Faida ya tunda la karoti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida ya tunda la karoti

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Faida ya matumizi ya zao la karoti pamoja na faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa zao hilo, ambalo kimsingi mizizi yake ndiyo hasa zao lenyewe.

  kumbuka kuwa karoti inalimwa karibu kila pembe ya dunia hii. Zao hili linatofautiana katika rangi, kwani kuna karoti nyeusi, zenye rangi ya pinki, nyekundu na njano. Karoti yenye rangi nyekundu na njano ndiyo hasa tunayolima hapa TZ. Karoti za rangi nyekundu na njano ndizo zinasemekana kuwa na virutubisho vingi sana kuliko karoti nyingine.


  [​IMG]
  Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama tulivyoona kwa tunda la avocado. Pia ina asili ya wanga, na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C na E. Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa beta-carotene ambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.

  Karoti ikitumiwa vizuri na tena mara kwa mara inasaidia kukinga na kuponya magonjwa yafuatayo: macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.


  [​IMG]
  Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine, inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye salad ya matunda au mbogamboga. Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili.

  Mada nyingine nitazungumzuzia kazi ya virutubisho vilivyomo ndani ya karoti.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  ahsante kwa elimu
   
 3. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Eti mzizi kuna mtu kaniambia ukidondoshes matone mawili au matatu kila siku kwenye macho; macho yanatakata na kuwa meupe ( imean yenye rangi nzuri angavu) maana binafsi napenda macho yangu yawe meupe bila madoadoa. kwa ufupi mimi pia ni mpenzi wa karoti kwa matumizi mbalimbali.
   
 4. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Kitu kingine naomba unifafanulie matumizi ya kila siku ya mlonge, faida na hasara zake. maana binafsi nimeshawishika kuanza kuutumia ingawa sijui kama una madhara maana kwenye vijarida vingi wanasema hauna madhara.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  ....Mkuu MziziMkavu mie natafuna sana hizi nimetokea kuzipenda kwa muda mrefu sasa. Ahsante kwa juhudi zako.
   
 6. m

  manasa Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanx jamani kwa faida za karoti
   
 7. G

  Greard Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashukuru mkuu. Naomba ufafanuzi ni jinsi gani unaweza kudondosha matone ya maji ya karoti kwenye macho bila madhala. LKN KAROTI SIO TUNDA Kama ulivoweka kwenye heading.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu@Greard Karoti unaweza kula pasipo na kupika na pia waweza kupika unaweza kuita karoti ni aina fulani ya mboga au tunda inategemea utakavyotumia wewe mwenyewe.
   
 9. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #9
  May 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante sana.
   
 10. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mzizi, still waiting the answer!
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  @Rubi uliyoyasema mimi siyajuwi lakini jaribu kufanya hivyo kisha uangalie je itawezekana hivyo alivyokukwambia huyo jamaa? siwezi kukuongopea mimi sipendi kusema maneno ya uongo jaribu kisha unipe na mimi Feedback.
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  @Rubi Mti wa Mlonge una faida nyingi tu kwa binadamu mojawapo ni hizi hapa.

  Moringa (Moringa spp.) maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao
  haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na
  kusafisha maji.

  i) Majani ya mti wa Moringa ii) Maua ya mti wa Moringa iii) Mbegu za mti wa Moringa
  1. Virutubishi

  Faida na matumizi ya mti wa Moringa
  Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa
  Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza

  ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi.
  Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.
  Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi
  hivi ni pamoja na;

  Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango
  chake katika majani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.
  Calcium (madini chuma)- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini.

  Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.
  Protini- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya
  Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.

  Vitamini A- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake
  katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.
  Potassium- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya

  Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi.
  Maua ya Moringa yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au
  kupikwa na kuliwa kama mboga.

  2. Mboga
  Majani ya Moringa huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati
  wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani.
  Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga).
  Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.

  3. Mafuta
  Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia
  hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka
  kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.

  4. Lishe ya Mifugo
  Majani ya Moringa huliwa na ng¡¦ombe, mbuzi, kondoo, sungura na kuku. Mbegu huliwa na kuku pamoja na wanyama wengine kwenye jamii ya ndege.

  5. Pambo la nyumba
  Mti wa Moringa hupandwa kwa wingi kwenye bustani kama ua au mti wa kivuli na hutumika katika upambaji. Pia miti ya moringa ikipandwa karibu karibu inaweza kutumika kama fensi.

  6. Chanzo cha kipato
  Mti wa Moringa ukitumiwa vizuri ni chanzo kizuri cha kipato. Mfano ni uuzaji wa miche ya mti wa moringa na utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na moringa.

  7. Tiba mbadala
  Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.
  „
  « Majani
  ¡E Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
  ¡E Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali

  inatibu kuharisha.
  ¡E Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.
  ¡E Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
  „
  « Mbegu
  ¡E Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
  ¡E Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
  „
  « Magome
  ¡E Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung¡¦atwa na wadudu kama nyoka na nge.

  Matumizi mengineyo

  Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka.

