Fahamu tatizo la Usonji (Autism)

Fahamu tatizo la Usonji (Autism)

conductor

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
838
Reaction score
714
(Copied and pasted)

Usonji (pia tawahudi, kwa Kiingereza autism) ni tatizo la kinafsi na la kihisia linalowatokea watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wengine.

Wenye tatizo hilo hawaonekani watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana na watu wengine katika mambo kadhaa. Pia, hawako vizuri katika mawasiliano. Muda mwingine huwa hawawezi kuongea au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine (ambaye hana tatizo la usonji) hafikirii kina umuhimu.

Mtu mwenye tatizo hilo anaelekea mara nyingi kurudiarudia matendo kadhaa, na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoeleweka kama tatizo na wengine.

Usonji ni ugonjwa wa ukuaji wa neva unaojumuisha kudhoofishwa kwa uwezo wa mwingiliano wa kijamii na mawasiliano, na kwa tabia finyu na ya kujirudiarudia. Dalili hizo huanza kabla ya mtoto kutimiza miaka mitatu.[1] Ugonjwa wa akili kwa watoto huathiri uchakataji wa habari katika ubongo kwa kubadili jinsi seli za neva na sinepsi zake zinavyounganika na kujipanga; jinsi gani hilo hutokea haileleweki vizuri.[2]

Ni moja ya matatizo matatu yanayotambulika katika wigo wa ugonjwa wa akili wa watoto (ASDs), nyingine mbili zikiwa maradhi ya Aspaja, ambayo haicheleweshi [3] ukuaji wa kiutambuzi na lugha, na Tatizo la Ukuaji Ulioenea-Usiofafanulika Vinginevyo (PDD-NOS), ambao hutambuliwa kikamilifu wakati vigezo vyote vya kawaida au Aspaja havijatimizwa.[3][4]

Usonji una msingi kamili katika jeni, ingawa mpangilio wa jeni za ugonjwa wa akili kwa watoto ni changamano na si bayana kama ASD inaelezeka zaidi kwa mabadiliko makuu ya jeni yasiyo ya kawaida, au kwa mchanganyiko usio wa kawaida wa aina tofauti za jeni ya kawaida.[5] Katika matukio ya nadra, usonji unahusishwa sana na visababishi vya kasoro za kuzaliwa.[6] Ubishi unakumba mapendekezo mengine ya visababishi vya kimazingira, kama vile metali nzito, viuawadudu au chanjo za utotoni;[7] nadharia tete ya chanjo haiwezekani kibiolojia na inakosa ushahidi yakinifu wa kisayansi.

Uenezi wa usonji ni karibu 1-2 kati ya watu 1,000, wakati uenezi wa ASD ni takriban matukio 6 kwa 1,000, huku idadi ya wanaume ikiwa mara nne kuliko ya wanawake. Idadi ya walioaguliwa kuwa na usonji umeongezeka kwa kasi tangu miaka ya 1980, kwa kiwango kutokana na mabadiliko katika jinsi ya uaguaji, swali la kama maambukizi shadidi yameongezeka halijafumbuliwa.[8]

Wazazi kwa kawaida hugundua dalili katika miaka miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto wao.[9] Dalili hizo kwa kawaida huendelea hatua kwa hatua, lakini baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa akili hukua kwa kawaida kijumla kabla ya ukuaji kubadilika.[10] Ingawa mwingilio wa mapema wa kitabia au wa kitambuzi unaweza kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa akili kujihimili, kupata ujuzi wa kijamii, na mawasiliano, hakuna tiba inayojulikana.[9] Si watoto wengi wenye usonji huishi kwa kujitegemea wanapofikia utu uzima, ingawa baadhi huwa wafanisi.[11] Kumeibuka desturi ya usonji, huku watu wengine wakitafuta matibabu na wengine wakiamini lazima usonji ikubalike kuwa utofauti, si ugonjwa.[12]

Dalili

Kukaa peke yake

Mtoto wa kawaida huwaangalia watu wakizungumza, hutazama wengine usoni, hutabasamu, na huwa na shauku na watu wengine. Watoto wenye usonji, wanaweza kupenda vitu kuliko sura au watu wengine. Wanaweza wakatazama usoni kwa sekunde tu, halafu mara moja wakageuka. Wanaweza wasitabasamu, au wanaweza wakatabasamu kwa kitu kile walichokipenda.

