Uchaguzi 2020 Fahamu kituo cha kupigia kura

Mjasi1

Member
Sep 1, 2020
68
25
TAMBUA KITUO UTAKACHOPIGIA KURA 28 OKTOBA 2020​

Kama tujuavyo mwezi huu wa Oktoba, tarehe 28 kuanzia saa 1:00 mpaka saa 10:00 jioni ni siku muhimu sana kwa Watanzania.Kwani watanzania watachagua viongozi wao wanaowataka ambao ni Rais,Mbunge na Diwani kupitia Uchaguzi Mkuu,ambao utafanyika kila baada ya miaka mitano(5).Kwamujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi orodha ya wapiga Kura itabandikwa katika kila kituo cha Kupigia Kura siku nane(8) kabla ya siku ya Uchaguzi.

Je,ni namna gani tunaweza kutambua vituo vyetu vya kupigia kura?Kwamujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi mpiga kura unaweza kutambua kituo chako cha kupigia kura kwa kufuata utaratibu ufuatao:

1.Kwa kutumia mfumo wa Voters’ Interaction System (VIS).

Kwa kufanya yafuatayo:
  • Piga namba *152*00#.
  • Chagua namba 9 (Uchaguzi Mkuu)
  • Chagua namba 1(Uhakiki wa taarifa za mpiha kura)
  • Ingiza namba ya kadi ya Mpiga Kura bila ya kuweka herufi (T) wala (-)
  • Utapata ujumbe “Ombi lako limepokelewa na linashughulikiwa”
  • Utapokea ujumbe mfupi (SMS) wenye taarifa zako na Kituo cha Kupigia Kura
2.Kwa kutumia Tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (www.nec.go.tz).

Kwakufanya yafuatayo:
  • Tafuta www.nec.go.tz katika mtandao
  • Bofya sehemu iliyoandikwa “Uhakiki”
  • Bofya sehemu iliyoandikwa “mfumo wa uhakiki taarifa za mpiga kura”
  • Ingiza namba ya kadi ya Mpiga kura.mf.T-####-####-###-#
  • Bofya sehemu iliyoandikwa “Tafuta” na taarifa zako zitaonekana
3.Kwa kupitia Kituo cha Huduma kwa Wapiga Kura (Call Centre)

(i) Piga simu namba 0800112100 (Bure) na kupata usaidizi wa taarifa zako.

Wananchi tuhakikishe tunatambua Vituo vyetu tutakavyokwenda Kupigia Kura mapema ilituweze kushiriki vyema Katika zoezi la Upigaji Kura siku hiyo ya kipekee kwa Taifa letu.
 
Back
Top Bottom