Fahamu kuhusu utajiri wa kishirikina

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,907
6,700
Ninaposema utajiri wa kishirikina nadhani sio kitu kigeni, kwani wengi tushapata kusikia stori mbalimbali zilizozagaa mtaani kuhusu utajiri wa namna hii.

Watu wengi hupenda kujua kuhusu mambo haya. Leo nataka nizungumzie baadhi tu ya zina za utajiri huo na jinsi unavyofanywa.

Sikushauri ufanye bali naandika tu ninachojua kuhusu haya mambo.

Utajiri wa kujitoa kafara mwenyewe
Katika njia hii ya kuutafuta utajiri wa kishirikina ni lazima mhusika akubali kujitoa kafara yeye mwenyewe.
Katika utoaji huo wa kafara kuna njia nyingi ila tutaangalia njia ya kuku.

Katika njia hii hapa baada ya mhusika kuelezwa na akakubali kuwa atapata utajiri wa kutosha na kafara ni yeye mwenyewe, analetwa kuku ambae amekaa muda mrefu bila kupatiwa chakula. Mhusika anakabidhiwa kiasi kingi cha punje za mchele na atatakiwa ammwagie kuku huyo huku wakiwa wanahesabu punje ambazo atakula kuku huyo.

Hapa kinachoendelea ni kuwa idadi ya punje za mchele atakazokula kuku huyo ndio idadi ya miaka ambayo utaishi baada ya kupewa utajiri na ukifika huo muda wanakuchukua unafariki Duniani na unaingia mkataba kwenye ulimwengu wa giza.

Wakati mwingine hutokea kuku akala punje nyingi sana hapo ni lazima utafarijika, lakini pia wakati mwingine kuku huweza kuichukua punje moja na akaikata katikati na akala kipande tu. Hii inamaanisha una miezi 6 tu ya kuishi na utajiri huo.

Utajiri wa kufuga nyoka mkubwa (Jini)
Katika njia hii baada ya kuafikiana na mtaalam, atakukabidhi kamba kubwa. Kamba hiyo unatakiwa ukaiweke kwako kwenye chumba cha peke yako ambacho hakiingiwi na mtu yeyote zaidi ya wewe tu.

Kamba hii itageuka nyoka mkubwa na nyoka huyu chakula chake ni damu za watu. Kwakuwa utakuwa na vyombo vya usafiri vya kutosha chakula chake kitatokea hapa.

Ikifika wakati wa kumpatia damu unasababisha ajali na damu inanywewa na kiumbe huyo, huku anaendelea kukuneemesha kwa kukupatia kipato zaidi na zaidi.

Hata usipofanya kazi yoyote ukiingia kwenye chumba hicho unazoa pesa kama unazoa taka!
Ila ukikosea masharti utajuta na kusaga meno.

Utajiri wa kuishi na mwanamke wa kijini
Huu pia ni sehemu ya utajiri wa kishirikina. Utapatiwa mwanamke jini ambae utaishi nae kama mke na mume (bila wengine kumuona) Atakupa penzi kama anavyokupa binadamu mwenzako na atakuridhisha kwa kukata kiu yako ya kimahaba kabisa lakini ana masharti usioe au kuwa na mahusiano na mwanamke/mwanaume mwingine yoyote, usivute bange, sigara au matumizi ya vilevi, uwe msafi muda wote na masharti mengine ni siri yenu wawili.

Utajiri wa kumtoa kafara kipenzi chako (wazazi, ndugu)
Katika njia hii ni sharti ukubali kumtoa kafara mtu unayempenda zaidi katika familia. Jinsi ya kumuua sio kazi yako, kazi yako ni kukubali tu. Alafu mwenyewe watawala wa ulimwengu wa giza watajua jinsi ya kummaliza na kuonekana kama amekufa kifo cha kawaida tu.

Baada ya hapo mambo yako yatabadilika na huyu ndugu yako utakuwa unaonana nae na ndie atakuwa anakupa pesa unazohitaji. Katika kumtoa kafara ndugu yako unaweza kupewa chupa mbili nzuri ukaambiwa uchague moja unayoipenda kuliko nyingine, ile utakayochagua ujue umemchagua mtu unayempenda.

Baada ya hapo utaambiwa uvunje kwenye jiwe na nyumbani atafariki na hutotakiwa ulie!

Mimi sio mfanyaji tafadhali usinitafute kwa ajili ya utajiri.
 
Hahahaa umeona eeh.
Bora za halali hata zikitoshea kula mihogo tu fresh.
Sio una mabulungutu ya hela af hutakiwi kulala kitandani, asa raha ya pesa iko wapi.
Si umeona Sasa, yaani hata wewe niwe nakuangalia kwa macho.

Hapana aisee
 
Back
Top Bottom