Faida 20 za mazoezi ya kutembea

Apr 26, 2016
23
28
Kutembea ni njia salama na nzuri inayosaidia kuujenga na kuuimarisha moyo uwe na afya nzuri na usio katika hatari ya kushambuliwa na maradhi. Mazoezi au tabia ya kufanya mazoezi inayo faida kubwa zaidi kuliko matumizi ya dawa.


Faida 20 za mazoezi ya kutembea


1. Mazoezi husaidia kupunguza uzito, tembea saa mmoja kila siku

2. Ni mazoezi yanayoweza kufanywa na kila mtu

3. Ni mazoezi yasiyohitaji vifaa/ hayana gharama

4. Ndiyo njia rahisi kabisa kuufanya mwili kuwa mkakamavu

5. Hupunguza dalili za majonzi na wasiwasi

6. Ni mazoezi yenye matikeo ya taratibu

7. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kolesto/ lehemu

8. Hupunguza na kutibu shinikizo la damu

9. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na baadhi ya kansa

10. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na kisukari

11. Hukufanya ujisikie vizuri

12. Husaidia kuimarisha mifupa

13. Husaidia kupunguza uwezekano wa kupatwa na shambulio la moyo

14. Ni mazoezi uwezayo kuyafanya bila kukusababisha ajari au maumivu makubwa

15. Hupunguza mafadhaiko/ stress

16. Hupunguza uwezekano wa kapatwa na ugonjwa wa moyo

17. Ni mazoezi unayoweza kuyafanya bure bila kuulipia chochote

18. Husaidia katika mfumo wa upumuwaji

19. Husaidia kuongeza mzunguko wa damu

20. Husaidia kuimarisha mishipa

Kama afya yako siyo nzuri sana anza kutembea kidogo kidogo labda dakika 10 kwa siku huku ukiongeza dakika 5 kila siku hadi hapo utakapoweza kutembea saa mmoja mfululizo bila kupumzika. Ili kupunguza uzito, unene, utipwatipwa, mafuta yaliyozidi au kitambi, fanya zoezi la kutembea kwa miguu mwendo kasi kidogo muda wa mwezi mmoja mpaka miwili mfululizo.


Je, ni muda gani mzuri wa kufanya mazoezi ya kutembea?


Wengi wanapenda asubuhi sana na jioni lakini mimi napenda kufanya mazoezi ya kutembea mchana wakati wa jua kali saa sita, saa saba au saa nane, tena huwa natoa kabisa shati na kubaki tumbo wazi. Utanishangaa kwa nini na fanya hivi, jua lina muhimu sana kwa afya ya mwili na ngozi pia kama chanzo cha vitamini D, vitamini ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha mifupa na hivyo kuzuia ugonjwa wa mifupa(osteoporosis), kuzuia maumivu ya mishipa, kushusha shinikizo la damu, kudhibiti kisukari, kudhibiti kolesto na kudharka. Unapotembea mchana wa jua kali unaruhusu jua kutua juu yako mwili mzima.
 
Changamoto ni uhaba wa hizo sehemu za kufanya mazoezi ya kutembea.
 
Acha uongo wewe, jua la saa sita au saba halina faida zozote kiafya zaidi ya mionzi mikali inayoharibu ngozi, jua lenye faida ni kabla ya saa nne asubuhi
 
Acha uongo wewe, jua la saa sita au saba halina faida zozote kiafya zaidi ya mionzi mikali inayoharibu ngozi, jua lenye faida ni kabla ya saa nne asubuhi
Lile jua la mchana hata uvae sunscreen kilo tano mionzi lazima itatoboa tu
 
Acha uongo wewe, jua la saa sita au saba halina faida zozote kiafya zaidi ya mionzi mikali inayoharibu ngozi, jua lenye faida ni kabla ya saa nne asubuhi

Lile jua la mchana hata uvae sunscreen kilo tano mionzi lazima itatoboa tu

Huwezi fahamu mleta mada yupo wapi, maana viwango vya jua vinatofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine, kuna sehemu jua la mchana ni sawa na jua la asubuhi kwa dar es salaam.
 
Ni kweli mazoezi ya kutembea yana faida nyingi hasa kwa wanaokuwa ofisini muda mrefu na wastaafu lakini muda ufaao ni jioni na asubuhi kabla ya saa 4 mchana jua ni hatari kwa ngozi na macho.
 
Back
Top Bottom