Watoto wenye tatizo hilo huwa na kawaida ya kukaa wenyewe tu, bila uwepo wa wengine. Wanaweza wasiwe na shauku ya kutaka urafiki na mtu yeyote. Pia, wanaweza wasiwe wanafanya mambo ya kawaida kama kukumbatiana na alama nyingine za upendo kwa wazazi wao. Hii haimaanishi hawawapendi wazazi wao, ni kwamba hawajui namna ya kuonyesha hivyo vitu.

Wanaweza wasione hisia za watu wengine; kwa mfano, wanaweza wasione tofauti kubwa sana kati ya mzazi kuwa na furaha ama kuwa na huzuni. Wanaweza wakacheka na kulia mara zisizoeleweka.

Kutozungumza
Mtoto mwenye usonji anaweza asithubutu kuongea, maana, au kujaribu kuelewa maongezi kati ya mwenzie mwenye umri sawa. Baadhi yao huwa hawaongei kabisa. Wengi wao hawawezi kuongea vizuri na watu wengine.

Kufanya vitu tena na tena
Baadhi ya wenye usonji hutumia muda mwingi kufanya vitu vya aina moja mara nyingi zaidi na zaidi, au kuwa na shauku na vitu ambavyo si vya kawaida; baadhi yao wanaweza kutumia muda mwingi kujizungushia mkono, kutembea na wanaserere wao, au kupanga vitu kwa mpangilio mmoja. Watu wenye tatizo la usonji wanaweza wakatumia muda mrefu kupanga visanamu au vyumbavyumba vyao kwa mstari mmoja na wanaweza kusikia jazba mtu akivivuruga katika eneo lake.

Baadhi yao hawataki badiliko lolote lile, na wanaweza wakafanya mambo yaleyale kila siku bila kubadilisha — kama vile wanapokula, wanavaa, wanapiga mswaki, au pale wanapokwenda shule — huwa na huzuni kama kuna badiliko lolote katika vitu hivyo. Pia, wanaweza wakawa na shauku na vitu vya ajabu na kutumia muda wao mwingi kujifunza vitu hivyo.

Ugunduzi na jina
Autism lilipewa jina hilo la Kiingereza kwa mara ya kwanza mnamo 1943. Leo Kanner alifanya utafiti huu kwa watoto wapatao 11 akagundua vitu ambavyo si vya kawaida kuhusu wao. Aliita early infantile autism.

Muda huohuo, daktari mwingine, Hans Asperger, akafanya utafiti mwingine karibu sawa. Alichokigundua kinaitwa sasa Asperger syndrome, wakati alichokigundua Leo Kanner kinaitwa autistic disorder, childhood autism, infantile autism, au autism tu.

Sifa bainifu

Usonji ni maradhi ya ukuaji wa neva yaliyo na ugeugeu mwingi sana[13]ambayo huonekana kwanza wakati wa ukembe au utoto, na kwa jumla hufuata mkondo fulani bila kupungua.[14] Dalili za kuonekana huanza polepole baada ya umri wa miezi sita, huwa dhahiri katika umri wa miaka miwili au mitatu,[15] na aghalabu huendelea hadi utu uzima, ingawa mara nyingi katika kiwango kilichopungua.[16]

Haitambuliki kwa dalili moja tu, bali kwa sifa bainifu tatu: udhaifu katika mahusiano ya kijamii; udhaifu katika mawasiliano, hamu finyu ya mambo na tabia ya kujirudiarudia. Vipengele vingine, kama vile ulaji usio wa kawaida, vinatokea pia mara nyingi lakini si muhimu kwa ajili ya uaguzi.[17] Dalili za mtu mwenye usonji hutokea katika jamii kijumla na huonekana hajihusishi sana, bila utenganisho wa sifa za kawaida na za kiambukizi.[18]

