Fahamu kwa uchache kuhusu nchi ndogo ya Nauru

MalcolM XII

JF-Expert Member
Mar 19, 2019
5,236
14,206
Kisukari hasa type II huwa kinawapata sana watu wanene ikikadiriwa kufika hadi asilimia 40.

Nauru ni nchi na pia ni kisiwa kidogo kinachopatikana kwenye bahari ya Pacific juu kidogo ya Australia.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO, Nauru ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wanene zaidi kwenye jamii zao, ikiwa na jumla ya watu takribani 10,000 nchi nzima huku asilimia 94.5 ya watu wake wakiwa ni wanene (obese) na wazito kupita kiasi (overweight).

Inakadiriwa kuwa watu wa Nauru wana wastani wa uzito wa kuanzia kilo 100 na kuendelea. Wastani wa BMI ukiwa kuanzia 34 hadi 35.

Sababu ikielezwa kuwa ni urithi unaopita kutoka kizazi hadi kizazi.

IMG_0746.jpg

Vijana wa Nauru

IMG_0747.jpg

Mgonjwa wa kisukari huko Nauru

IMG_0752.jpg

Mkazi wa Nauru

IMG_0751.jpg

Wanawake wa Nauru

IMG_0753.jpg

Rais wa Nauru

Vile vile nchi ya Nauru ni moja kati ya nchi ambazo hazina mito inayotiririsha maji, huku ikiwa na jumla ya kilomita 30 tu za barabara zote.

Pia Nauru ni moja kati ya nchi 16 duniani ambazo hazina jeshi la nchi. Wao wanategemea/wanahakikishiwa ulinzi kutoka katika nchi ya Australia.

Hakuna hata kituo cha polisi!

Kama na wewe mwanajamvi ukiambiwa ukaanze maisha huko utaenda?
 
Hawa jamaa ni malofa wa kutupwa. Walikuwa na madini ya phosphate nadhani walichima yote kama Barrick wanavyofanya kanda ya ziwa. Hakuna cha maana walichowekeza. Madini yameisha wameachiwa mashimo. Kwa sasa wanaishi kwa ruzuku toka wasamaria wema wa Australia na nchi nyingine.

Hakuna maisha Nauru.

Kabisa! Kwa sasa watu wake ni masikini sana huku wakiathiriwa sana na aina ya vyakula wanavyotumia plus lifestyle ndio inakuwa balaa zaidi.
 
Hawa jamaa ni malofa wa kutupwa. Walikuwa na madini ya phosphate walichimba yote kama Barrick wanavyofanya kanda ya ziwa. Hakuna cha maana walichowekeza. Madini yameisha wameachiwa mashimo. Kwa sasa wanaishi kwa ruzuku toka wasamaria wema wa Australia na nchi nyingine.

Hakuna maisha Nauru.

Ruzuku zinawanenepesha.
 
Sijawahi kuisikia hii Nchi
Ni nchi ndogo sana hata ukiangalia kwenye ID ya mwanajamvi Ritz the zombie boy anasema ametoka Nauru. Nilishangaa sana 2013 nilipoangalia profile yake.

Wenyeji wa Nauru ni Polynesians. Nilishaletaga Uzi kuwahusu kwenye ile ID yangu nyingine ya iliyopigwa life ban. Kuhusu The pasific islanders.

Nchi zingine za pacific ambao Wenyeji wao ni Polynesians ni Kiribati, Tonga, Hawaii (Marekani) , French Polynesians (Tahiti), Tuvalu, Vanuatu, Samoa, American Samoa na Wenyeji wa asili New Zealand Maori .

Pia cha kushangaza hawa Polynesians wako hadi Canada na Chile (Easter Island)

Cha kushangaza zaidi wa Madagascar ni Polynesians.

Australia imeamua kuwalipa hela nyingi Nauru kwa kuwapeleka asylum seekers.

Fijian papuan, Vanuatu, Marshall Island, New caledoneans na watu wa cook islands hao ni astronasians.
 
Ni nchi ndogo sana hata ukiangalia kwenye ID ya mwanajamvi Ritz the zombie boy anasema ametoka Nauru. Nilishangaa sana 2013 nilipoangalia profile yake.

Wenyeji wa Nauru ni Polynesians. Nilishaletaga Uzi kuwahusu kwenye ile ID yangu nyingine ya iliyopigwa life ban.

Nchi zingine za pacific ambao Wenyeji wao ni Polynesians ni Kiribati, Tonga, Hawaii (Marekani) , French Polynesians (Tahiti), Tuvalu, Vanuatu, Samoa, American Samoa na Wenyeji wa asili New Zealand.

Sijaelewa hiyo misamiati mkuu..
 
Interesting,maelezo zaidi kama unayo mkuu.
 
Back
Top Bottom