Fahamu kuhusu wazo la biashara

Aug 5, 2017
5
45
Maana ya wazo la biashara
Kabla mtu hajaanza biashara, huwa anaanza kupata wazo la nifanye nini? Mawazo haya hupitia hatua kuu mbili:

1. Hatu ya kwanza
Mawazo mbalimbali humiminika kichwani kwa mfano: sijui jinsi ya kuanzisha duka, sijui kuuza nyama, sijui kufanya usafi. Mawazo ya namna hii huitwa mawazo ghafi kwani hayajachujwa. Pamoja na hayo, mawazo haya hayajafanyiwa uchunguzi wa awali kama yatatekelezeka. Kama utaanzisha biashara katika hatua hii, uwezekano wa kuanguka ni mkubwa.

2. Hatua ya pili
Wazo ghafi hutathiminiwa, na kama litaonekana kuwa linaweza kutekelezeka kuwa biashara kamili huitwa wazo muafaka. Pamoja na kuwa na wazo muafaka, mafanikio ya biashara hutegemea uwezo wa mtekelezaji au mtafutaji.

Kubuni wazo la biashara ni muhimu kwa mtafutaji kwasababu sababu zifuatazo:
 • Ni hatua ya kwanza kabla ya kuanza biashara yoyote ile.
 • Ni muhimu ili kufanya biashara ifanikiwe.
 • Mara kwa mara wateja hubadilika na kupendelea viu vingine ambavyo ni tofauti na vile vilivyopo.
 • Mabadiliko ya tekinolojia ni endelevu.
 • Athari zinazoikabili biashara yako.
 • Ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
 • Kutokana na mianya na nyanja za biashara pindi zinapojitokeza.
 • Hali duni ya maisha.
 • Ongezeko la mahitaji ya watu
Namna ya kupata wazo la biashara
Mawazo mengi ya kuanzisha biashara yoyote huanzia au hutokana na mambo yafuatayo:
 • Uzoefu kutoka katika familia.
 • Kuhamasika kutokana na kutembelea maonyesho ya biashara wilayani, mikoani, na hata kimataifa.
 • Kufanya ziara sehemu nyingine za nchi za nje na kuona watu wengine wanavyofanya.
 • Kuona kwenye luninga na kusoma katika magazeti pamoja na majarida yanayoeleza mambo ya biashara.
 • Kujiunga na vikundi, jumuiya na hata vilabu mbalimbali vya biashara.Upenzi wa vitu mbalimbali.
 • Matukio kama vile gharika au majanga.
 • Hali ya uchumi inaweza kumfanya mtu aingie kwenye biashara ili aweze kupata faida ya kumudu maisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom