Fahamu kuhusu andalio la somo

Fahamu kuhusu andalio la somo

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,861
Reaction score
6,822
Ieleweke shughuli zote zinazofanyika darasani zinapaswa kuwa katika mpango unaoakisi Falsafa ya Elimu.

Mipango katika ngazi za juu inaweza pia kuwa kupangwa na kusimamiwa na Sera ya Elimu.

Kwa ngazi ya shule mipango inaweza kuonekana kwenye"
syllabus"

Ngazi ya Darasa tunaweza tukaiona kwenye Maazimio ya Kazi"Schemmes of work"

*Lakini kwenye utendaji wa kila siku tunakutana na ANDALIO LA SOMO*

Na hapa ndipo tunapopaswa kupaangalia sana Waalimu kwa sababu ndipo panapotuhusu kila siku katika ufundishaji wetu.

Baadhi ya Waatalamu wa masuala ya Elimu na ufundishaji wanadai kuwa *"Kushindwa kuwa na mpango wa kufundisha ni sawa na kushindwa kufundisha"*

Kwa maana hiyo kutokuwa na Andalio la somo au Maandalio ya masomo ni kushindwa kutekeleza wajibu wetu wa kila siku.
Ikiwa Taifa linajiwekea mipango kwa ngazi yake basi hatuna budi kuwa na mpango ili kuweza kutimiza mpango mkubwa wa Taifa.

*ANDALIO LA SOMO NI NINI?*

_Ni ule mpango/muongozo wa kiufu dishaji anaouandaa Mwalimu ili kufikia matokeo tarajiwa katika kipengele mahsusi na katika siku husika_•

Mpango huo ndiyo unaooonesha muelekeo wa kiufundishaji wa Mwalimu mahususi katika kipengele mahsusi ndani ya siku mahususi.

*Ni kwa nini ni muhimu kwa Mwalimu kuwa na Andalio/Maandalio ya somo au masomo?*

Zipo sababu nyingi mno zinazodhihirisha umuhimu wa Mwalimu kuwa na Andalio lakini Sababu hizo zinaweza kuingia ndani ya sababu zifuatazo:

_1.Wanafunzi kubaini kama Mwalimu alojiandaa au hakujiandaa_

_2.Kwa waalimu Andalio hutoa picha au umbile la ufundishaji_
Kama vile tunavyowatathmini wanafunzi kwa kuwapa maswali ya aina mbalimbali kisha kuwapa alama"grade" vivyo hivyo maandalio au andalio la somo linaweza kabisa kutumika kumtathmini Mwalimu.

*Kwa msingi huo basi ni dhahiri kuwa Mwalimu anaweza kabisa kupimwa kutokana na namna anavyoandaa Andalio la somo*

*_Ni kwa jinsi gani Mwalimu anaweza kuandaa andalio la somo?_*
Mambo yafuatayo ni muhimu sana kuyabaini wakati wa kuandaa.

1.Kutambua aina ya Wanafunzi unaowafundisha:Ni vyema sana Mwalimu kutambua umri au rika tamaduni za jamii walikotokea Watoto pia mitindo yao ya usomaji(learning styles)

2.Weka malengo na malengo mahususi ya kipengele au mada unayotaka kwenda kuifundisha.

2.Unapaswa kutambua pia utatumia Muda gani(how long will it take)

3.Unapaswa upange namna ufundishaji utakavyofanyika kwa mfano ni wakati upi utawagawa wanafunzi kimakundi? Je utatumia zana zipi?

4.Unapaswa pia kubashiri ni matatizo yapi yanaweza kutokea?
*Mwalimu mzuri ni yule anayeendana na mabadiliko*
Victor MlakiJr
 
Andalio la "SOMOW". Mwalimu wa somo gani anayeshindwa hata kuandika neno "Somo" ataweza kuandaa lesson notes kwa lugha ipi iwapo hata lugha ya upili inamshinda?...
Tuna safari ndefu.
 
Back
Top Bottom