Fahamu website hatarishi zilizopo kwenye dark web

Fahamu website hatarishi zilizopo kwenye dark web

Status
Not open for further replies.

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,221
Reaction score
2,425
Duniani kuna mambo mengi ya ajabu ambayo watu wengi hawayajui na ikitokea umeyajua unaweza sema hauko dunia hii!

Dark web ni ulimwengu wa tovuti ambao huwezi kupata au kuingia kwa kawaida kutafuta tu. Maana yake ni mfumo wa tovuti ambao hautumi www (world wide web). Ni mtandao wa siri ambao una mambo mengi ya ajabu yanayopatikana huko.

Ukitaka kuingia kwenye dark web basi kuna software au app ambayo inaitwa maalum ukitumia hiyo utaweza ku access dark web, kule akuna kutumia (.com) utakuta na (.onion).


Kwenye dark web kuna Facebook mitandao mingine ya kijamii iko kule, japo mambo mengi ya haramu yanapatikana kule kama uuzaji wa sliaha, madawa ya kulevya, mauaji, wizi, hacking nk.

Je, una zifahamu website hatarishi zilizopo kwenye dark web?

Human experiment
Hii ni tovuti ambayo kazi yao ni kufanya majaribio binadamu walio hai, yaani wanachukuliwa kutoka maeneo tofauti tofauti wanatekwa na kwenda kufanyiwa majaribio kama upasuaji, kumwagiwa tindikali, kutolewa mimba, kuzikwa ukiwa hai nk.

Kwenye hii tovuti kauli yao wanasema "Not all human are equal", some of them were born to superior to others ~ "Binadamu wote hatuko sawa, baadhi wamezaliwa kuwa Bora kuliko wengine."

cannibal forum
Hii ni tovuti inayohusika na ulaji wa nyama za binadamu tena live live, yaani kwenye hii tovuti wanaonyesha jinsi ya kula baadhi ya viungo vya mwanadamu tena vibichi au kwa kuvipika.

Last words
Hizi ni tovuti ambazo zinakuonyesha sauti pamoja na video za watu tofauti tofauti wakisema maneno yao ya mwisho kabla hawajafa, hivyo utasikia sauti za watu wakitamka maneno ya mwisho mwisho.

The human product
Katika dark web, bidhaa kadhaa zinauzwa zilizotengenezwa na wanadamu kama vile chakula, pochi za mikanda na na mavazi. Tovuti hii kauli yao wanasema "Usivae Manyoya" ~ Do not wear Fur.

Kazi ya hii website ni kuuza bidhaa zinatokana na ngozi ya binadamu kuanzia viatu, nguo, mikanda, pochi, ni hatari.

Hitman service
Hii ni tovuti ambayo ina kundi la wauaji na kazi yao ni kuua watu ambao unawapa oda wanakufanyia kazi, wao wanafanya kazi popote japo wapo USA, Canada na European wale wenye ma Ex .

Ila sheria yao wanasema hawawezi kuua mtoto mdogo mwenye umri kuanzia miaka 16 kushuka chini pamoja na wanasiasa wakubwa.

Teknolojia ni yetu sote
 
Kuna vitu vya ajabu kule wengine wanajadili vitu vya hovyo nakuweka picha za watoto wako utupu!,utapeli ni mwingi na ukitapeliwa huna pa kushitaki..😂

Baada ya kuona wanarusha picha za watoto nikaanza kuwatukana kwa kiswahili,niliona kwa kiingilishi wanaweza nijua wakanihack waanze kuweka picha zangu!.. unapowatamanisha watu kwenda huko wape na tahadhari.
 
TAHADHARI: Mashirika mengi ya ujasusi yapo huko, unaweza ukawa umeingia kujaribu ukajichanganya na kuangukia kwenye 18 ukaanza kutafutwa kama mhalifu, kumbe hujui lolote kuhusu mambo ya huko.
Baada ya komenti hii nimeghairi..
Ahsante mkuu na ubarikiwe sanaaaa
Na hiyo Toe browser nimeuninstall ngoja niendelee humu humubinsta na fb kwa vilaza.
Madini nitayapata JF toshaaa
 
Salama wakuu,

Unajua mtaani kumekua na story nyingi sana kuhusu Dark Web, story nyingine zinaweza kuwa ni za kweli ama uongo, lakini tulio wengi hatujui kama tunadanganywa ama lah, na sababu kubwa ni kuwa na uoga wa kile tulichoaminishwa.

Kwa wale wazoefu wa kutumia dark web, kama hamtojali mngekuja kutujuza ni nini kipo huko, na je vile vitu tulivyo aminishwa ni kweli?

Kama Dark web ni sehemu hatari ambayo ukingia kama sio mtaalamu wa IT huwezi pata chochote wala kuona lolote, na pia kama utafanikiwa kuingia, utakutana na vitu vya kutisha kama video za ukatili kwa watoto, mauaji ya watu wakikatwa viuongo wakiwa wazima na viuongo vyao kuuzwa kwa watu wanaofanya maonyesho ya kula nyama za watu, ama wateja wa kawaida (hata wewe unaweza kununua.

Je, matukio hayo ni kweli, na mengine wachangiaje waulize wazoefu mtujuze kwenye Dark Web kuna mambo gani hasa.

Karibuni kwa michango.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom