KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
FAHAMU KUHUSU MITEGO MITATU HATARI YA KICHAWI NA JINSI YA KUIEPUKA.
Wachawi wengi hutumia mbinu mbalimbali katika kufanikisha mipango yao ya kichawi kwa watu walio kusudia kuwadhuru kwa uchawi.
Katika kufanikisha hilo, wachawi hutumia mbinu na mitego mbalimbali ya kichawi. Miongoni mwa mitego hiyo ni ya kawaida kabisa ya kichawi ni pamoja na mchawi kukukaribisha chakula ama kinywaji ambacho kimewekwa uchawi ama kukupitisha katika njia ambayo imewekwa tego la kichawi na kadhalika.
Sitaizungumzia sana mitego ya aina hiyo hapo juu kwa sababu inajulikana na wengi na ni rahisi kubaini kuwa unategwa kichawi.
Leo nitaizungumzia mitego mikuu mitatu ambayo watu wengi hawaifahamu.
UCHAWI WA MTEGO WA SHILINGI
Uchawi wa mtego wa shilingi ni uchawi unao fanya kazi ya kufunga ridhiki ya mtu na kumfilisi kabisa.
JINSI INAVYOKUWA :
Ili mchawi afanikiwe kufunga ridhiki ya muhusika wake kwa kutumia aina hii ya uchawi ni lazima afanikiwe kupata hela yoyote yenye thamani ya chini sana kutoka kwa mhusika wake. Hela hiyo ni lazima isiwe ya karatasi na ni lazima iwe hela yenye thamani ndogo sana.
Huwa inakuwa hivi, mzee mmoja unae muheshimu sana mtaani kwenu ama kijijini kwenu atakufuata na kukuomba umsaidie shilingi hamsini, au shilingi mia au shilingi mia mbili (Miaka ya nyuma walikuwa wanaomba shilingi, thumni, sh.kumi au sh.tano au shilingi ishirini zile za chuma,ambazo kwa sasa hazipo tena kwenye mzunguko wa fedha.)
Mzee huyo atakwambia ana anataka kununua kahawa au ugoro na ana shida na shilingi hamsini tu. Kama sio mzee basi anaweza kutumwa hata mtoto mdogo na kukwambia “ Uncle naomba sh. Hamsini nikanunue pipi n.k.
Ukimpa shilingi hamsini, utakuwa umecheza bonge la
blanda. Shilingi hiyo hamsini itakwenda kufanyiwa uchawi
mbaya sana ambao siwezi kuelezea hapa namna
unavyo fanyika. Matokeo ya uchwai huo ni kwamba ridhiki yako
itafungwa kabisa, utakuwa unashika sh. Hamsini hamsini tu, thamani yako itakuwa sawa sawa na thamani ya shilingi hamsini, na mwisho wa siku utafilisika kabisa na kurudia maisha ya chini kabisa.
JINSI YA KUJIEPUSHA NA UCHAWI HUU :
Njia bora kabisa ya kujikinga na uchawi ni kuuepuka. Hivyo basi kujikinga na uchawi huu, fanya yafuatayo :
1. Mtu akikuomba hela yoyote yenye thamani ya chini kama vile sh. Hamsini, mia, au mia mbili, mkatalie usimpe kabisa.
AU
2. Mpe shilingi elfu kumi. wengine ukiwapa elf kumi wana kataa wanakwambia kachenchi basi we kataa
MTEGO WA NYOKA.
Lengo la mtego huu ni kumchukua mtu msukule ama kumuua kabisa kwa njia ya uchawi. Vile vile mtego huu unatumika kuua vitoto vichanga, kumuua mwanamke mjamzito au kunyofoa mimba ya mwanamke mjamzito na kumfanya asizae.
Mtego huu ni wa hatari sana kwani kuubaini ni vigumu sana na kwa jinsi unavyo tumwa ni vigumu sana kuchomoka , yaani lazima uingie mtegoni.
JINSI INAVYOKUWA :
Mtego huu mara nyingi huwa unakuja katika sura kuu
tatu :
1. Sura Ya Kwanza : Jini aliye vaa sura na umbo la nyoka huingia hadi chumbani
kwako, au hukutokea bafuni au chooni . Kwa vyovyote vile lazima utatafuta njia ya kumuua, ukimuua tu huyo nyoka na wewe ndio unakuwa
mwisho wako hapo, kwa sababu utakuwa unajiua mwenyewe. Baada ya kumuua nyoka huyo utaugua kwa sana na mwisho wa siku utakufa . Nyoka huyo wa kichawi anakuwa ameunganishwa na nafsi yako mwenyewe , hivyo kitendo cha wewe kumpiga nyoka huyo wa kichawi unakuwa unainyonga nafasi yako mwenyewe bila kujijua. NI HATARI SANA!
2. Ndugu yako ama jirani yako ( ambaye lazima atakuwa mwanamke) atakuja nyumbani kwako na kukwambia kuwa kuna nyoka mkubwa ameingia nyumbani/chumbani kwake, sasa ameshindwa kumuua au anaogopa kumuua, na nyumbani kwake kuna watoto tu, hivyo anakuomba ukamsaidie kumuua huyo nyoka. Ukienda kumuua huyo nyoka, umejiua mwenyewe. Utaugua sana na mwisho wa siku utakufa.