  Mti wa Moringa unaota katika mazingira yote, kwenye ukame na meneo yenye maji. Angalizo huchukuliwa kuhakikisha kuwa maji hayatuami kwenye mti kwasababu maji huweza kusababisha ugonjwa na kufanya mizizi ioze. Karibu aina zote za udongo zinafaa kwa mti wa Moringa. Mbegu, kipande cha tawi na hata mzizi vinaweza kutumika koutesha mti wa moringa.

  Namna ya kupanda mti wa Moringa
  I. Mbegu

  Mbegu iliyokomaa ya mti wa Moringa hulowekwa siku moja kabla ya kuoteshwa, kama maji sio tatizo mbegu inaweza kupandwa moja kwa moja kwenye udongo baada ya kuchimba shimo, weka maji na kisha changanya udongo na samadi angalau kilo tano kabla ya kupanda mbegu halafu endelea kumwagilia katika miezi ya mwanzo. Baada ya angalau siku kumi na tano mbegu inatakiwa iwe imeshachipua.
  Pia unaweza kuotesha mbegu za Moringa katika vifuko kwenye kitalu kisha kuhamishia shambani baada ya kuota.

  II. Kipande cha tawi
  Vipande vya tawi lililo komaa huweza kutumika katika kupanda mti wa Moringa, hivi hupandwa eidha moja kwa moja shambani au kwenye vifuko katika kitalu. Kama ukipandwa moja kwa moja angalau robo moja ya tawi inatakiwa ipandwe kwenye udongo, usimwagilie maji mengi sana kwani inaweza kusababisha kuoza.

  [​IMG]
   
 13. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Mzizi Shukrani hakika umenijibu vyema. Nafikiri nimepata ufahamu zaidi kuhusu Moringa na kuhusu kudondoshea matone ya juis ya caroti kwenye macho nitajaribu maadamu si sumu. Unajua zamani nilikuwa nina aleji sana ya macho hasa kipindi cha kiangazi ambacho kunakuwa na vumbi jingi, macho yalikuwa yananiwasha sana na kila wakati nikawa nayafikicha hivyo kusababisha kuwa mekundu muda wote na kuniuma. pamoja na dawa za hosipitali nilizokuwa natumia bado niliendelea kusumbuliwa.

  Kuna mama mmoja akaniambia niwe nadondoshea matone ya maji kama mawili yaliyochanganywa na chumvi na sukari. Kwa kweli sikufichi kwa jinsi nilivyokua nahangaika nikawa nafanya hivyo unapodondoshea lile tone la maji yaliyochanganywa na sukari na chunvi cha moto unakiona unakua kama umeweka pilipili lakini kama dk moja jicho linapoa kisha nanawa na maji yabaridi so baada ya muda nilipata nafuu muwasho na kujifikicha kulipungua.

  Ila mimi baadae niliogopa nisije kuja ua macho yangu hapo baadaye maana najua sukari inachangia kuua macho.

  Hivyo baada ya kuperuzi huku na huku nilipata dawa ambayo ni kula karoti kwa wingi (in everyday life) nanasi, mbogamboga pia kuacha matumizi ya sukari na badala yake kutuma asali mbichi kwenye vinywaji vinavyohitaji sukari. Kwa kweli nina muda zaidi ya miaka mitano sisumbuliwi na macho na kila siku huwa naona macho yangu yana nguvu hata ya kusoma vile viandishi vidogo sana.

  Na ninanomba Mungu anisaidie yadumu katika hali hii. that's why nazidi kutafuta jinsi ya kuyatunza na kufanya yaendee kuwa na nuru. si unajua jicho linapokuwa na Nuru unauhisi hata mwili wako kuwa una nuru ukiachia mbali maradhi yanayotukabili kila kukicha.
   
 14. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  KAROTI; KINGA DHIDI YA SARATANI UGONJWA WA MOYO

  [​IMG]
  WIKI iliyopita tulianza kuangalia umuhimu wa karoti kwa afya ya binadamu. Leo tunendelea na sehemu ya pili na ya mwisho juu ya mada hii. Endelea...

  Kama karoti imestawishwa kwa kutumia madawa ya mimea na mbolea au kama huna uhakika na usafi wake, ni vizuri ukwangue maganda yake ya juu na kuyaondoa. Unaweza kuamua kukata vipande virefu au vya mviringo, kukata na mashine maalum vipande vidogo vidogo au kula nzima nzima.

  Karoti ni tamu vyovyote utakavyoamua kuila, iwe mbichi au iliyochemshwa. Ingawa kula karoti mbichi ni bora zaidi, lakini hata ukila iliyopikwa bado haipotezi virutubisho vyake, zaidi inaelezwa kuwa, kambalishe, virutubisho pamoja na sukari yake inapatikana kirahisi na hivyo kuifanya kuwa tamu.

  Jambo la kuzingatia kama ukiamua kuipika, usiipike sana, bali inatakiwa kuchemshwa au kupikwa kwa muda mfupi ili virutubisho vyake visipungue au kupotea kabisa.

