Kaab msafi
Member
- Jun 13, 2013
- 62
- 119
Wakuu nina wasalimu,
kwa Hakika majaribu ni mengi na mambo ambayo tunapitia ni mengi sana ambayo kimsingi ni vigumu sana kuweza kufanya vizuri kama huwezi kujipamba na vazi la Subira maana walisema zamani “Subira huvuta heri” Sasa leo tuangalie faida tano tu ,kwanini ni muhimu kuchagua upande wa kuwa mtu Mwenye Subira daima huku ukijitahidi kutatua changamoto zinazo kukabili bila kuvunja sheria wala kukanyaga haki za watu wengine?
1- Subira itakuepusha na Kufuru
Bwana Yesu Kristo alituonesha kwa mifano pale alipo jaribiwa masiku arobaini jangwani na shetani kwa vitu ambavyo leo tunavua utu wetu kuvikimbilia! Kuhusu NJAA Shetani akamwambia “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate” (Mathayo 4:3). Akajibu “Imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu” kuhusu kumjaribu Mungu hasa kwa vipawa na karama alizo nazo shetani akamwambia “Ukiwa wewe ni mwana wa Mungu jitupe chini” akamjibu “Tena imeandikwa usimjaribu BWANA, Mungu wako” na mwisho alimshinda na kumfukuza katika Matayo 4 alimwambia “Nenda zako shetani, kwa maana imeandikwa, Msujudie BWANA, Mungu wako, umwabudu yeye peke yake” Majaribu ya Ibrahimu kutakiwa kummchinja mwanaye kipenzi na Ayubu kuugua kwa miaka mingi na kufilisika lakini hawakumkufuru Mungu bali walisubiri.Na wewe kuwa na Subira utabarikiwa.
2-Subira itakusogeza kwenye mafanikio daima
Kwa Hakika walisema zamani pia “Mstahimilivu hula mbivu” Yusufu kutoka utumwani mpaka kuwa mfalme ni somo lenye manufaa makubwa kwetu, kuwa na subira kutakunyenyua juu zaidi ya hapo ulipo Sasa.
3-Subira itakuepusha na Madhara/balaa
Leo kuna watu lukuki wameingia kwenye matatizo kwasababu tu walikosa Subira katika utatuzi wa mambo yaliyo wasibu. Pengine walitoa adhabu isiyo stahiki kwa walio wakosea hata kusababisha wao wenyewe kuingia matatani.
4-Subira ni ufunguo wa ushindi
Kila unae Unaemuona amepiga hatua kuna uwezekano mkubwa kuwa alipitia majaribu ambayo leo wewe unapitia lakini walikuwa na Subira hivyo jitahidi pia na wewe kuwa mtu mwenye Subira.
5-Paradiso(Mbinguni) wataingia wale walio kuwa na Subira ulimwenguni.
Huko mbinguni pia ni kwa watu ambao walikuwa na Subira katika maisha yao ya ulimwenguni , Sala,Sadaka, kuwa tendea vema wazazi,kuwa nasihi wengine katika yale yenye manufaa,kutembelea wagonjwa na kuwapa huduma wazee,kusamehe ,kusema vema na majirani na mengine yanataka uwe na Subira katika kuyafanya. Utapata thawabu kwa Muumba na utaingia katika ufalme wa milele. Kuna jambo gani ambalo unajutia kwa kukosa Subira wakati Fulani katika maisha yako?
Niwatakie kila la Heri katika kuuanza mwaka mpya 2019 kwa kuwa mwenye Subira ziku zote.
Asanteni sana
Diwani Mstaafu
Beijing-China.
Sent from my iPhone using JamiiForums