Ukuaji kijamii
Mapungufu ya kijamii hutofautisha usonji na maradhi mengine yaliyo katika wigo unaofanana (ASD) kutoka matatizo mengine ya ukuaji.[16] Watu walio na usonji huwa na mapungufu ya kijamii na mara nyingi hukosa uwezo wa kufikiri haraka kuhusu wengine, jambo ambalo watu wengi huchukulia kwa mzaha. Temple Grandin, mgonjwa wa akili mtambulika, alieleza hali yake ya kutoweza kuelewa mawasiliano ya kijamii ya watu wasio na matatizo ya neva, au watu wenye ukuaji wa kawaida wa mfumo wa neva, kama unaomwacha kujihisi "kama mwanaanthropolojia juu ya Mirihi".[19]

Ukuaji wa kijamii usio wa kawaida huanza kudhihirika mapema utotoni. Watoto wachanga wenye usonji huonyesha makini ndogo kwa michocheo ya kijamii, ni nadra kutabasamu na kuwaangalia wengine, aidha ni nadra kuitikia jina lao wenyewe. Watoto wachanga wenye usonji huenda kinyume kabisa na kanuni za kijamii, kwa mfano, hawaangalii sana watu machoni wala kujibu wengine katika mazungumzo, na upo uwezekano mkubwa wa kuwasiliana kwa kuchezea mkono wa mwingine.[20] Watoto wa umri wa kati ya miaka mitatu na mitano walio na ugonjwa wa akili huenda wasionyeshe uelewa wa masuala ya jamii, huenda wasijue kutangamana moja kwa moja, huiga na kuitikia hisia, hujieleza bila kuzungumza, na hawachangii inapofika zamu yao katika mazungumzo. Hata hivyo, huonyesha mapenzi kwa walezi wao.[21] Watoto wengi wenye ugonjwa wa akili huonyesha kiasi kidogo cha mapenzi wakilinganishwa na watoto wasio na ugonjwa, ingawa tofauti hii hutoweka kwa watoto walio na ukuaji mkuu wa akili au walio na athari ndogo ya ASD.[22] Watoto wakubwa na watu wazima walio na ASD hufanya vibaya katika mitihani ya utambuzi wa nyuso na hisia.[23]

Watoto walio na kiwango kikubwa cha athari ya usonji hukabiliwa na upweke wa kiwango kikubwa na cha mara kwa mara wakilinganishwa na wale wa rika lao wasio na ugonjwa wa akili, licha ya imani ya kawaida kwamba watoto walio na usonji hupendelea kuwa peke yao. Kuanzisha na kudumisha urafiki mara nyingi huwa vigumu kwa walio na usonji. Kwao, ubora wa urafiki, wala si idadi ya marafiki, huchangia kiwango cha upweke wanachohisi. Urafiki amilifu, kama vile unaojumuisha mwaliko kwa karamu, huweza kuathiri ubora wa maisha kwa undani zaidi.[24]

Kuna taarifa nyingi za matukio ya kweli, lakini chunguzi chache za kijarabati, kuhusu uchokozi na vurugu unaotekelezwa na watu walio na ADS. Data chache zilizopo zinaonyesha kwamba, kwa watoto wenye akili taahira, usonji unahusishwa na uchokozi, uharibifu wa mali, na hamaki. Utafiti mmoja wa mwaka 2007 uliowahoji wazazi wa watoto 67 walio na ASD uliarifu kuwa thuluthi mbili za watoto hao waliwahi kuwa na hamaki kali, takriban thuluthi moja wakiwa na historia ya uchokozi, huku wakiwa na uwezekano mkubwa wa hamaki kuliko watoto wasio na ugonjwa wa akili mbali na matatizo ya lugha.[25] Utafiti uliofanyika Uswidi mwaka 2008 uligundua kwamba, kwa watu wenye umri wa miaka 15 au zaidi walioachiliwa kutoka hospitalini baada ya kutambuliwa kuwa na ASD, waliotekeleza uhalifu kwa nguvu pia walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na matatizo mengine ya kisaikolojia kama vile wendawazimu.[26]

