Faida na athari za mafuta ya "ubuyu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Faida na athari za mafuta ya "ubuyu"

Discussion in 'JF Doctor' started by Fadhili Paulo, Jul 8, 2014.

 1. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #1
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Maajabu ya juisi ya Ubuyu

  [​IMG]

  Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.
  Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

  1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
  2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng'ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
  3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
  4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
  5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng'enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
  6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
  7. Huongeza nuru ya macho
  8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
  9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
  10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

  Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.


  Ili upate faida za unga wa ubuyu zinazoelezwa hapa, lazima ule ubuyu halisi usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.


  Tazama video hapo chini jinsi ya kuandaa juisi hii ya ubuyu. Ikiwa utahitaji unga wa ubuyu uliotayari kama utakaouona kwenye video hii usisite kuwasiliana na mimi kwa simu namba 0769142586 au email hizi: info@fadhilipaulo.com au fadhilipaulo@gmail.com

  Makala hii ni kutoka fadhilipaulo.com

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. LUBEDE

  LUBEDE JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2014
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 2,697
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  tumeelewa mkuu..


  Sent from my iPhone using JamiiForums
   
 3. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #3
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana mkuu

   
 4. kigori wa kilwa

  kigori wa kilwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2014
  Joined: Nov 17, 2013
  Messages: 490
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nimetoka kunywa jana tu ila mtoto Wangu aipendi mpka nichanganye na Matunda mengine vip hapo itakuwa pouwa?
   
 5. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2014
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,198
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Ni bora sana!!!!
   
 6. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2014
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,423
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  kama haiongezi nguvu za kiume, kwangu mimi haina mantiki
   
 7. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #7
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Kama inaondoa sumu mwilini basi automatikali itaongeza nguvu ya mwili na ya kiume, umeelewa mkuu?

   
 8. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #8
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Siyo mbaya sana

   
 9. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2014
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,423
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  hapo nimekuelewa dokta
  ahsante sana!
   
 10. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2014
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,576
  Likes Received: 1,540
  Trophy Points: 280
  wenye ulemavu utawajua tu! kula vyakula vya asili uwo ulemavu wako wa nguvu za jinsia utakwisha
   
 11. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,600
  Likes Received: 9,671
  Trophy Points: 280
  Shukrani sana mkuu kwa darasa Murua

  Naona ubuyu na mlonge longe vinakaribiana sana kwa virutubisho
   
 12. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2014
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,198
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Vita!!!!!
   
 13. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2014
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 1,907
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Isije ikawa kama yale mafuta ya ubuyu ambayo watu waliyafakamia mwisho wa siku ikawa taharuki baada ya yule jamaa wa external kuamka toka usingizini
   
 14. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2014
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,423
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mkuu nani kasema ana ulemavu wa nguvu za kiume?
  Mi niko fiti kama daraja la salenda
   
 15. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #15
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Mafuta na juisi ni vitu viwili tofauti na hata hayo mafuta ni njama tu za watu wachache kuwaharibia kazi wajasiriamali

   
 16. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #16
  Jul 8, 2014
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,243
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 135
  Karibu sana mkuu

   
Loading...