha hivyo husaidia kwenye kutibu upungufu wa damu na huongeza damu mwilini.
->Hutibu kuhara damu -juisi ya ndizi husaidia kutibu kuharisha damu kwa watoto.

Kwa tatzo lolote kiafya usisite kuwasiliana nami DM kwa ushauri zaidi#afya#ndizi#health#tanzania
Screenshot_2018-09-06-21-16-54-01.jpeg
 
UMESAHAHU FAIDA MOJA: INAKATA POMBE KWA MUDA...YAANI HANGOVER...nikaona nazingua kwahiyo huwa najiununulia karafuu ya ths 100. HAPO NIMEPUNGUZA BAJETI (ndizi 2 ni tsh 400) NA PIA NIMEKATA HARUFU YA POMBE WIKI NZIMA.
 
Back
Top Bottom