Mawasiliano
Takribani thuluthi au nusu ya watu walio na usonji hukosa umilisi wa mazungumzo wa kutosha kukidhi mahitaji yao ya mawasiliano ya kila siku.[27] Tofauti katika mawasiliano inaweza kuwepo katika mwaka wa kwanza wa uhai, na inaweza kujumuisha kuchelewa kuanza kubwabwaja, ishara zisizo za kawaida, mwitikio mpungufu, na mifumo ya matamshi isiyooana na ya mlezi. Katika mwaka wa pili na wa tatu, watoto walio na ugonjwa wa akili hubwabwaja mara kidogo na maneno yao huwa machache iliyo uchache wa konsonanti, maneno, na mchanganyiko wa maneno, ishara zao mara nyingi haziambatani na maneno. Watoto walio na usonji ni nadra kuomba kitu au kujieleza, kuna uwezekano wa wao kurudia tu maneno ya watu wengine (ekolalia)[28][29] au kugeuza kinyume viwakilishi.[30] Mwongozo shirikishi wa makini unaonekana kuwa muhimu katika mazungumzo amilifu, na upungufu katika mwongozo shirikishi wa makini unaonekana kuwatofautisha watoto wachanga walio na ASD:[3] kwa mfano, wanaweza kuangalia mkono unaoashiria badala ya kifaa kinachoashiriwa,[20][29] na pia hushindwa mara nyingi kuashiria vitu ili kutoa maoni au kujieleza.[3] Watoto walio na ugonjwa wa akili wanaweza kuwa na ugumu katika michezo ya ubunifu na kufanya ishara kuwa lugha.[28][29]

Katika jozi la chunguzi, watoto walio na umri wa miaka 8-15 na wenye ugonjwa wa akili wa kiwango cha juu walifanya vizuri kuliko waliokuwa wakilinganishwa nao katika mtihani wa msamiati na tahajia. Jozi la watu wazima lilifanya vizuri zaidi. Makundi yote ya walio na ugonjwa wa akili yalifanya vibaya zaidi kuliko waliokuwa wakilinganishwa nao katika mitihani changamano ya lugha kama vile, jazanda, ufahamu na uchanganuzi. Kwa kuwa mara nyingi watu hutathminiwa kutokana na uelewa wao wa kimsingi wa lugha, chunguzi hizi zinaonyesha kwamba watu wanaozungumza na watu wenye ugonjwa wa akili wanaweza kukadiria juu zaidi kuhusu uelewa wa wasikilizaji wao.[31]

Tabia radidi

Watu walio na ugonjwa wa akili hudhihirisha aina mbalimbali ya tabia radidi au tabia finyu, ambayo Mizani ya Tabia Radidi-Iliyorekebishwa (RBS-R)[32] inainisha kama ifuatavyo.

Mvulana mdogo aliye na usonji, na msururu sahihi wa vijidude aliotengeneza.

Uradidi ni msogezo wa kujirudiarudia, kama vile kupigapiga mkono, kufanya kelele, kutikisa kichwa, au kutikisa mwili.Tabia ya kulazimisha inanuiwa na huonekana kufuata kanuni, kama vile kupanga vitu katika vitita au mistari.Uhafidhina ni kukataa kukubali mabadiliko, kwa mfano, kusisitiza kwamba samani isisongozwa au kukataa kukatizwa.Uhalisia unahusisha tabia isiyobadili mpangilio wa shughuli za kila siku, kama vile kutobadili chakula au mavazi. Hii huhusishwa kwa karibu na uhafidhina na wathibitishaji wa kujitegemea wamependekeza kuchanganya vipengele hivi viwili.[32]Tabia vikwazo ni finyu katika lengo, nia, au kitendo, kama vile mshughuliko na kipindi kimoja cha runinga, mwanasesere, au mchezo.Kujiumiza hujumuisha vitendo vya kudhuru au vinavyoweza kumdhuru mtu, kama vile kuchokora macho, kujichokoa ngozi, kuuma mkono, na kugonga kichwa.[3] Utafiti mmoja wa mwaka 2007 uliarifu kwamba majeraha ya kujiumiza wakati fulani yaliathiri 30% ya watoto walio na ASD.[25]

