griffin griffith
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 549
- 442
Watafiti wa Taasisi ya Pine Street, ambayo inashughulikia utafiti kuhusu kansa, wanasema kwamba ubongo na pua ya mbwa zinapofanya kazi pamoja zinafanyiza “mojawapo ya vifaa tata zaidi vya kutambua harufu duniani.” (soma hapaStudy Reveals Dogs Can Smell Cancer in Patients' Breath).
Mtafiti kiongozi wa zoezi hilo la utafiti aitwae Michael McCulloch ,anasema mbwa ana uwezo wa kutambua harufu itolewayo na cells zilizokumbwa na ugonjwa wa kansa(cancers hidden beneath the skin can be detected simply by [dogs] examining the odors of a person's breath,")
Inasemekana cells za mwili zilizoathirika na saratani (cancer) zinatoa harufu ambayo pua za binadamu haziwezi kuhisi, inasadikika harufu hiyo husababishwa na benzene compounds, japo haijathibishwa rasmi nini kinasababisha cells zenye saratani kutoa harufu.
Hivyo Watafiti wa Taasisi ya Pine Street, ambayo inashughulikia utafiti kuhusu kansa, wanasema kwamba ubongo na pua ya mbwa zinapofanya kazi pamoja zinafanyiza “mojawapo ya vifaa tata zaidi vya kutambua harufu duniani.” Wanasayansi wanajitahidi kubuni “pua” ya kielektroni inayoweza kutambua kuwepo kwa mabomu, dawa za kulevya, na magonjwa, kutia ndani kansa.
KWANINI MBWA ANA UWEZO MKUBWA HIVYO:
1. Pua ya mbwa ina unyevunyevu kwa hiyo, inaweza kunasa harufu kwa urahisi zaidi.
2. Pua ya mbwa imejigawa mara mbili—njia moja ni ya kupumulia, nyingine ya kunusa. Mbwa anaponusa
3. Hewa inaelekezwa upande wa pua wenye vipokezi vya kutambua harufu.
4. Sehemu ya pua ya mbwa iliyotengwa kwa ajili ya kunusa inaweza kuwa na ukubwa wa sentimita 130 za mraba au zaidi, ilhali sehemu hiyo kwenye pua ya mwanadamu ni sentimita 5 tu za mraba.
5. Idadi ya chembe za kutambua harufu za mbwa inaweza kuwa mara 50 ukilinganisha na zetu.
Hayo yote yanamsaidia mbwa kutofautisha sehemu mbalimbali zinazofanyiza harufu fulani. Kwa mfano, wataalamu fulani wanasema kwamba wanadamu wanaweza kunusa supu, lakini mbwa anaweza kunusa kila kiungo kwenye supu hiyo.
Una maoni gani? Je, uwezo wa mbwa wa kunusa ulijitokeza wenyewe? Au ulibuniwa?