  DONDOO ZA KUTENGENEZA KAROTI
  Unaweza kuitengeneza karoti kama unavyotaka ili kupata ladha tofauti bila kupoteza virutubisho vyake. Unaweza, kwa mfano, kutengeneza saladi ya karoti kwa kuchanganya na majani yake kwa kukatakata vipande.

  Aidha, unaweza kutengeneza saladi kwa kukata vipande vidogo vidogo kisha kuchanganya tufaha na matango na kula pamoja kwenye mlo wako wa siku kama kachumbari.

  Unaweza kutengeneza supu ya karoti kwa kuchemsha vipande vyake na nyanya. Chukua karoti na nyanya ulizochemsha, kisha weka kwenye blender' au chombo kingine unachoweza kusagia. Saga mchanganyiko huo ili kupata supu, unaweza kuongeza viungo vingine ili kupata ladha. Unaweza pia kuinywa ikiwa ya moto au ikiwa imepoa.

  Kinywaji kingine unachoweza kutengeneza kwa afya yako ni juisi ya karoti, soymilk' na ndizi mbivu. Tengeneza nusu glasi ya juisi ya karoti, chukua glasi moja ya soymilk na ndizi mbivu moja kisha changanya kwa kutumia blender'. Kama huna changanya kwa kutumia kijiko au mwiko na kupata milk shake' ya ukweli.

  KAROTI IKIZIDI MWILINI
  Ingawa siyo rahisi kutokea lakini inawezekana kuna watu matumizi ya mboga hii kwao yako juu. Karoti ikizidi mwilini, huweza kumfanya mtu aonekane wa njano', hasa katika sehemu za viganja vya mikono, nyayo za miguu na nyuma ya masikio. Kitaalamu hali hii hujulikana kama carotoderma'.

  Hata hivyo, hali hiyo hutoweka pale mtu huyo anapopunguza ulaji wa karoti au vyakula vingine vyenye kiwango kikubwa cha virutubisho vya carotene' na hakuna madhara mengine anayoweza kuyapata.
  Mwisho, katika nchi za Asia, ambako ndiko karoti inaelezwa kuanzia, inaaminika pia kuwa na uwezo wa kurekebisha masuala ya nguvu za kiume na ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi (sexual dysfunction & sexual drive).

  Pia karoti inaaminika kuimarisha ufanisi wa figo na kuondoa hewa chafu na baridi mwilini. Baada ya kujua faida za karoti, bila shaka kuanzia leo umepata sababu ya kuiangalia upya karoti kama mzizi' muhimu kwa afya yako.
   
 15. C

  CHADEMA Mpya Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda mada yako kuhusu karoti,ni ya muhimu sana kiafya.ila huo mlonge ndo umeniacha na maswali maana naujua mmoja unaostawi sana kwenye mkoa wa Tanga.Una harufu sana hauwezi kutumia majani yake kwa kula ukiwa mbichi kwa sababu ya harufu yake mbaya!
   
 16. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu nimekupata na asante sana kwa ufafanuzi wako
   
 17. M

  Muwazi JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2014
  Joined: May 16, 2014
  Messages: 355
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Dr. MziziMkavu, nashukuru sana umetoa somo zuri sana ila nina swali juu ya mti wa mlonge. Nimewahi kusikia kuwa mlonge unatibu ugonjwa wa bawasiri (Hemorrhoids) lakini sijajua kuwa kama inatibu unafanyaje yaani unaiandaaje ili iwe tiba kamili ya bawasiri. Naomba maelezo ili niwe na uelewa kuhusu hili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Dec 8, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Unaweza kuponda ponda hayo majani ya mlonge kishaukajipaka sehemu ya siri iliyotoka hiyo Bawasiri au unaweza kutwanga magome yake upate unga uchanganye na maji ujipake sehemu zasiri iliyotoka hiyo bawasiri utapona.
   
 19. M

  Muwazi JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2014
  Joined: May 16, 2014
  Messages: 355
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Dr. MziziMkavu nimekupata lakini naomba usinichoke maana uelewa ndo natafuta zaidi.

  1: Ina maana hayo majani ukishaponda unakuwa unasugulia ile sehemu iliyoathirika?

  2: Huo unga wake unaweza kuchanganya na mafuta ya mwili badala ya maji?

  3: Katika kutumia, kuna masharti yoyote?

  4: Je, kuna vyakula ambavyo unatakiwa kuviepuka kula wakati unao huo ugonjwa?

  5: Maziwa huwa yanasemekana kuwa yasitumike ikiwa unatumia aina ya dawa Fulani. Je, kwa dawa ya mlonge hakuna madhara yoyote yatokanayo kwa kutumia maziwa?

  Yangu ni hayo tu Dr.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2014
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Majani ukisha ponda unajipaka sehemu ya siri au unga unaweza kuchanganya na mafuta ya nazi ukajipaka hiyo sehemu iliyoathirika. Na unaweza kuchemsha majani ukanywa maji yake. Lakini huo ugonjwa unatibika Ma-Hospitali kwanini huendi kujitibia Hospitalini? Kama hujapona na unataka mawasiliano na mimi bonyeza hapa.Mawasiliano
   
Loading...