Hakuna tabia moja radidi au maumivu ya kujisabishia yanayoonekana kuwa mahsusi kwa walio na ugonjwa wa akili, lakini ni ugonjwa wa akili unaoonekana kuwa na mfumo wa ongezeko na ushadidi wa matukio ya tabia hizi.[33]

Dalili nyinginezo
Walio na ugonjwa wa akili wanaweza kuwa na dalili zisizoonekana kwa uaguzi, lakini zinaweza kumwathiri mtu binafsi au familia.[17] Inakadiriwa kuwa 0.5% hadi 10% za watu walio na ASD hudhihirisha vipaji visivyo vya kawaida, kwa mfano ujuzi wa kukumbuka maswali madogomadogo pamoja na vipaji vya nadra sana na kuwa watumishi wa ajabu.[34] Watu wengi walio na ASD hudhihirisha ujuzi mkuu katika mtazamo na makini, wakilinganishwa na watu wa kawaida.[35]Ulemavu katika hisia hupatikana miongoni mwa zaidi ya 90% ya watu walio na usonji, na hudhaniwa na baadhi ya watu kuwa sifa msingi,[36] ingawa hakuna ushahidi mzuri kwamba dalili za kihisia hutofautisha usonji na maradhi mengine ya ukuaji.[37] Tofauti ni kubwa katika mwitikio-chini (kwa mfano, kutembea kuelekea jambo) kuliko mwitikio-juu (kwa mfano, kuitikia sauti kubwa kutokana na taharuki) au kwa kutafuta mhemko (kwa mfano, misogezo yenye urari).[38] Takribani 60-80% za watu walio na ugonjwa wa akili huwa na matatizo katika mwendo ikiwa ni pamoja na misuli iliyodhoofika, mpangilio hafifu wa kusogeza viungo, na kutembea kwa viganja vya miguu, [36] upungufu katika taratibu za kusogeza viungo ni chache kwa walio na ASD na ni kubwa miongoni mwa walio na usonji uliokithiri.[39]

Tabia isiyo ya kawaida katika ulaji hutokea katika robo tatu za watoto walio na ASD, kiasi kwamba awali ilikuwa moja ya viashiria vya uaguzi. Ubaguaji ndilo la tatizo la kawaida zaidi, ingawa desturi za ulaji na kukataa kula pia hutokea;[25] hii haionekani kusababisha utapiamlo. Ingawa baadhi ya watoto walio na usonji pia huwa na dalili za ugonjwa wa tumbo na utumbo (GI), kuna ukosefu wa data madhubuti zilizochapishwa kuunga mkono nadharia kwamba watoto walio na ugonjwa wa akili wana tofauti au dalili zaidi za GI kuliko kawaida,[40] chunguzi zimeripoti matokeo yanayokinzana, na uhusiano kati ya GI na matatizo ya ASD si wazi.[41]

Wazazi wa watoto wenye ASD huwa na viwango vya juu vya msongo.[42] Ndugu wa watoto walio na ASD wameripoti kupokea pongezi zaidi na migogoro michache kutoka kwa ndugu walioathirika kuliko ndugu wa watoto ambao hawajaathirika au wa wale walio na akili taahira, ndugu za watu walio na ASD wana hatari kubwa zaidi ya kutoendelea vizuri na kuwa uhusiano mbaya baina ya ndugu kama watu wazima.[43]

image_8d8a2f43-dc7a-45c0-b92f-6360ec4463ed20210101_210819.jpeg
 
Back
Top Bottom