Fahamu zaidi kuhusu korodani na Ovari

complex31

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
379
1,208
Koradani hupatikana katika mwili wa mwanaume katika sehem za uzazi. Korodani hutumika kuhifadhi na kuzalisha mbegu za kiume na kike X na Y.

Mwanaume pekee ndio anazalisha mbegu za kiume na kitaka mbegu mmoja inakua na Chromosome 23

Mbegu za kiume ndio Cell ndogo zaidi katika mwili wa mwanaume yeyote na katika tendo la ndoa hutoka zaidi ya mamillioni kwenda katika harakati za kuwahi kwenda kupevusha yai la kike ama Ovary.
Mbegu ya kiume ina kichwa na mkia na ili iweze kupevusha yai la mwanamke mbegu hii itahitajika iwe nzima na imekamilika yani kichwa na mkia iweze kuogelea katika uterus ya mwanamke kwa msaada wa semen.

Mbegu za mwanaume hukaa nje ya mwili (kwenye korodani) kwa sababu ili ziweze kuzalishwa huitaji baridi kiasi flani hivo joto la mwili 36.5°/ 37 sio sahihi kwa mbegu hizi kuzalishwa.

Hivyo unashauriwa kutokuvaa nguo za kubana kusudi mbegu hizi ziweze kuzalishwa kwa wingi zikiwa na afya njema.

Mwanaume ndio anabeba mbegu yenye jinsia ya mtoto wa kiume hivyo kukosa mtoto wa kiume sio tatizo la wanawake kama wengi wanavosema pia swala la kukosa mtoto inaweza kusababishwa na mbegu hizi kutokua kamili yani kichwa na mkia pia majimaji ama Semen yanayowezesha ziogelee mpaka zifike kurutubisha mbegu ya kike kutokua na maji maji ya kutosha. Mbegu za kiume huwezi kuzalishwa kwa kipindi cha maisha yote ya mwanaume.

===

Ovary
kwa upande wa mwanamke ni tofauti kabisa na mwanaume. Zenye ziko ndani ya mwili na huzalishwa moja kila mwezi tofauti na kwa mwanaume hua mamilioni kwa mamilioni.
Ovary ndio cell kubwa zaidi katika mwili wa mwanamke kule tuliona sperm ndio cell ndogo zaidi katika mwili wa mwanaume.

Ovary hua na chromosome 23 pia hivo inapokutana na sperm hufanya chromosome ziwe 46 na kufanya iwe DNA 🧬 iliokamilka hivo mtoto hua na vitu anavoridhi kuotoka kwa baba na mama. Ovary huitaji mbegu moja tu iliokamili ili iweze kupevushwa na kuanza kuumba mtoto ama Zygote tumboni kwa mama.

Ovary zenyewe zina mwisho wa kuzalishwa ambapo kipindi chake cha ukomo huitwa Menopause na ni kati ya miaka 40’s na 50’s mwili wa mwanamke huacha kutengeneza Ovary hivo kupelekea kutoweza kubeba mimba tena.

Matatizo kama Afya, Mawazo na magonjwa ya uzazi huweza pia kuchangia Menopause kwa mwanamke kuwahi zaidi.

Kipindi cha Menopausal mwanamke anabadalika mambo mengi hua mkali, kua na hasira sana kutokana na mabadiliko ya mwili.
 
Asante sana kwa somo zuri la baiolojia ila ungekuwa umetulia huku ukiandika ungetiririka vizuri. Mfano, umejichanganya kidogo kwenye seamen na sperms.

Pia kuhusu uzalishaji wa sperms na store yake. Naamini una ufaham mzuri sana wa hili somo hivyo next time tulia utajieleza vizuri.

Swali:
Je, ni nini mantiki ya hili somo lako kwetu?
 
Kwanini xx huwa zinachomoka (zina spidi) kushinda xy?
Kwanini korodani nyingi hata kwa wanyama huwa moja ndogo nyengine kubwa kidogo?

Ni kivipi mtoto akiwa tumboni mwa mama yake halafu mama akawa na maambukizi labda ya virusi vya ukimwi,kipi kinafanya mtoto asipate maambukizi akiwa bado tumboni kwa mama yake?
 
KENZY,
Maumbile ya korodani ndio yalivo moja kua kubwa kuliko nyingine, mbegu ya kiume Y huwai kufairiki mapema kuliko X ya kike.

Mama na mtoto tumboni wameunganishwa na Umbilical cord, huu ni kwaajili ya kupitisha chakula na hewa peke yake. Damu, Organs, Nervous System ya mtoto alie tumboni hujijenga baada ya kupata chakula cha kutosha kutoka kwa mama na hewa.

Pia mtoto anakua na nyumba yake (Placenta) inayomuwezesha kutokugusana na viungo ama nyama za mama kwa namba yeyote ile wakati wa ukuaji tumboni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom