Hapa mkuu kila mtu atasema lake kulingana na experience aliyo nayo. Kiufupi binafsi naweza sema uhai wa mapenzi ya namna hii unategemea sana stability ya mwanamke Ikiwa amekupenda kweli na tayari ya dunia yamesha mchosha basi unawezafanya naye familia ambayo badae itakaa sehemu moja.
Ili mtu huyo awe OFF na mambo ya kidunia ni lazima awe mtu mwenye kumjua MUNGU ktk Roho na kweli na si vinginevyo, yani kumjua Mungu ndo ulinzi wa penzi lenu, coz hutakuwa na haja ya kuhofia kupigiwa n.k.
Nasema hivyo kwasababu mtu huyo lazima atakuwa na hofu ya Mungu, pamoja na hilo ni lazima anajua nafasi ya mwanaume ktk maisha yake na kwamba hajakupata kwasababu ame kutafuta bali kwasababu Mungu amekuleta wewe ktk maisha yake...,hivyo si rahisi kukusaliti hata kama mpo mbali mbali maana anajua si wewe anaye kukosea bali Mungu aliye mpa wewe.
Finally, nimeongea kwa personal experience, sio takwimu maamuzi yote unayo wewe mkuu, fanya kitu na usisahau kutupatia mrejesho, ALL THE BEST 😎