tarakilishi ni nini?
La muhimu hapa kwa mawazo yangu ni kuwa kitu tumekitumia kwa miaka nenda rudi kwa jina fulani. Wataalamu wanakuja na majina ya ajabuajabu. Ah nimekumbuka, calcultor inaitwa kikokotozi, ovyo kabisa. Tungesema kalikuleta. Asante.Congo nakubaliana na wewe ila nafikiri computer ingeitwa kompyuta badala ya komputa!
La muhimu hapa kwa mawazo yangu ni kuwa kitu tumekitumia kwa miaka nenda rudi kwa jina fulani. Wataalamu wanakuja na majina ya ajabuajabu. Ah nimekumbuka, calcultor inaitwa kikokotozi, ovyo kabisa. Tungesema kalikuleta. Asante.
Ninajaribu kukuelewa: unaona kama ni kupoteza wakati na rasilimali kutafuta tafsiri ya 'Kiswahili' ya maneno hasa yanayohusiana na sayansi na teknolojia. Unadhani hakuna haja ya kuwa na istilahi mpya, unataka tuendelee na 'utohozi'.
Sioni shida sana ingawa sikubaliani na wewe kwenye baadhi ya maeneo.
Lakini, huu u--'hovyo' unaouona umeutoa wapi?
ni sawa kabisaMh! nakumbuka kuna mtu alishawahi kusema, je TARAKILISHI na NGAMIZI ni sawa? maana mimi naifahamu kuwa ni Tarakilishi
point tupuNawalaumu sana hao wanatoa tafsiri za maneno na vitu mbalimbali. Tukiangalia kwa uzuri lugha ni muingiliano wa lugha mbalimbali. Ndio maana tuna maneno bora kama shati, meza, chai, pesa, hela, gari n.k. Hivi kwa nini fan iitwe pangaboi badala ya feni tulivyozoea? Computer ingekuwa komputa, television ingekuwa televisheni, fax mashine ingekuwa faksi n.k. Hakuna ubaya kuiga. Lugha zote zinaiga.
tarakilishi ni nini?
Napenda kujulisha wanaoshirki sehemu ya Lugha kwamba mimi peke yangu nimetunga Kamusi Fupi ya Istilahi ya Ngamizi/Tarakirishi. Kwa wakati huu sokoni hakuna kitabu cha namna hii kinachopatikana.Waswahili wengi hufikiri kwamba hakuna maana halisi ya computer na badala yake wanatohoa neno hilohilo nakuandika "Kompyuta". Hivyo ni makosa maana halisi ya Computer ni neno "NGAMIZI" na kwa laptop computer huitwa "NGAMIZI PAKATWA" Source: Ulimwengu wa kiswahili TBC1, Nawasilisha.