Sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma zinakataza mtumishi kuwa na madeni yaliyokithiri. Kopa kwa kiasi.
Hata hivyo sishauri ukope benki. Wana riba kubwa na makato ya yasiyo maana. Ukikopa shilingi alfu moja, utarejesha wastani wa alfu moja na mia kadhaa.
Bora ukope SACCOS. Kila mtumishi wa umma ni mwanachama AU mwanachama-mtarajiwa wa Hazina SACCOS. Jiunge nayo au SACCOS iliyo ofisini uliko.
Na ukopapo, fanyia jambo lidumulo au lenye matokeo makubwa sasa.