Faida ya Password katika simu za wenzi wenu

Faida ya Password katika simu za wenzi wenu

kampelewele

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2014
Posts
2,998
Reaction score
2,414
Kila siku tunasisitiza kujua password za marafiki au wake/waume zenu wanaochati na na jinsi tofauti hamsikii. Sasa faida yake ni kama ifuatayo:



KWELI
mchepuko siyo dili!

Kauli hii imedhihirika kufuatia mwanadada, Ashura Maulid, mkazi wa Ilala jijini Dar, kukumbwa na mauti kwa madai ya kunyongwa ndani ya gesti na mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Charles ambaye inasemekana ni mpenzi waliyekutana kwenye mtandao wa kijamaii wa Facebook.




Marehemu Ashura Maulid enzi za uhai wake

Tukio hilo lililojaa majonzi tele na kuacha maswali mengi, hasa kwa mume wa marehemu, Suleiman Othman, lilijiri Mei 19, mwaka huu kwenye nyumba ya kulala wageni (jina lipo) iliyopo kandokando ya barabara ya kutoka Sinza Afrikasana kwenda Kijitonyama kupitia Kituo cha Polisi cha ‘Mabatini', Dar.

Chanzo kinadai kuwa, enzi za uhai wake, mwanadada huyo alikuwa akijihusisha na biashara ya kuuza duka la friji maeneo ya Sinza ya Afrikasana na inasemekana amekuwa ndani ya ndoa na mumewe, Suleiman kwa miaka 15 na kujaliwa kupata watoto wawili, wa mwisho akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

Akizungumza na Uwazi, Ijumaa iliyopita huku akiwa katika majonzi mazito, mume huyo alisema Jumanne ya Mei 19, mwaka huu, mkewe alimuaga anakwenda kazini huku akiumwa, alimtaka apumzike lakini mwanamke huyo akasema anajiona amepona hivyo ana uwezo wa kumudu majukumu yake.

"Ilipofika saa moja usiku akanitaarifu kuwa ameshatoka kazini. Cha ajabu mpaka saa nne usiku alikuwa hajafika nyumbani na nilipompigia simu hakupokea."Mara kwa mara mke wangu alipokuwa akimaliza kazi na kuanza safari ya kurudi nyumbani alikuwa ananitaarifu, nachati naye kila wakati mpaka anafika.

Siku hiyo nilikuwa nina majukumu mengi aliponitaarifu kamaliza kazi ndo' anarudi sikuwa na presha.

"Sasa ilipofika saa nne mimi nikiwa nyumbani na simu hapokei, nikashangaa. Mbaya zaidi, baadaye simu yake ikawa haipatikani kabisa."Nilifanya jitihada za kumtafuta kwa ndugu na jamaa, vituo vya polisi na hospitali mbalimbali, ikiwemo Muhimbili kuulizia kwenye wodi za wagonjwa lakini sikumkuta.



Mume wa marehemu Ashura Maulid.

"Juzi (Mei 20), nilishtuka kupigiwa simu na polisi wa Kijitonyama, wakaniambia kuna maiti imekutwa mahali (walimficha kama ilikuwa gesti) na aliyehusika na mauaji ni mwanaume ambaye walianza kufahamiana na mke wangu kupitia Facebook. Walisema marehemu alionekana alikufa kwa kunyongwa.

"Waliniambia huyo mwanaume alikimbia baada ya kufanya mauaji hayo. Palepale ndo' wakaanza jitihada za kumtafuta mpaka wakamkamata," alisema mume huyo.Akiendelea kuelezea tukio hilo alisema kisa cha kugundua kuwa Charles alikutana na mke wake kwenye Facebook ni siku ya tukio baada ya mawasiliano waliyoyafanya kwa kipindi kirefu bila yeye kujua.

Kutoka Globalpublishers

Alisema ilionesha kuwa, siku hiyo waliamua kuonana laivu ambapo alimkaribisha dukani kwake na kuondoka naye baada ya kumaliza kazi na kufunga duka huku akiwa amemtaarifu bosi wake (si mumewe) fedha zilizopatikana siku hiyo."Niliambiwa na rafiki wa mke wangu kuwa siku hiyo mwanaume huyo alifika dukani kwa mke wangu akawatambulisha mashosti zake kuwa ni rafiki yake waliyejuana Facebook.

