Buhaya Empire
Senior Member
- Aug 3, 2016
- 116
- 299
Habari,
Lengo la uzi huu ni kufahamishana historia yetu ambayo katika upande wa makabila imekuwa vigumu sana kuipata kulingana na kukosekana kwaa taarifa za moja kwa moja zilizohifadhiwa kuhusu uwepo wetu (waafrika kiujumla)
Historia hii haina lengo la kubeza wala kuchafua kabila tajwa. Na nina iman ndugu msomaji historia hii wanaoijua ni wachache sana.
Wakerewe ni kabila linalopatikana katika mkoa wa Mwanza (Nyanza). Ikumbukwe kwamba ukelewe ni muunganiko wa visiwa vingi vodogovidogo na si kimoja kama watu wengi wasiofatilia geographia ya nchi wanavofahamu.
Pamoja na kwamba Ukelewe imewekwa katika mipaka ya mkoa wa Mwanza lakini nataka ujue kwamba makabila yanayopatikana wilayani ukerewe yanashabihiana sana na kabila la wahaya wa mkoani Kagera.
Nini kilitokea?
Zamani za kale za mfalme wa Buganda "Kabaka" alitawala maeneo ya uganda ya leo kuja mpaka mkoa wa kagera ukanda wa ziwa Victoria na maeneo ya karibu. Ulikiwa ni moja ya falme zenye nguvu katika ukanda wa Afrika mashariki kabla ya kugawanyika katika koo tofauti hapo baadae.
Kabila la Wahaya lilikuwa ndani ya ufalme huu wa Buganda kabla ya kuwa wahaya wa Tanganyika waliojulikana kutawaliwa na mfalme wao aliyeiitwa Omukama.
Zamani za mfalme kabaka na baadae Omukama kwa wahaya palikuwa na utawala wa sheria iliyosaidia kutoa hukumu kwa makosa mbali mbali.
Sheria ya ufalme huu ilikuwa ni ya kushangazas kidogo..
Wao waliamini katika kuwatenga watu waliokutwa na hatia ya uhujumu wa ustawi wa amani na ushirikiano katika ufalme.
Moja ya mokosa yalioweza kusababisha mtu kutengwa ni pamoja na Uchawi.
Historia ambayo kwa sasa chanzo chale ni kabila la wahaya inasema kuwa watu walitengwa na kupelekwa visiwani na kuachwa pekeyao ikiaminika kwamba watakufa tu kwa kukosa msaada na mahitaji muhimu ya kimaisha.
Adhabu hii mpaka hivi leo kuna baadhi ya jamii za wahaya na hata ukerewe penyewe zinatekelezwa kwa siri kubwa.
Sasa basi.. Wakerewe ni jamii ambayo ilikuwa ni wahanga wa adhabu hii ya kutengwa na baadae wakafanikiwa kustahimili na kuzaliana mpaka leo hii wakati ambapo historia hii haifahamiki tena.
Fikiria jambo hili.. Asilimia 34.7 ya maneno ya kikerewe yanamaana au yanaeleweka kàtika kabila la wahaya.. Yaani katika kila maneno 100 ya kikelewe zaidi 34 yana maana pia katika lugha ya kihaya mengine yakiwa na utofauti wa Lahaja ya kiumbali.
Lakini tafakari pia, uchawi bado ni kosa la aibu na la kificho kikubwa sana katika kabila na jamii yote ya koo za wahaya waliopo Tanzania leo.. Ila ndugu msomaji nataka nikujuze kwamba Huko katika visiwa vya ukerewe uchawi ilikuwa ni sifa na watu waliona fahari kuwa na nguvu za kishirikina waziwazi katika jamii yao. Ni kweli uchawi upo kila sehemu lakini tatizo kubwa ni jamii husika inauchukulia vipi?
Mpaka leo hii Visiwa vya ukelewe vinasifika kanda ya ziwa kwa shughuri za ulozi wa kutisha hii ni kwa sababu wakaazi wake wa mwanzo walitengwa kwa sababu hiyo na swala la uchawi kama kawaida yake likawa ni swala la Urithi.
Nawasilisha.