Faida za Komamanga

Faida za Komamanga

Herbalist Mtaturu

Senior Member
Joined
Aug 17, 2023
Posts
171
Reaction score
259
🌱 FAHAMU KUHUSU KOMAMANGA 🌱
Tunda la komamanga (kwa Kiingereza pomegranate, jina la kisayansi huitwa: Punica granatum) ni tunda lenye nguvu kubwa ya kiafya na hutumika sana katika tiba za asili.

🌿 Maradhi Ambayo Komamanga Hutibu 🌿

👉1. Tezi dume (Prostate health):
- Juisi ya komamanga hupunguza uvimbe na kusaidia kupambana na saratani ya tezi dume.

👉2. Shinikizo la damu (High blood pressure):
- Inasaidia kupunguza shinikizo kwa kuboresha mzunguko wa damu.

👉3. Sukari (Diabetes):
- Hupunguza kiwango cha sukari mwilini na kuimarisha usikivu wa insulin.

👉4. Saratani (Cancers):
- Antioxidants zake huzuia kuenea kwa seli hatari, hasa saratani ya matiti na tezi dume.

👉5. Moyo (Heart health):
- Huzuia mishipa ya damu kuziba na kupunguza cholesterol mbaya.

👉6. Vidonda vya tumbo (Ulcers): Tumbo kujaa gesi, pia asidi na kuhara damu
- Maganda yake husaidia kuponya vidonda vya tumbo.

👉7. Nguvu za uzazi:
- Huongeza uzalishaji wa shahawa na nguvu kwa wanaume, pia husaidia mzunguko wa hedhi kwa wanawake na kupevusha mayai.

👉8. Kutibu mawe kwenye figo, minyoo aina ya tegu
👉9. Hutibu uvimbe wa wengu (spleen) , pia homa ya ini.
👉10. Huondoa sumu za kemikali mbalimbali katika mwili

Namna ya Kutumia

⚡1. Juisi ya tunda:
- Kunywa glasi 1 kila siku, hasa asubuhi kabla ya chakula.

⚡2. Maganda yaliyokaushwa:
- Saga maganda na chemsha kijiko 1 kwenye kikombe cha maji.
- Kunywa mara 2 kwa siku kwa vidonda vya tumbo au matatizo ya mdomo.
⚡3. Mbegu mbichi:
- Tafuna au changanya na asali kwa nguvu za uzazi.

⚡4. Mizizi (kwa wataalamu wa tiba asili):
- Mizizi yake huchemshwa kwa kuondoa minyoo tumboni na kutuliza homa.

🔥 Tahadhari:
Wenye matatizo ya figo au wanaotumia dawa kali za presha au damu wanapaswa kutumia kwa uangalifu.

Je, una changamoto yeyote kuhusu afya tuweze kukusaidia??
Iwe changamoto ya kimwili ama kiroho,

Kwa ushauri na tiba za maradhi mbalimbali wasiliana nami.
 

Attachments

  • FB_IMG_1755426338270.jpg
    FB_IMG_1755426338270.jpg
    25.4 KB · Views: 25
  • FB_IMG_1755426455832.jpg
    FB_IMG_1755426455832.jpg
    134.5 KB · Views: 21

Similar Discussions

Back
Top Bottom