3. Ukiwa na mgonjwa ambaye amelazwa nyumbani , atatokea nyoka karibu na kitanda chake na wewe ukiwa kama mwanaume katika familia hiyo, utalazimika kwenda kumuua nyoka huyo ili asimdhuru mgonjwa wako…Ukisha muua tu huyo nyoka, mgonjwa wako hatomaliza siku saba atakufa.
4. Mke wako akiwa anakaribia kujifungua, nyoka huyo atajitokeza katika chumba unacholala wewe na mke wako au katika eneo lolote atakalo kuwapo mke wako. Ukiwa kama mwanaume, kwa vyovyote vile utalazima kumuua nyoka huyo. Ukifanya hivyo, mke wako atakufa wakati wa kujifungua. Au atazaa mtoto aliyekufa na yeye ataugua sana na mwisho wa siku atakufa.
5. Mke wako akiwa amejifungua mtoto au watoto, nyoka huyo ataonekana katika chumba ambacho watoto wenu watakuwa wamelala, eidha peke yao au pamoja na mama yao. Kwa vyovyote vile, utalazimika kwenda kumuua huyo nyoka, ukifanya hivyo, watoto wako wataugua sana na mwisho wa siku watakufa.
UFANYEJE NINI KUEPUKANA NA MTEGO HUU ?
1. Mtu akikuita uende kuua NYOKA usiende.
2. Kwa kuwa ni vigumu sana kujua kama nyoka aliye mbele yako ni halisi au nyoka wa kichawi unapaswa kutumia dawa ya kujikinga na nyoka wa kichawi. Dawa hii yenye nguvu sana haitakukinga tu na nyoka wa kichawi bali pia itakukinga na nyoka wengine wa kawaida. Ukitumia dawa hii, basi kwanza nyoka wa kichwai hawataweza kuingia nyumbani kwako na hata kama ukiwekewa mtego wa kichawi, utamuua nyoka huyo na hutopata madhara yoyote.
MTEGO WA ULIMI :
Uzima na umauti upo ndani ya ulimi wa mwanadamu.
Wachawi wa nchi wanapotaka kumuua mtu kichawi hufanya mambo mbalimbali ya kichawi. Baada ya kufanya ulozi wao ,moja kati ya mambo makubwa wanayo yafanya ni kutengeneza hati ya kichawi ya kifo cha
mlengwa wa uchawi. Hati hiyo ya kichawi itasainiwa na mlengwa mwenyewe kabla ya kutekelezwa bila ya mlengwa mwenyewe kujijua kama ana saini hati ya kifo chake mwenyewe.
KWA NINI NI LAZIMA MLENGWA ASAINI HATI YA KICHAWI YA KIFO CHAKE MWENYEWE :
Kila binadamu ana ye ishi duniani ameletwa na Mungu kwa ajili ya ku timiza mission maalumu. Binadamu huyo hawezi kurudi kwa Mungu bila kutimiza mission hiyo, hivyo ni vigumu sana kwa wachawi kumuua kichawi mtu yoyote Yule bila ya ridhaa yake mwenyewe ama bila ushirikiano wake mwenyewe.
Hivyo basi wachawi hufanya namna au kutengeneza mtego utakao mfanya mlengwa kutia saini kwenye hati ya kifo chake mwenyewe bila kujua kama anajiua mwenyewe.
JINSI INAVYO KUWA
Siku saba kabla ya mtu Fulani kuchukuliwa kichawi. Maneno ya kichawi yatakayo kuwa yameandikwa kwenye sura ya nafsi ya mlengwa huwa kama ifuatavyo :
Kwa mfano kama wewe jina lako unaitwa “ MADEVU” na imekusudiwa uwe haupo duniani ifikapo siku ya alhamisi ya kesho. Maneno yatakayo kuwa yameandikwa kwenye sura ya nafsi yako ni “ MADEVU BIN (JINA LA MAMA AKO ) SIKU YA ALHAMISI YA KESHO TAREHE 04/09/2025 HATOKUWEPO DUNIANI “Ili maneno hayo yakamilike, ni lazima MADEVU mwenyewe akiri kwa kinywa chake kuwa siku hiyo hatokuwepo.
WANAVYO FANYA WACHAWI
Kwa mfano mchawi anajua kuwa , wewe Madevu ambaye una miliki tuseme duka la spea pale Kariakoo, dini yako ni msabato na siku za Jumamosi huwa haufanyi kazi.
Siku moja kabla ya “ kifo” chako, mtu mmoja atakupigia simu na kukwambia kuwa, kesho atakuja dukani kwako kuchukua mzigo hapo, halafu atamalizia kwa kukuuliza “ UTAKUWEPO ?” Kwa vyovyote vile lazima utamjibu “ KESHO SINTAKUWEPO !”. Hapo ndio utakuwa umesaini hati ya kifo chako mwenyewe. Maneno yako yatakwenda kutumika dhidi yako mwenyewe.
Kwa ufupi tu ni kwamba, katika mtego huu, utaulizwa swali “ utakuwepo?” ambalo kwa vyovyote vile majibu yake yatakuwa “ SINTOKUWEPO “
KUJIKINGA NA UCHAWI HUU :
Kujikinga na uchawi huu, epuka sana kutumia neno “ SINTOKUWEPO!” Badala ya kujibu “sintokuwepo” jibu kwa kutaja sehemu utakayo kuwepo.
Kwa mfano,hapo Bwa. Madevu atatakiwa kujibu “ SIKU YA KESHO NITAKUWA KANISANI” AMA ANAWEZA KUSEMA NITAKUWA NYUMBANI