Faida na hasara ya kumiliki gari ya kutembelea

Kwanza tuanze na faida.

Sio siri kumiliki gari kunaimarisha hadhi yako hapo kitaani kwako. Unaonekana wa tofauti mwenye hadhi ya juu. Si ajabu watu wakamwacha mjumbe au balozi wa mtaa wakaja kwako wakidai eti uwasaidie pesa au kusuluhisha migogoro yao.

Unaonekana una fedha na uwezo hata kama ni apeche alolo.

Unaonekana mwenye furaha na amani hata kama kiukweli kwa ndani una huzuni ya moyo na masikitiko.

Unaonekana mwenye kujiamini hata kama ukweli haiko ivo.

Hasara kubwa ya kuwa na gari ya kutembelea ni hii hapa.

Gari ya kutembelea haiingizi pesa yoyote badala yake inakutaka utumie pesa yako kwa ajili ya kununua mafuta, spea na kugharamia matengenezo mbalimbali.

Kifupi kama una pesa ya mawazo au pesa yako ni ya ngama ni heri uachane kabisa kufikiria kumiliki gari au vinginevo nunua gari ya biashara ikuizingie pesa.
Haha kuna siku mtasema na choo cha kisasa ni hasara.
Acha watu wamiliki magari ili wafunguke na wapate presha ya kutafuta pesa zaidi kukidhi mahitaji ya gari na familia
 
Umeongea point kubwa sana. Kadri unavyoongeza matumizi ndivyo upo uwezekano wa kupata hela zaidi. Pressure huenda pasipo na Pressure, ongeza matumizi pata msukumo wa kutafuta pesa zaidi. Ukijihurumia hata Honda la mtumba utakufa huna, hasa ukiendelea kuwasikiliza wale wa food,shelter and clothes
 
Ninaongea kwa uzoefu mkuu.

Ni kweli kumiliki gari ya kutembelea kuna hasara lkn.
Nimepata faidi nyingi kuliko hasara
Faida:
1. Unaaminika hata kupewa kazi kubwa
2. Urahisi wa kufanya kazi nyingi kwa siku moja.
3. Msukumo wa kutafuta pesa zaidi ili uendelee kubaki kwenye game
 
Uko sawa mkuu, wewe level za kuwaza hela ya mafuta umeshavuka. Kuna hawa waajiriwa wese wanaweka mwisho wa mwezi hela ikikata wanapaki gari
Hata wao wako sawa tu kuwa na gari, gari kuwa nayo, ukufae wakati muhibu, kuliko kuto kuwa nayo kabisa

Unaweza kuwa na gari, ila kulingana na mfuko wako ukawa unatumia wakati muhimu tu, ndiyo umuhimu wa gari uko hapo.
 
Nikionaga abiria wa mwendokasi wanavyopata changamoto ya usafiri ni bora kuendesha IST. Unapanda mwendokasi unanukia kapafymu kako kazuri ka elfu kumi lakini unashuka unajikuta unanukia kiti moto.
Tafuta hela ununue perfume nzuri za 50,000/-, unaendesha ist halafu unanunua perfume ya 10,000/-, bwashee njoo huku kwetu kwenye wapanda daladala
 
Kwanza tuanze na faida.

Sio siri kumiliki gari kunaimarisha hadhi yako hapo kitaani kwako. Unaonekana wa tofauti mwenye hadhi ya juu. Si ajabu watu wakamwacha mjumbe au balozi wa mtaa wakaja kwako wakidai eti uwasaidie pesa au kusuluhisha migogoro yao.

Unaonekana una fedha na uwezo hata kama ni apeche alolo.

Unaonekana mwenye furaha na amani hata kama kiukweli kwa ndani una huzuni ya moyo na masikitiko.

Unaonekana mwenye kujiamini hata kama ukweli haiko ivo.

Hasara kubwa ya kuwa na gari ya kutembelea ni hii hapa.

Gari ya kutembelea haiingizi pesa yoyote badala yake inakutaka utumie pesa yako kwa ajili ya kununua mafuta, spea na kugharamia matengenezo mbalimbali.

Kifupi kama una pesa ya mawazo au pesa yako ni ya ngama ni heri uachane kabisa kufikiria kumiliki gari au vinginevo nunua gari ya biashara ikuizingie pesa.
Acha hayo mawazo ya kimasikini, watu wanataka kuvimba kitaa hata kama hana hata mia mradi yuko na ka vitz powa tuu.
 
Tafuta hela ununue perfume nzuri za 50,000/-, unaendesha ist halafu unanunua perfume ya 10,000/-, bwashee njoo huku kwetu kwenye wapanda
Sisi wazanzibari tuna shamba letu la viungo na miti yenye harufu nzuri kwa hivyo pafyumu ni bei chee maana ni home made.
 
Tarehe kama hizi kwa watumishi wa umma familia inakula ugali maharage ili upate HeLa ya mafuta
 
Hata wao wako sawa tu kuwa na gari, gari kuwa nayo, ukufae wakati muhibu, kuliko kuto kuwa nayo kabisa

Unaweza kuwa na gari, ila kulingana na mfuko wako ukawa unatumia wakati muhimu tu, ndiyo umuhimu wa gari uko hapo.
Unakuwa na gari kama pambo,
Mshahara wako chini ya 4m gari la nini? Matokeo yake ni kufanya familia ile ugali mchicha
 
Back
Top Bottom