Wakiwa hapo, mke wangu alimpigia simu bosi wake kumwambia siku hiyo aliingiza shilingi milioni moja na laki saba. Huenda hicho ndo' kilimfanya jamaa amgeuke na kumuua kwa tamaa ya zile fedha," aliongeza.

Mumewe huyo alisema, haamini kama mkewe alishindwa kuiheshimu ndoa yake na kuwapa nafasi wanaume wengine tena kwa kwa mtu ambaye hakufahamiana naye ila kwa kukutana naye kwenye mtandao na kuanzisha uhusiano kwani yeye alimtosheleza kwa kila jambo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura alipotafutwa ili aulizwe kuhusiana na tukio hilo, simu yake iliita bila kupokelewa.Uwazi lilipofika kwenye gesti hiyo ambayo marehemu alifia chumba Namba 4.

Lakini wahusika waligoma kutoa ushirikiano na kudai hakukuwa na tukio hilo.
Kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini' faili Namba KJN/RB/5081/15 TAARIFA YA KIFO huku mtuhumiwa akishikiliwa hapo baada ya kukamatwa akiwa na gari aina ya Toyota Carina (namba za usajili zipo).
 
kuna mambo mengine yanatia hasira sana ila ndo basi mtu unakua huna jinsi!! naanzaje kuwa na mpenzi tena kwa njia ya mtandao na wakati nina mume ndani!! mambo mengine tunajitakia wenyewe haya Mola akamueke pale alipopachagua mwenyewe alipokua hai
 
Nadhan haya n malipi ambayo allah hutoa kwa waja wake hv kwel wapata mchepuko kupitia fb tn ukiwa ktk ndoa.mmmhhh
 
n mcba hasa ila cjakuelewa hyo faida ya password hapo imekujaje?
Kama mwanaume angalikuwa anafungua fungua simu ya huyo mama angelimfumania na wala asingechepuka. Hiyo ndiyo faida ya aidha kutoweka password katika simu au kuiwacha wazi. Naamini ukiona mwenzi anag'ang'ania simu yake jua ni michepuko na mwisho wa yote ni hayo yalompata Ashura. Wewe utafikiri janga hili ni lake tu, la hasha maana watoto watamkosa mama yao na hapo ndipo baba yao atataabika maana akioa mke mwingine kuna uwezekano akawa hawapendi. Hivyo kama si mitandao basi asingepata huo mchepuko na hata angepata asingechati nao kwa kuhofia kuwa mumewe atagundua.
 
mtu akiamua lake hashindwi na lolote ndugu yangu ndo yashatokea tena hayo kubwa kuwa waaminifu kwenye ndoa zenu tu
Kama mwanaume angalikuwa anafungua fungua simu ya huyo mama angelimfumania na wala asingechepuka. Hiyo ndiyo faida ya aidha kutoweka password katika simu au kuiwacha wazi. Naamini ukiona mwenzi anag'ang'ania simu yake jua ni michepuko na mwisho wa yote ni hayo yalompata Ashura. Wewe utafikiri janga hili ni lake tu, la hasha maana watoto watamkosa mama yao na hapo ndipo baba yao atataabika maana akioa mke mwingine kuna uwezekano akawa hawapendi. Hivyo kama si mitandao basi asingepata huo mchepuko na hata angepata asingechati nao kwa kuhofia kuwa mumewe atagundua.
 
dunia ni ile ile walimwengu ndo wabaya mkuu

Sijaamanisha kwamba dunia mbaya ndg yangu ila imebadilika sio ile dunia ya wazee way back huko now days haikupi guarantee hata kama umeoa partener wako ndo hata cheat
 
Sijaamanisha kwamba dunia mbaya ndg yangu ila imebadilika sio ile dunia ya wazee way back huko now days haikupi guarantee hata kama umeoa partener wako ndo hata cheat

ahahaha nimekuelewa dear
 
Huko Facebook mda wowote unamvua pichu mke wa mtu
 
Bado nayashangaa MAPENZI ya leo.....yaani mtu anaithamini simu kuliko hata tupu yake......
 
Back
Top Bottom