Tatizo mara nyingi hizi hoja hujengwa upande mmoja. Juzi juzi kulikuwa na sifa za mwanaume anayefaa kuwa mume. Kama hizo ndio sifa za mwanamke, je huyo mwanaume anayetaka sifa hizo, yeye binafsi awe na sifa zipi? Au iandikwe wanandoa watarajiwa wawe na sifa zipi? Kibaya zaidi hata hizo zilizotajwa kila mtu ana tafsiri yake. Mfano mdogo - mwanamke mvumilivu ni yupi? Anayevumilia shida na raha katika ndoa, anayevumilia kipodo, anayevumilia michepuko ya mumewe?
Nakufanyia tathimini wewe kama una sifa hizo hapo juu unakuwa baby wangu wewe Heaven on Earth!
Kupata sifa zote hizo tano kwa ulimwengu huu tulionao sijui, niseme bahati labda
Mzeee umebugi sifa ulizosema za mwanamke kuolewa sizo kabisa hebu cheki hizi halafu nambie
1 awe mzuri kioo cha macho yako
Akiwa na sifa hio ya uzuri utatulia hutohangaika na wapita njia kwani na utaepuka zambi ya zina kwa 90%
2 awe na nasabu nzuri
Mwanamke akitokea katika familia nzuri ilio na malezi hakupi tabu kwani atajua wajibu na majukumu yake kukutunza na kukuthamini
3 awe na mali
Mwanamke akiwa na mali inasaidia sana kwani munapiga maendeleo fasta na atakua ni mtuzaji na mtumiaji mzuri wa kile mungu anachokujaalie hatokua na fujo katika matumizi
4 awe na dini
Mwanamke akiwa na dini atakulelea watoto wako katika misingi mizuri ya dini atakuhimiza ili mupatr ufaulme wa mbinguni pia yakikukuta majanga atakuvumilia kwani anajua ni maandiko ya mungu
Hebu niambie unazionaje hizi?
Sent from my HTC Desire S using JamiiForums mobile app
Tatizo mara nyingi hizi hoja hujengwa upande mmoja. Juzi juzi kulikuwa na sifa za mwanaume anayefaa kuwa mume. Kama hizo ndio sifa za mwanamke, je huyo mwanaume anayetaka sifa hizo, yeye binafsi awe na sifa zipi? Au iandikwe wanandoa watarajiwa wawe na sifa zipi? Kibaya zaidi hata hizo zilizotajwa kila mtu ana tafsiri yake. Mfano mdogo - mwanamke mvumilivu ni yupi? Anayevumilia shida na raha katika ndoa, anayevumilia kipodo, anayevumilia michepuko ya mumewe?
Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya shida.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.Umeongea vizuri sana ndugu....neno UVUMILIVU mimi huwa silielewi.....tena huwa sikurupuki kulijibu km nikiulizwa iwapo mimi ni mvumilivu
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtamkia kwamba anataka kumuoa.
1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
2. MWENYE TABIA NZURI
3. MWENYE UCHU NA MAENDELEO
4. ASIYEPENDA MAKUU
5. MVUMILIVU
Mwanamke ukiwa na sifa hizo tano hapo juu unauwakika wa 100% kuolewa.
Nawasilisha!
Sifa za kuoa ua kuolewa ziko subjective sana....it will depend frm one person to another
Huwezi uka generalize ktk kitu kama hicho
Namtafakari sana huyu anayeitwa heaven on earth