Faida za kiafya za Biringanya

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
204
451
Biringanya ni moja ya vyakula maarufu sana katika jamii nyingi ulimwenguni. Hupatikana pia kwenye maeneo mengi ya bara la Afrika. Kwa upande wa nchi za Ulaya, hupikwa kama kifurahisha kinywa (snack).

IMG_6752.jpeg


Biringanya ni nini?
Pamoja na nyanya, viazi na pilipili hoho, Biringanya (Solanum melongena) ni ya familia ya mmea wa nightshade (Solanaceae). Biringanya hukua kwa njia kama nyanya, zikining'inia kutoka kwa miti ya mmea unaokua kwa urefu wa futi tofauti. Zina ngozi ya rangi ya zambarau inayong'aa, ndani yenye rangi ya krimu, kama sifongo iliyo na mbegu ndogo zinazoweza kuliwa.

Mbali na aina ya zambarau ya kawaida, biringanya zinapatikana katika rangi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kijani kibichi, chungwa na manjano, na pia zinapatikana katika aina mbalimbali za maumbo na ukubwa.

Virutubisho vyake
Vifuatavyo ni baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye Biringanya;
  • Nishati
  • Protini
  • Mafuta
  • Wanga
  • Nyuz lishe
  • Potassium, Copper, Manganese, Vitamini B6 na Thiamine
  • Kampaundi za phenolic ambazo hutumika kama viondoa sumu
Faida kwa afya
1. Inaweza kudhibiti sukari

Biringanya ni chanzo kizuri cha nyuzi lishe na kiwango cha chini cha mafuta na sukari, na hivyo kuzifanya kuwa mjumuisho mzuri kwa wale wanaodhibiti ugonjwa wa aina ya 2 ya kisukari. Tafiti za afya zinaweka bayana kuwa mboga hii hufaa kwa watu wenye aina ya 2 ya kisukari.

2. Afya ya ubongo
Huwa na kampaundi za 'nasunin', ambazo hulinda mafuta yanayotengeneza kuta za seli za ubongo, huongeza uwezo wa kutunza kumbukumbu pamoja na kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya akili.

3. Inaweza kusaidia kudhibiti cholesterol
Husaidia kushusha chini aina mbaya ya mafuta ya cholesterol, maarufu kama Low Density Lipoprotein (LDL) ambayo husababisha kuziba kwa mishipa ya damu na kuhatarisha afya ya moyo, kuchochea kiharusi pamoja na shinikizo kubwa la damu.

Pia, biringanya husaidia;
  • Kuboresha afya ya macho
  • Kutunza uzito sahihi wa mwili
  • Kulinda seli za mwili na kuzuai aina mbalimbali za saratani.
Chanzo: Medical News Today
 
Mkuu shukurani kwa bandiko hili la lishe lililo katika Kiswahili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom