Fahamu kuhusu njia ya kupunguza uzito kwa kukata utumbo na madhara yake

Rahma Salum

Member
Sep 7, 2020
30
59
Njia hii kitaalamu inaitwa “Gastric bypass”. Ni aina ya upasuaji unaosaidia mwili kupungua kwa kubadilisha namna ambavyo tumbo na utumbo mdogo unashughulikia chakula. Upasuaji huu hulifanya tumbo kuwa dogo na kupelea tumbo kupokea kiasi kidogo cha chakula.

Baada ya kukatwa na kupunguzwa kwa sehemu ya utumbo, chakula hakitafika katika baadhi ya sehemu hizo zilizoondolewa (tumboni na katika utumbo mdogo) ambazo ndio sehemu zinazochukua chakula. Kutokana na hili mwili hautapata "calories" kutoka katika chakula unachokula.

Upasuaji huu huwa na hatua mbili. Moja, Kupunguza ukubwa wa tumbo na pili, Ku-bypass chakula kutoka katika njia yake ya kawaida. Baada ya hatua hizi mbili mtu hula chakula kidogo tofauti na awali.

Historia inaonesha upasuaji wa kwanza wa Gastric bypass ulifanyika Uhispania katika karne ya 10. Miaka ya 1990 njia hii ya upasuaji ilianza kuwa maarufu na kufanikiwa kupunguza ukubwa wa tumbo kwa asilimia 90.

Moja ya shida kubwa inayowakumba watu waliofanya Gastric bypass ni utapiamlo na upungufu wa madini ya calcium, iron, zinc, Vitamin B12, protein, Vitamin A na folate. Kutokana na mwili kushindwa kuchukua aina ya vyakula vyenye madini hayo.

Vilevile kutokana na mwili kushindwa kunyonya virutubisho vizuri hupelekea magonjwa kama “Anemia” na “Asteoporosis”.

Kupunguza utumbo mwembamba husababisha mwili kushindwa kumeng’enya vyakula vigumu na kupelekea kupata shida katika kumeza na mara nyingine hupelekea hadi kutapika.

Miongoni mwa madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na Gastric bypass ni ugonjwa wa Ngiri “hernia” na tatizo la damu kuganda “blood clot” mara nyingi huanzia miguuni kuelekea kwenye moyo. Madhara haya hutokea kwa nadra sana.

Gharama ya upasuaji huu ni zaidi ya shilingi milioni 50 kwa India.

Chanzo: Mtaalamu wa vipimo maabara Festo D Ngadaya Tanzania na National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases (NIH) U.S
 
Utumbo unashineka kwanii

Vipi kuhusu ngozi ya tumbo maana ikikuwa imetanuka haitoning'inia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom