Fahari ya macho ni hadaa katika mapenzi

Fahari ya macho ni hadaa katika mapenzi

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Wasalaam wakuu

Ni ukweli usiopingika macho hayashibi kutazama. Utaona leo na kesho yatatamani kuona tena.

Sasa linapokuja suala la mapenzi macho yamekuwa yakihada watu wengi na kuwasababishia vilio na huzuni.

Katika Dunia ya leo mpenzi mwenye muonekano mzuri wa umbo, au hali ya maisha yake kama kazi yake vimekuwa ndio vigezo vya ushawishi wa kimapenzi na uhusiano.

Tatizo linakuja unapoingia kwenye uhalisia, kumbe fahari ya macho kamwe haiwezi kukata kiu ya mapenzi.

Nguvu ya kutawala mapenzi ni tabia. Tabia uvumilia mazaifu ya mwenzio
Tabia uthamini utu wa mwenzio
Tabia huondoa ubinafsi
Tabia utafuta kumfurahisha mwenzio
Tabia umuonea huruma mwenzie
Tabia umliwaza mwenzie
Tabia umulinda mwenzie
Tabia iko tayari kulipa gharama ili kutunza mahusiano n.k

Mm bado naamini fahari ya macho
Shepu na kiuno
Sura na mwendo
Mapambano na nakshi za mahaba....

Yooooote ni fahari ya macho tu lakini Tabia ndio mpango mzima katika mapenzi.


Nipe mtazamo wako mkuu....
 
tabia utarekebisha ila mpiganaji me/ke katika mahusiano ni bora zaidi
 
Unaakili saaaana

Ungekuwa katika tume ya makenikia wala tusingepata icho tulicho pata
 
Wajuvi wa mambo wanasema fahari ya macho haifilisi duka...na mwanamke mzuri sio urembo ni tabia
 
Umemaliza mkuuu.
A good woman always deserve this " I will love you more than forever simply because even the eternity is not enough time for me to express my love for you "

Sasa kosea upate aliyemzuri lkn Tabia mbovu .. Hutoisha kusema " Unataka nikufanyie nini weee lkn ??? Daaaaahhh!!.
 
Ndo maana hata kuoa ni kazi miaka hii.
Watu wanaangalia hayo hasa kazi na kipato na si tabia na mapenzi ya dhati.
 
Tabia ni kitu muhimu kwenye mahusiano ila lazima nioe mwanamke ambae ata akiniudhi nikimuangalia usoni hapo hapo nasahau kero zote.
 
Kweli mkuu macho muda mwingine hudanganya...unaona mtu fulani ni mzuri kwa hiyo na tabia nayo atakuwa nayo nzuri kumbe ni tofauti kabisa
 
Umenena vyema naunga mkono hoja macho hayaliziki mpaka kifo
 
Umemaliza mkuuu.
A good woman always deserve this " I will love you more than forever simply because even the eternity is not enough time for me to express my love for you "

Sasa kosea upate aliyemzuri lkn Tabia mbovu .. Hutoisha kusema " Unataka nikufanyie nini weee lkn ??? Daaaaahhh!!.
Thanks
 
Muyaishi basi maneno yenu wapenda tabia, unaoa mtu ana tabia nzuri, sura ya mjomba, hana takko unabaki kumfungia ndani tu kama kochi hutoki nae, huku nje unakuja kusumbua wake za wenzio
 
Back
Top Bottom