Fahamu kuhusu Bangungut

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,704
Bangungut ni neno la kiphilipino , kwa kiswahili hujulikana kama JINAMIZI, ambapo huaminika ni jitu kubwa, zito lenye mfano wa mtu ambalo hukaa kifuani kwa mtu wakati anapo kuwa amelala haswa wakati wa sleeping paralysis.

Hali hii inatokea pale mtu unapokuwa umelala na unajitambua lakini mwili unakuwa mzito na hauwezi kunyanyuka, huwa wengi ikisha watokea hali hii hujawa na hofu na kuupelekea ubongo kutengeneza mawazo yanayo ambatana na picha kuwa kunakitu cha kutisha ...sasa ukisha tengeneza hiyo picha machoni mwako utaona "Bangunguti/ Jinamizi" lina kuja au limekukalia kifuani na kukukaba kitu ambacho kina fanya mwili kuwa mzito haswa kifua na pumzi inakuwa ya tabu sana.

unambiwa hili Bangungut ni hatari kwasababu lina 10% ya kukusababishia kifo, hususani pale unapo shtuka ghafla ukiwa katika hali hiyo hivyo inauwezo wa kukusababishia heart attack (mshtuko wa moyo) na kufa , ndomana muda mwingine unamkuta mtu amelala salama lakini Asubuhi Mnamkuta Amefariki.

Hii hali husababishwa na baadhi ya viungo wakati wa usiku kupararaizi na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Endapo kama hali hii ya Bangungut inakutokea ,usiangaike inakubidi ufumbe macho kwa utulivu kisha chezesha kidole chako chochote , utakuwa salama ....pia unashauriwa kujiepushe sana na stress wakati unapokuwa unaenda kulala.

FB_IMG_1654035803908.jpg
 
Halaf unakuwa unasikia kama mlango unafunguliwa mtu anapita lakin kugeuka umuone haiwezekani
Yaaani acha kabisa ile hali ilikuwa inanipata sana miaka fulani,alafu nilikuwa nalala kitanda cha juuu. Yaani unamkaa hoi km umetoka kukumbiza mwizi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom